Elimu Bora iko Wapi Kati Ya Tanzania,kenya Na Uganda?

Arnold Ndosi

Member
Aug 14, 2012
65
3
Mwana Jf Naja,
Jukwaani Napanda,
Ninataka Kujua,
Niondoe Ugiligili.

Tz,Kenya Na Uganda
Ni Ipi Inatisha,
Inatisha Kwa Elimu Bora?
Niambieni,nipate Fahamu.

Nina Rafiki Mkenya,
Pia Mganda,
Wote Kwa Wajisifia
Kitaaluma Eti Wanatisha

wanadai Afrika Mashariki
Elimu Yao Haipimiki
Kwa Ubora Haizidiki
Et,hawavutii Upande Wao?

Mtanzania Hapa Sina Moyo
Najiisi Poyoyo
Tena Kibogoyo
Wameniweka Dilemma.

2changie Wasomi,
Wanafalisafa,wanadini
Na Hata Wapenda Mapenzi.
jamani,ni Sisi Au Wao?

Mwamba Ngoma,yadaiwa
avutia Kwake Sana,
Tusiwe Wachekelea Donda
Tuseme Ukweli Adharani

Waganda wapewa Uhondo
Eti Kisa Wajua Kimombo! Je Twatongozwa Kwa Hilo
Na Tukubali Ka Mazuzu?

Wakenya Wasimetemete
Wala wasichekecheke
Kama Ndege Au K"kwete
Kwa Kupongezwa Uozo.
 
Mwana Jf Naja,
Jukwaani Napanda,
Ninataka Kujua,
Niondoe Ugiligili.

Tz,Kenya Na Uganda
Ni Ipi Inatisha,
Inatisha Kwa Elimu Bora?
Niambieni,nipate Fahamu.

Nina Rafiki Mkenya,
Pia Mganda,
Wote Kwa Wajisifia
Kitaaluma Eti Wanatisha

wanadai Afrika Mashariki
Elimu Yao Haipimiki
Kwa Ubora Haizidiki
Et,hawavutii Upande Wao?

Mtanzania Hapa Sina Moyo
Najiisi Poyoyo
Tena Kibogoyo
Wameniweka Dilemma.

2changie Wasomi,
Wanafalisafa,wanadini
Na Hata Wapenda Mapenzi.
jamani,ni Sisi Au Wao?

Mwamba Ngoma,yadaiwa
avutia Kwake Sana,
Tusiwe Wachekelea Donda
Tuseme Ukweli Adharani

Waganda wapewa Uhondo
Eti Kisa Wajua Kimombo! Je Twatongozwa Kwa Hilo
Na Tukubali Ka Mazuzu?

Wakenya Wasimetemete
Wala wasichekecheke
Kama Ndege Au K"kwete
Kwa Kupongezwa Uozo.

Kwa kifupi ni hivi shule zote za primary nchini uganda zinatumia kiingereza ktk kufundishia.kwa hiyo unakuta wanakuwa na msingi imara ktk lugha ya kiingereza.hilo la kwanza.la pili masomo yao yanawajenga ktk kufikiri zaidi kuliko kumeza.hata mitihani yao inapima uwelewa wa kufikiri zaidi.kwa mfano uganda mwanafunzi anaweza akaletewa maswali ambayo hajawahi kukutana nayo lakini akayajibu.kwa hiyo unakuta hamna tofauti kati ya shule za serikali na zile za binafsi labda mambo ya mazingira, chakula na malazi hapo ndo wanatofautiana.kwa shule za sekondari unakuta practicals wanawaanzishia toka kidato cha kwanza.literature pia wanaanza kusoma kidato cha kwanza.biology wanatumia "introduction to biology " tangu kidato cha kwanza.kwa hiyo unakuta wanasoma vitu vingi sana wakiwa bado wako madarasa ya chini.chemistry hatujatofautiana.ila wao wanasema tanzania kwa hesabu tupo juu.pia masomo yao yanatoa uwanja mkubwa wa kujielezea zaidi.
 
Back
Top Bottom