Elimu,ajra na biashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu,ajra na biashara

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Eliamini, Feb 18, 2012.

 1. Eliamini

  Eliamini JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 316
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 60
  Mtaala wa elimu ya tanzania unatuandaa vijana wengi tunaomaliza elimu ya juu namaanisha vyuo vikuu kuwa mategemezi na si kujitegemea na kukomboka na elimu tuliyopata. Wengi tunafikiria sana kuajiriwa na sikujiajiri pindi tumalizapo vyuo,mfano kijana unampa ushauri wa kufanya biashara anakuliza atapata wap mtaji wakat mkopo anaopewa na bodi anaumalizia katika starehe.vijana tuamke na tuwe na fikra za kibiashara kwan ukiwa mfanyakazi unakuwa mtumwa wa hela wakati mfanyabiashara hela ndo inamtumikia yeye,ni hayo tu ndugu zangu
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu hili swala la Vijana wa vyuo vikuu kujiajiri lina Historia ndefu sana na ni mchanganyiko wa factor nyingi sana ambazo ukijumlisha pamoja unakuja kupata hili tatizo la graduate kushindwa kujiajiri na kuishia kusubiria ajira za serikali au sekita bianfisi,

  1. MFUMO WA UCHUMI WA NCHI YETU, UJAMAA NA KUJITEGEMEA

  Huu mfumo ungali vichwani mwa watanzania wengi sana na kibaya zaidi umekuwa ukirithiswa kwa vijina ambao wamezaliwa baada ya UJAMAA KUWA UMEANGUKA MIAKA YA 90,
  Mkuu Ujamaa unalemaza sana na Nchi kama Urusi kilicho isaidia kumove fasta kutoka Uchumi wa kijamaa kwenda uchumi wa huru ni kwa sababu ilikuwa imeisha jiimarisha kwa viwanda na makampuni makubwa sana na Ukiangalia uchumi wa URUSI unashukiliwa na Warusi wenyewe walibinasifisha makampuni yao kwa wao wenyewe,

  Ingawa hata urusi Entrpremership culture si kubwa kama ilivyo INDIA na nchi zingine

  China kilicho wasaidia ni Kuwa na mifumo miwili kwa wakati mmoja Socialism na Market economy,

  Watanzania bado tuko katika huu mfumo wa kijamaa na ndo maana bado tunaamini Serikali ndo inatakiwa kuwatafutia masoko wafanya biashara, iwaanzishie biashara, iwaambie waanzishe biashara na kazalika, so watoto wanakuwa wanaaminishwa kwamba serikali ndo inatakiwa kufanya mambo mengi sana na wao ni kusoma na kuajiriwa tu.
  Nchi kama kenya wao kutokana na kuanza na mfumo wa ubepari tangia wapate uhuru wao wako juu sana kwa vijana wao kupenda kujijiri kuliko TZ

  2. UBINASIFISHAJI MBAYA WA MASHIRIKA YA UMA HASA VIWANDA ULIDESCOURAGE ENTREPRERSHIP CULTURE

  Vijana wengi hawana pa kujifunza ujasiriamali kwa sababu Viwanda vyote walipewa wahindi na hii indescourage sana entreprenership culture sema tu hatujajua, Tungefanya kama URUSI ingesaidia sana kuhamasisha vijana waingie katika Ujasirimali, kwa sasa tunajifunz kwa MENGI PEKEE NA WENGINE WACHACHE, na nivigumu kujifunza kwa makaburu na wahindi.

  3. MALEZI YA WAZAZI WETU

  Hili ndo tatizo namba moja linalo fanya Vijana wasijiingize kwenye Biashara/ujasirimali, waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi na ukiangalia kweli nchi kama India na kwingineko Vijana wanaanza ujasirimali wakiwa na umuri wa miaka 20 mpaka 38 na huu ndo muda wa mtu kuingia ktika ujasirimali,
  Tangia tukiwa watoto tunasisitizwa tusome sana tuje kuwa MAMENEJA, WAHASIBU WA MAKAMPUNI, TUFANYE KAZI BENKI, TUWE WAKURUGENZI, TUWE MARUBANI, na hii ni sumu mbaya sana ambayi kwa kweli inafanya watoto wakuwe wakiamni wao wanatikiwa kufanya kazi na si kujiajiri,

  4. SUCCESSFUL IS GENETIC
  Ili kijana aje kuwa mjasirimali mzuri inategemeana sana na ndugu zake, marafiki zake na majirani zake, kama hawa watu wote nilio wataja ni Wafanya kazi mtoto atasoma aili aje kuwa kama wao,

  Ingawa kuna wachache ambao wanakuwa wajasirimali wazuri pamoja na kwamba ndugu zao, marafiki, majirani na wafanya kazi, ila kwa kiasi kikubwa sana hili linachangia sana

