witnessj
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 28,839
- 47,769
Affidavitnami nataka ku-re new yangu ila wazazi wangu hawana cheti cha kuzaliwa! Nifanyeje?
Affidavitnami nataka ku-re new yangu ila wazazi wangu hawana cheti cha kuzaliwa! Nifanyeje?
Kweli mkuu, kwa nchi yetu bado tuna mtazamo wa kizamani sana, huwa nacheka sana hata NMB wanapoona internet banking kama ni kitu kikubwa sana kwamba ili upate huduma hiyo ni lazima uwe na corporate account, yaani ni mitazamo ya ajabu na.isiyoendana.na wakati, taasisi husik badilikeni kimtazamo.Si kila anayeomba passport anasafiri na ana kazi .Passport huhitajika kwa ajili ya kufanya mitihani ya nje kama vile ya BRITISH COUNCIL ya IELTS (International English Language Testing System na kwa ajili ya kuomba scholarship,Nchi zote za Afrika mashariki ni Tanzania tu yenye haya masharti na imani kuwa mtu huomba passport kwa sababu anasafiri!!!!!!!!! VERY SAD.Mtu anataka afanye mitihani au aombe scholarship fomu ya kuomba passport inakomaa andika nchi unakoenda na ambatanisha uthibitisho wa safari!!!!!!!! ha ha ha
Jamani na kwa sisi tunao renew za zamani zineisha muda wake tunahitajika kuwa na vitu vyote ivyo? Nahitaji kwa ajili ya kusafiri binafsiHakikisha una
1. Kitambulisho cha taifa
2. Cheti cha kuzaliwa
3. Affirdavit ya mzazi mmoja
4. Barua ya mwaliko au uthibitisho wowote wa safari
5. Application form ambayo utakuwa umeapply online(utalipia 20,000)
6. Barua ya mtendaji wa kijiji/kata kama sio mwajiriwa.
7. Uthibitisho wa shughuli zako unazofanya i.e barua ya mwajiri kama ni mfanyakazi e.t.c
8. Kitambulisho cha kazi kama ni mwajiriwa
9. Barua ya ombi la passport
Wanaweza wakahitaji zaidi kulingana na madhumuni ya safari yako na pia shuguli zako e.t.c
Ingia kwenye hii link utapata kila kitu ikiwemo namna ya kujaza ombi lako online
Online ppt form
Sehemu inayosumbuaga sana ni hapo uhamiaji mkoa kwa maombi ambayo unaombea mkoani ila ukishakamilisha kila kitu na wakapitisha basi ombi lako likishaenda Dar ni chap tu passport yako itatumwa.
Hakikisha wanajua kuwa tarehe unayosafiri imekaribia as watakusaidia uweze kupata kwa haraka kabla ya safari
Ukienda siku ya kwanza kama wakikuambia kuna kitu bado hujakamilisha waambie wakague wakuambie kila ambacho kinamiss maana inawezekana vinamiss vitu vingi ila wakakuambia kimoja tu halafu siku ukirudi tena ndo wanakuambia hicho kingine unajikuta unaenda na kurudi mara nyingi.
Kila kitu utakachotoa kopi i.e cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha taifa e.t.c hakikisha kinathibitishwa(kupigwa muhuri) na mwanasheria/hakimu, sijui kama hili ni lazima lakini mimi waliniambia nikapige muhuri.
Kwa ushauri wangu usiwe mtu wa story nyingi za kuelezea kwa nini huna unapoulizwa document ambayo huna, we nenda kaitafute(utaipataje utajua mwenyewe) usipende sana kuvunja sheria au kutofuata inachosema we ikunje halafu pita, mara nyingi wanachotaka ni kuiona suala la kuwa genuine au sio hawataangalia sana isipokuwa kwa zile document za kitaifa zinazojulikana na kila mtu kama birth certificate na kitambulisho cha taifa. Kumbuka na yeye anapoipeleka kwa mkuu wake inabidi akaanze kuelezea story za kwa nini document fulani haipo na hapo unakuwa unawapa kazi ya ziada kwa hiyo hawapendi sana hizo story.
Kila la heri.
kachukulia dar yupo darPaspoti kachukulia hapa Mwanza?
Hizi passport za siku hizi za electronic kuna vishoka?
Kwa sasa hivi anayerenew ni sawa tu na anayeomba kwa mara ya kwanzaJamani na kwa sisi tunao renew za zamani zineisha muda wake tunahitajika kuwa na vitu vyote ivyo? Nahitaji kwa ajili ya kusafiri binafsi
Je ukiwa na cheti cha kuzaliwa cha mzazi mmoja inafaa au ni vya wote wawili?Hapo documents nyingine zote zinazonihusu mm ninazo hata wakitaka kadi ya clinic ninayo.Una cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha taifa, cheti cha kuzaliwa au affidavit ya mzazi wako? Kama ndio utaipata kabla ya muda huo.
Cheti cha mzazi mmoja kinatosha, lakini kama una ngozi nyeupe mfano mhindi, mwarabu lazima vya wazazi wote na babu na bibi.Je ukiwa na cheti cha kuzaliwa cha mzazi mmoja inafaa au ni vya wote wawili?Hapo documents nyingine zote zinazonihusu mm ninazo hata wakitaka kadi ya clinic ninayo.
Cheti cha mzazi mmoja kinatosha, lakini kama una ngozi nyeupe mfano mhindi, mwarabu lazima vya wazazi wote na babu na bibi.
Kwa taarifa nilizozipata hii idara kule Rwanda imewahi kutunukiwa tuzo za huduma bora kwa taasisi ya serikali kimataifa kwa mfululizo wa zaidi ya miaka mitatu. Kuna jambo la kujifunza hapo.Rwanda inachukua siku nne kupata passport mpya ku renew inachukua siku mbili sisi......
Four (4) working days for first application and two (2) working days for renewal
Ni ndani ya siku 7. Mtoto wangu alipata siku ya 4 tu baada ya kuwasilisha maombi na kulipia. Kama viambatanisho vyote viko sawa. Tuliombea hapa Dar es salaam. Hakuna rushwa wala usumbufu wowote. Sijajua kwa nje ya Dar es salaam.Kama una viambatanisho vyote ni Siku 21 za kazi, hakikisha hakuna kasoro, majina yawe sawa, kama kuna kasoro kwenye majina basi nenda kwa mwanasheria yupo hapo jengo LA Nyumba atakusaidia ( affidavit)
Nili submit kila kitu trh 2 passport nikapata trh 27.mwezi huo huo. Hakuna mbwembwe Siku hizi, andaa 150000 weka mpesa yako utalipia online.
Yeah nina kilakitu
Wapate affidavit (uthibitisho) wa ndugu/rafiki zao wanaowazidi au kupishana kiasi kiumri. Fomu hizo utazipata mahakamani au ofisi za wanasheria, hao ndugu watajaza taarifa zao na wanasheria kuweka mhurii wao.nami nataka ku-re new yangu ila wazazi wangu hawana cheti cha kuzaliwa! Nifanyeje?
Kumbe uko dar uliza wa mikoani wanapata baada ya muda gani?Ni ndani ya siku 7. Mtoto wangu alipata siku ya 4 tu baada ya kuwasilisha maombi na kulipia. Kama viambatanisho vyote viko sawa. Tuliombea hapa Dar es salaam. Hakuna rushwa wala usumbufu wowote. Sijajua kwa nje ya Dar es salaam.