nina swali hapa ambalo ninapenda kujadili na watu wanaoelewa nalo ni kwamba kila mtu anafahamu kwamba atom imejengwa na nucleas ambayo proton (+) na nutron (0), pamoja na elektron (-).
Na sote tunafahamu kwamba elektron inazunguka nucleas mithili ya sayari zinavyolizunguka jua.
Sasa swali langu ni kwamba ni kwa nini electron haiangukii kwenye nucleas kwa maana tunafahamu kwamba chaji chanya na hasi zinavutana na ukichukulia kwamba electron ni hasi na nucleas ina chanya kutokana na neutron? na kama hilo halitoshi Je ni kwa nini proton ndani ya nucleas hazipambani na na kusukumana pande mbili tofauti kwani zoote zina chaji ya aina moja (+)!!!!
Nadhani umeshapewa majibu kwa namna mbalimbali, inawezekana nikawa nafanya marudio. Mambo haya ya nature tumekuwa tunajenga majibu yake kwa kuweka hypothesis na kujaribu kuthibitisha kuwa hizo hypothesis zetu ni sahihi, na hivyo kuzifanya kuwa ndiyo majibu yenyewe yaani theory. Kwa bahati mbaya imetokea kuwa baadhi ya thories hizo zimekuwa baadaye zinaonekana kuwa siyo sahihi. Inawezekana huko mbeleni majibu yaliyopo sasa hivi kuhusu swali lako likaja kuonekana kuwa siyo sahihi.
Mpaka sasa hivi jibu la swali lako linatokana na hypothesis ijulikanayo kama symmetry; hypothesis hii imetanabahisha Gauge Laws ambazo ndizo zinazotambulisha Four Forces of Nature: Strong forces, Weak Forces, electromagnetic Forces, na Gravitational Forces. Electromagnetic na Gravtitaional Forces kwa pamoja zimo katika kundi lijulikanalo kama "inverse square laws." Sasa wewe swali lako limeangalia jinsi gani electromagnetic forces zinavyoweza ama kuvuta electrons kwende kwenye protons, au kusambaza protons zisikae mahala pamoja. Hata hivyo inaelekea kuwa umesahau kuwapo kwa hizi strong forces na weak forces.
Strong forces zinavuta protons mahala pamoja, na katika umbali mfupi hizi strong forces zina nguvu kuliko electromagnetic forces. Kwa hiyo hata kama electromagentic forces zinataka kusambaratisha hizo neutrons, bado strong forces zitazielemea hizo electromagnetic forces na kuziacha protons mahala pamoja.
Kuhusu swala la Neutrons kushindwa kuzama kwenye neucleus kwa sababu ya electromagnetic attraction itokanayo na negative charges hili linajibiwa kwa kutumia taswira ya sayari na jua. Sayari na jua zinavutana kwa kutumia gravatitational law ambayo ni inverse square law sawa na electromagnetic forces. Hata hivyo sayari hazianguki kwenye jua kwa sababu kila sayari ina nishati yake (kinetic Energy) inayotumia kuzungukia jua, na hii haibadiliki (Conservation of Energy). Kwa hiyo, ili kufanya sayari ianguke kwenye jua, inabidi kwanza iishiwe hiyo nishati. Vivyo hivyo kulingana na theories tulizonazo mpaka sasa kuhusu spartial relationship kati ya protons na electrons ni kwamba ili electrons zianguke kutoka kwenye njia zake kuelekea kwenye kwenye neuclear inabidi zipunguze energy levels zake. Kuangusha energy level ya electron ni njia mojawapo inayoweza kutumika ili kuvuna atomic energy, ingawa mpaka sasa hivi atomic energy imekuwa inavunwa kutokana na strong forces kwa kuvunja nuclear na ndiyo maana imekuwa inajulikana kama nuclear enegry.
Hata hivyo, nikumbushe kuwa theories hizi bado zina utata kadhaa na zinaweza kuja kuwa proved wrong huko mbeleni lakini hadi sansa ndizo theory tunazoamini kujibu swali lako.