  5. MIFUMO MI BOVU YA ELIMU YETU

  - Tunakaririshwa sana, tunasoma theory sana badala ya Vitndo, kuna vyuo vinatoa elimu ya ujasirimali, MZUMBE WANATOA DEGREE NA MASTER, UD WANATOA, UDOM WANATO, ila ukifuatilia wote walio maliza hapo wameajiriwa na kuna ambao wako mitaani wanatafuta kazi pamoja na kwamba wanaelimu ya Ujasirimali

  6. KUKOSEKANA KWA VIVUTIO
  ,
  Ni kweli hakuna vivutio vingi vya kuhamasisha Vijana wengi wajiajiri wamalizapo masomo na badala yake kuna vitu kama mamilioni ya JK yaliyo tolewa kisiasa bila kujali kama wanaohitajo wana nia ya kufanya biashara au la,

  Nchi nyingi hasa za ASIA zina vivutio kwa ajiri ya Graduate wao kama vile , ila huku naona vivutio vya kuwafanya watu wasome SCIENCE lakini hakuna mikakati ya kuwafanya graduate wajiajiri wamalizapo masomo,  SIJAWAHI SIKIA MZAZI AKIMSISTIZA MTOTO WAKE KWAMBA ASOME AJE KUWA MFANYA BIASHARA MKUBWA KAMA WAKINA MENGI.
   
 3. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Umezungumza suala lililo wazi mkuu.
  Naomba ufafanue mwanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania anawezaje kutumia pesa ya boom kufanya biashara..Inawezekana wewe mwenzetu umeweza kuitumia kama mtaji!
  Nadhani suala la muhimu ni namna ya kuwafanya vijana wajiajiri.
  Kusoma kozi za ujasiriamali ni hatua muhimu, lakini kuchukua hatua ni jambo muhimu zaidi.
  Napendekeza kitabu cha POOR DADY RICH DADY cha Robert...... kisomwe na wale wote wanaotarajia kujiajiri
   
 4. J

  JBAM Member

  #4
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani wakuu pamoja na matatizo meeeeeengi ya kisera, kimfumo, utanaduni, namengine mengi tunayoyajua bado ukweli unabaki pale pale kuwa tanzania imejaa resources kibao katika kila eneo la nchi hii ambazo vijana tukiamua kufanya mapinduzi makubwa kwenye fikra zetu na kuamua kuzitumia tutatoka tu. hii habari ya kusubiri serikali ifanye oo mara ujamaa mara elimu yetu wazee muda unakwenda na uzee unakuja na wanaoamua kufanya kazi kwa kutumia maarifa waliyoyapat vyuoni wanatajirika na sisi tunazidi kulia lia huku tukijifaraji na visingizio kibao.

  kijana wa jitanzania huna haja ya kutorokea ulaya ili ufanikiwe. na kama ukiweza kufanikiwa ukiwa ulaya basi kwa hapa bongo wewe utakuwa bilionaire kama hizo effort utakazotumia ulaya kufanikiwa utazitumia bongo.

  hata hao wazungu, wahindi, wachina na wengine wanakuja hapa bongo kwa kasi na wanaanza kijingajinga then baada ya mwaka unakuta ni tajiri. na anakuajiri graduate tena kwa mishahara nyau nyau.

  narudia tena tuache kulalamika tupambane maana uzee unakuja na uzee wa enzi zetu kama hutakuwa umejiwekezea utakuwa ni uzee mgumu balaa.

  umewahi mkuta muhindi baa kalewa chakali? tupunguze starehe (aka kujipongeza) tuzidishe juhudi katika kazi.
  shukrani wakubwa
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu hata watu wakisoma vitabu ni kazi bure, na kuna hadi degree zinatolwea za ujasirimali na kuna semina zinatolewa kila kukicha mkuu, kama nilivyo sema entreprenership culture kwa watanzania ni tatizo ambalo lina sababu nyingi sana,

  Na kama mtu hana ari ya kutaka kujiajiri hata ukipmatia nini ni kazi bure, hatuna entreprenrship spirit ndo maana utakuta mtu kajiajiri lakini mfuate siku moja mwambie kuna ajira mahali inalipa, atafunga biashara siku hiyo hiyo so utaona kwamba tu nakosa entreprenrship spirt mkuu na si kingine chochote,
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280

  Hapo kwenye red ndo tatizo lilipo na kufanya mapinduzi ya fikira kunahitaji kuwashirikisha watu wengi sana
  Inatakiwa kuwashirikisha
  1. Wazazi wetu
  2. Walimu
  3. Serikali
  4. sisi wenyewe

  Mapinduzi ya fikra yakishirikisha kundi moja tu itakuwa ni kazi bure, unaweza wah\shirikisha vijana tu wakati upande mwingine Wazazi wanawaimbia vijana wao wasome waje kuwa na kazi nzuri waje kuwa mameneja,
   
 7. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #7
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  To me, entrepreneurship means starting with nothing but a dream, pulling yourself up by the proverbial bootstraps, and making something good happen for yourself.

