Umeme ambao ungekuwa ndio mbadala hapa kwetu ni ghali kama kitu cha luxury vile. Wiki iliyopita kuna kampuni moja ya solar ilifanya maadhimisho yake ya miaka 10 pale makumbusho, nilienda nikifikiri kuna nafuu yoyote lakini nilikata tamaa ni ghali kuliko umeme wa tanesco.
Windmills nahisi kama inahitaji mtaji mkubwa, hasa kwa ajili ya haya mapanga boi, sijui.
Kwangu mimi teknolojia rahisi ambayo nafikiri inaweza kuwasaidia watumiaji wadogo wadogo vijijini na hata mjini ni kutumia inverter, hii niliiona hata south. Wale wanaopigisha simu mtaani kwenye vioski vyao wanatumia inverter na kwa kweli wanajikomboa katika kujikimu. DIT, UDSM n.k wakijikita katika kutengeneza inverter wanaweza kusaidia watu wa hali ya chini wengi, sababu unahitaji betri ya gari na inverter ili kuzalisha umeme. Ukubwa wa inverter utategemea na mahitaji ya mtumiaji, kiasi unaweza kukuta hawa jamaa wenye saluni za kunyolea wasingekuwa walalamikia umeme wa tanesco tena na wangeweza kupunguza gharama za uzalishaji.