Elimu bure hakuna, Serikali imekurupuka

Elimu bure hakuna, Serikali imekurupuka

Hiyo ni pesa ambayo moja ya shule imepata kwa shule ya msingi sijapiga hesabu ya bil 18 hii ni hesabu tu ya kiasi gan shule imepata waraka wa elimu umefuta michango yote kwa shule za msingi sasa hapo hiyo laki mbili itatosha kweli kuendesha shule kwa mwezi???
Hivi unapopiga uongo na ukijua kabisa unapiga uongo na kufanya majungu moyoni unajisikiaje? Hiyo shule mahitaji yake ya mwezi kabla ya elimu bure uliyafahamu? Hiyo shule ina wanafunzi wangapi? Hiyo shule gharama zake za uendeshaji ni shilingi ngapi kwa mwezi? Siyo kubwabwaja tu kama hayawani ili mradi useme, sema mambo yenye mantiki na uliyoyafanyia uchunguzi wa kina si kuendeshwa na hamu ya kuona jitihada zinashindwa
 
Siku zote wachawi ni adui wa maendeleo. Wachawi kama huyu mleta mada hawastahili hata kuishi. Ni wale ambao kwa mikoa ya wenzetu wanaangamizwa huku wanajiona
punguza gongo we jamaa shule zimegawiwa pesa kulingana na mahitaji yao sasa unapopinga kuwa hata na uthibitisho wa unayo pinga.
 
bilion 18 sio kila shule nafahamu hilo, ila inatolewa bilioni 18.6 kila mwezi na hakuna necta kila mwezi, mimi siungi mkono kama inatosha au haitoshi na serikali inapochemsha ni vizuri kuikosoa kwa nguvu, point yangu ni kuwa unapokuja kupost mada jamiiforums post kitu ulichokifafanua vizuri kwa facts& figures, ili uonekane una point, sio kusema vitu nusunusu, au vitu ulivyovifanyia utafiti nusu alafu unajifanya unajua full
Soma.post #59
 
Dah! Kuna watu wanakurupuka sana. Sijui huyu mleta mada kaandika wakati amepakatwa au ameinama! Yaani nawaza tu wadau.

jamani kumbukeni hizo hela zinatolewa fidia ya ada kwa idadi ya wanafunzi hivyo msikimbilie kushutumu huenda ni kweli kama shule hiyo inawanafunzi wachache
 
Mbona mnakuwa wakali sana kila anayehoji haya mambo!!?

Lengo ni kujadiliana na pengine kuishauri serikali namna bora ya kutekeleza hii sera ambayo kwa vyovyote vile ni nzuri na hakuna anayeipinga.

Na tukunbuke pia kuwa utekelezaji wake ndo tu umeanza na ni kitu kilichokuwa nje ya utaratibu wa kibajeti. Kwa hiyo ni lazima tu kutakuwa na mapungufu ya hapa na pale ktk utekelezaji wake!!

Binafsi nimemuelewa mleta hoja na
wewe pia nimekuelewa.
Ni kwamba hizi 18.6bn ni kwa ajili ya
shule zote za msingi na sekondari kwa
mwezi desemba, 2015.
Kwa mujibu wa magawanyo wa fedha
hizo ni kwamba;

Kwa sekondari kidato cha I -IV kila mwanafunzi atalipiwa na serikali
Tshs. 45,000 kama fidia ya ada ambayo ilipaswa kulipwa na mzazi wa mwanafunzi.

Kwa shule za msingi kila mwanafunzi atalipiwa na serikali Tshs. 10,000= kwa mwaka.

Kwa utaratibu wa serikali ni kwamba hizo fedha zitakuwa zinatolewa kila mwezi kwa kutumwa moja kwa moja ktk shule husika, hazitalipwa kwa mkupuo mmoja!!

Sasa kwa mfano kama shule ya sekondari X ina wanafunzi 145 kidato cha I - IV (nyingi ya shule za vijijini zina idadi ya wanafunzi inayo range kati ya 90 - 350) maana yake shule hii shule ktk mgawa wa mwezi desemba imepata;

45,000 ÷ 12 × 145 = Tshs. 543,750/=

Maana yake haya ndiyo matumizi ya shule hii kwa mwezi January, 2016 mara shule zitakapofunguliwa!!

Hii ndiyo hoja nadhani nilivyomuelewa mleta mada. Swali lake ni kwamba, hizi pesa zinatosha kuendesha shule kwa mwezi??

Mimi binafsi sina jibu ktk swali hili kwa sababu kila shule ina mahitaji na bajeti yake ya mwezi, muhula na kwa mwaka mzima. Ninachoweza kusema ni kuwa inategemea na shule.

Kwa sababu kuna shule zina wafanyakazi (casual labours) ambao hawako ktk payroll la serikali na hulipwa na shule kama walinzi, wahudumu wa ofisi nk kulingana na vyanzo vya mapato ya shule husika iwe ni kutoka EK au michango ya wazazi kwa wakati ule kabla ya sera ya elimu bure kuanza. Pia kuna shule zingine vijijini hazina walimu wa kutosha especially wa sayansi na shule huajiri parttime teachers ambao hulipwa posho ya kati ya Tshs. 150,000 hadi 250,000 ili wanafunzi hawa wafundishwe

Hii kitu ni halisi wala si kuandika tu hapa. Mimi hapa naandika nikiwa Shinyanga na natembea sana vijijini. Kuna shule za sekondari ziko kwenye very remote areas na mazingira ni magumu sana to the extent kwamba walimu hupakimbia huko kila wanapopangiwa. Kuna shule moja iko wilaya ya Kishapu inaitwa Paji ina wanafunzi 123 wa kidato cha 1 - 4 na walimu 5 wote wa masomo ya Arts na language hasa Kiswahili ns History, Geography na Civics. Hakuna mwalimu wa Mathematics, physics, Biology na Chemistry.

Anachofanya mwalimu mkuu alikuwa anatafuta vijana wa walionaliza kidato cha sita na kusaidia kufundisha. Na huwezi amini kuwa kila mwaka mwalimu huyu hupeleka vijana wawili au watatu kidato cha tano (A'level). Sasa serikali ime consider hii kitu??

Na kuna shule zingine wala hazina watu wa namna hii kwa sababu kama ni walinzi au muhudumu wa ofisi ama mtunza bustani wote wanalipwa na serikali. Kwa hiyo ni wazi, shule kama hii pesa kama hii inaweza kutosha tu kwa mwezi japo kwa kubanana sana!

Kwa hiyo hii 18.6bn ni nyingi kwa kutamkwa kwa pamoja lakini zikishagawanywa mashuleni, picha halisi ya kitakachokwenda ktk kila shule ni kama nilivyoonesha hapo juu na kwa hakika kuna shule zinaweza kupata hata Tshs. 150,000 tu kwa mwezi!!!
EBANA MIMI SIJAWA MKALI NIMEULIZA NIPEWE MCHANGANUO, MIMI NAPENDA MTU AKILETA HOJA YAKE AILETE AKIWA AMEIFAFANUA VIZURI, SIO KUPOST KWA KIFUPI KAMA ALIVYOFANYA, AKIPOST HIVYO BASI ATEGEMEE MASWALI
 
Back
Top Bottom