Mwalimu Mkuu
Member
- Dec 26, 2010
- 62
- 39
ni mara nyingi nimekuwa nikijiuliza juu ya kiwango cha elimu kinachotolewa hasa katika taasisi zetu za elimu ya juu kama vyuo vikuu. kumekuwepo na idadi kubwa ya uandikishaji (addmission) jambo ambalo ukiliangalia kwa haraka unaweza kuona ni jema, kwani hata watoto wa maskini wanaweza kupata elimu walau ya chuo kikuu.
jambo linaloshangaza ni product inayotolewa na vyuo hivi sasa, juzi nilikuwepo eneo fulani ambalo watu walikuwa wanafanya usaili wa wafanyakazi, ilikuwa ajabu kabisa kwamba wanafunzi waliotoka katika vyuo kama UDSM ama UDOM hawakuwa na kipaumbele katika jopo la usaili, kwani wanadai wanafunzi hao wanaweza kuwa na GPA hata za point 5 lakini kiukweli ni wabovu katika fild walizosomea. kwa maan hiyo walipendelea kupata wanafunzi kutoka katika vyuo binafsi ambavyo kwa sababu binafsi sintovitaja.
hoja ni kuwa kweli vyuo vyetu hivi vilivyokuwa na heshima ulimenguni kama chuo cha Dar es salaam kinaweza kuwa na picha hii iliyopo kwa jamii? tunakuza elimu au tunaiua, vyuo havina vyumba vya mihadhara vya kutosha, osteli za wanafunzi zenye mahitaji muhimu, matatizo ya mikopo inayoandamana na migomo ya wanafunzi kwa kutaja machache
je elimu inakuwa au tunaiua?