Malisa Godlisten 23:08 7th September 2015
Leo ngoja niwasaidie jamaa zangu wa CCM
ambao wengi wao hawajui Hesabu. Tangu
Mgombea Urais wa UKAWA Mhe. Edward
Lowassa atangaze Elimu bure, kuna watu
wamekuwa wakiona huo kama muujiza.
Kwa kifupi zipo njia nyingi sana zinazoweza
kufanya Elimu kuwa bure kuanzia Shule ya
msingi hadi Chuo Kikuu. Leo ngoja niongelee
'alternative' moja.
Kwa mujibu wa TAMISEMI Tanzania ina jumla ya
shule za msingi 16,343 zenye wanafunzi 8.3 mil.
Kwa upande wa sekondari shule zimeongezeka
kutoka 531 mwaka 2005 hadi 4,576 mwaka 2014.
Idadi ya wanafunzi nayo imeongezeka kutoka
524,325 mwaka 2005 hadi 1,804,056 mwaka huu.
Kwa upande wa elimu ya juu, idadi ya vyuo
imeongezeka kutoka 26 hadi 54 kati ya mwaka
2005 hadi mwaka 2014 na kufanya idadi ya
wanafunzi wa vyuo vikuu iongezeke kutoka
wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi
200,986 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Hotuba ya bajeti ya wizara ya
Elimu na mafunzo ya ufundi ya mwaka
2014/2015, wanafunzi wa shule za msingi
wanakadiriwa kugharamia kiasi cha Sh.10,000/=
hadi 15,000/= kwa mwaka. Hii ina maana kuwa
wanafunzi wote wa shule za msingi Tanzania
wanahitaji Bilioni 80 waweze kusoma BURE.
Shule za Sekondari za Serikali zinakadiriwa kuwa
2,446 zikiwa na jumla ya wanafunzi 1,004,071.
Kati yao wanafunzi 185,652 ni wa Shule za
Kulala (Boarding), na wanafunzi 818,419 ni wa
shule za kutwa (Day).
Wanafunzi wa Shule za kutwa wanalipa ada TZS
20,000 kwa mwaka. So ukichukua 20,000 ×
818,000 utapata Bilioni 16.3. Wanafunzi wa shule
za Bweni wanalipa ada TZS 70,000/= kwa
mwaka. So ukichukua 70,000 × 185,652 utapata
Bilioni 11.2.
Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu wa vyuo
vya Serikal na vya binafsi wapo 200,986. Kati yao
wanafunzi 162,987 wanasoma Course za 'Social
Science, Law, Humanities, Education etc' ambao
ada zao hazizidi Mil.2 kwa mwaka. So chukua
162,989 × 2000,000/= utapata Bilioni 325.
Wanafunzi 37,997 wanasoma course za
"Science" kama Engineering, Udaktari etc na ada
zao ni zaidi ya Mil.3 kwa mwaka. So hawa
watahitaji Bil 113.5 kulipa ada ya mwaka mzima.
Fedha ya kujikimu pamoja na chakula (Meals &
Accomodation) inayotolewa kwa sasa ni TZS
7,000 kwa siku kwa mwanafunzi mmoja. Hivyo
basi mwanafunzi mmoja anapata Jumla ya
Shilingi 1,680,000/= kwa mwaka. Hii ina maana
kuwa wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu
ambao ni 200,986 wanahitaji Bil 337.
Fedha ya Utafiti (Research), Mafunzo kwa njia ya
vitendo (Field) na vitabu (Stationeries) hutolewa
jumla ya Shilingi 735,000/= kwa mwaka ambayo
hugawanywa kulingana na asilimia ya mkopo ya
mwanafunzi. Hivyo basi wanafunzi wote
wanahitaji Bil 147 kwa mwaka.
Ukijumlisha gharama zote hapo juu utapata jumla
ya Shilingi Bilioni 934 tu. Kwa lugha rahisi ni
kuwa ili kila mwanafunzi nchini asome bure
kuanzia Elimu ya msingi, sekondari na akifika
Chuo Kikuu alipiwe gharama zote bure kwa
asilimia 100%, serikali inahitaji kutoa Shilingi
Bilioni 934 tu kila mwaka.
Swali, Je hizi Bilioni 934 zinapatikanaje?
Ukisoma hotuba ya Bajeti ya wizara ya Maliasili
na Utalii kwa mwaka 2014 utagundua kuwa
Mlima Kilimanjaro peke yake unachangia karibu
Bil.800 kwenye pato la Taifa (Gross National
Income of $350 Milion).
Kwa lugha Rahisi ni kuwa tunahitaji Mlima
Kilimanjaro mmoja tu ili watoto wetu wasome
bure kuanzia shule ya msingi hadi Chuo Kikuu.
Yani tukiamua mapato yote ya Mlima Kilimanjaro
tuyapeleke kwenye sekta ya Elimu bila
kuchakachua, tutakua na uhakika wa kusoma
bure kuanzia shule ya msingi hadi Chuo kikuu. Je
hatuwezi??
Hapo hatujagusa Mbuga za wanyama, hatujagusa
Bandari, Madini, Gesi, Mazao ya misitu, Uvuvi,
Kilimo, Viwanda, etc. Tumegusa mlima
Kilimanjaro peke yake. Kama CCM wanaona
hawawezi wakae pembeni wanaoweza wafanye.!