  One of the rule of Entrepreneurship spirit

  The first rule of entrepreneurship spirit you should realize is that your job is not a route to financial security.


  A job may help you pay the bills, but it is by nature, not designed to help you create wealth Here are just a few reasons why


  • An employee is not able to take advantage of tax breaks afforded the business owners

  • An employee must always answer to a boss who controls the purse strings.

  • An employee is subject to being laid off or fired at any moment.

  • An employee is unable to increase his or her income unless a boss agrees to it.
  When you accept that your job is not a route to financial security, and recognize that owning your own business is the best way to go, you are on your way to a secure financial future.
   
 8. J

  JBAM Member

  #8
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu nani wa juyaanzisha hayo mapinduzi kama sio cc vijana? mapinduzi ya fikra lazima yaanzie kwetu na hao wengine uliowataja watafuata baada ya kuanza kuona kwa vitendo. wala huna haja ya kuwachapa viboko.

  nimetembea nchi nzima ya tanzania kasoro lindi na mtwara, nakuhakikishia tuna resources nyingi kuliko unavyozifahamu.

  kumbuka kila penye matatizo/changamoto pana nafasi ya kufanya biashara/ujasiriamali na tanzania tuna lundo la matatizo katika kila sekta, lets b seriou and decide to see money & success guys
   
 9. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Mkuu komando nakubaliana na mawazo yako kwa asilimia zote.
  Wazo kuwa watu wasome vitabu linapata nguvu kwa kuwa si watu wote walio vyuoni wanaweza kusoma ujasiriamali maana wakati mwingine ratiba za masomo zinabana na wingi wa kozi kwa muhula.
  Nilipokuwa Chuo,ingawa nilitamani sana kusoma kozi ya option ya ujasiriamali, nilishindwa kufanya hivyo kwa kuzingatia sababu nilizotaja hapo juu.Hata hivyo sikukata tamaa,nikaamua kutafuta vitabu mbalimbali vinavyozungumzia masuala ya biashara na naendelea kufunguka kifikra .
  Kwa sasa naendelea kusoma kitabu cha Rich Dady Guide to Financial Freedom cha Robert Kiyosaki.
   
 10. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #10
  Feb 19, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu naomba mabadiliko yaanze pamoja na wewe,

  Mkuu ni kweli kabisa kuna resorces nyingi sana Tanzania ila cha kutia uchungu ni hiki,


  1. Watanzania wengi sana tunapenda biashara za uchhuzi, kuuza bidhaa kutoka china, India, Ulaya na kwingineko, cheki kariakoo, ailimia 99% ya wafanya biashara pale wanafanya biashara ya uchuuzi,

  2. Tanzania hatutaweza kusongo mbele kwa biashara za uchuuzi mkuu,

  3. Ni lazima Tufanye project ambazo zina feature nzuri sana ila tunapenda biashara za kutoa faida siku hiyo hiyo

  FURSA NYINGI NA NZURI TUMEWAACHIA WAGENI KAMA VILE

  1. MAKABURU

  2. WAHINDI

  3. WAKENYA
  4WAZUNGU WA ULAYA

  C C WATANZANIA TUMEJIKITA KWENYE BIASHARA KAMA VILE

  1. Saloon

  2. Kuuza chakula

  3. kumiliki Bodaboda

  4. Kumiliki Hiace

  5. Mabasi

  6. Gest

  7. Mabaaa

  MIRADI MIKUBWA KAM HIYO HAPO CHINI TUMEWAACHIA WAGENI

  1. Madini

  2. Utalii

  3. Kilimo

  4. Uvuvi
   
 11. m

  makeda JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Great thinkers hii ilikuwa debate nzuri na nzito. Nmejifunza vitu.
   
 12. Lyamber

  Lyamber JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,187
  Likes Received: 2,629
  Trophy Points: 280
  haya yote tisa kumi ni kwamba vijana inabidi tujiajiri kama mungu amesaidia bum inabidi tuache ama waache starehe kujipanga Mungu atatutoa tu sala nyingi, uchapakazi, siku moja business itakua succesful tu yan amini hivyo....
   
 13. Lyamber

  Lyamber JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,187
  Likes Received: 2,629
  Trophy Points: 280
  pure robert kiyosaki kaka hapo daah huyu jamaa namkubali kinoma noma yan ukisoma vitabu vyake lazima unapata michongo ya kupata pesa fresh tu mim naamin siku moja mambo yatakua fresh tu katika kujiajiri tu...
   
Loading...