Election Expenses Bill 2009

nafikiri walikuwa wanafikiria kutunga sheria ya kuondoa rushwa kitu ambacho kwa masikitiko makubwa naweza kutangaza kuwa wameshindwa. Sheria hii inafungua mlango mpya kabisa wa matumizi ya rushwa katika chaguzi.

Ni
Kweli kama kweli serikali ina dhamira na nia ya dhati ya kuweka mazingira ya haki ya uchaguzi nadhani inabidi waangalie kwa upana mfumo mzima wa uchaguzi.

- Sifa ya mgombea -Kuna issue ya mbombea binafsi
- Sheria ya matumiz haiwezi kuwa fair kama CCM inamiliki mali na vitega uchumi ambavyo wananchi wa vyama vtote na watanzania walichangia.Kuweka mazingira sawa ya mapambano hii sheria ingependekeza mali za CCM zilizopatiakana wakati wa chama kimoja zirudishwe serikalini. Na kama so hivyo labda Hii sheria iwe kwa CCM alafu waweke kifungu kingine chenye kukidhi vyama viliyokuja baada ya mfumo wa vyama vingi.
 
Rais Kikwete akihutubia wananchi kuhusu sheria ya mpya Gharama za Uchaguzi alielezea mambo kadhaa baadhi yake ni haya: Je the "law of unintended consequences" itajionesha vipi?

Ndugu Wananchi,
Sheria pia inaweka sharti la uwajibikaji wa vyama vya siasa, wagombea na washiriki wengine kuhusu michango, mapato na matumizi katika uchaguzi. Sheria inaelekeza kwamba:-
1. Kila mchango unaopokelewa na matumizi yatakayofanyika kwa ajili ya uchaguzi vifanywe na Chama na siyo vinginevyo.

2. Chama cha siasa kitawajibika kwa matumizi yote yatakayofanywa na chama au wagombea wake, na kwamba matumizi yote yanatakiwa kuwa na risiti.

3. Kila mgombea atawekewa mgawo wake wa matumizi ya kampeni na chama kitatoa taarifa ya fedha iliyokaguliwa kwa matumizi hayo.

4. Chama kitakachoshindwa kutunza taarifa hizo kitakuwa kimetenda kosa na kitastahili adhabu.

5. Kila mgombea atakayepokea mchango atapaswa kutoa taarifa kwa chama chake kuhusu mapato na matumizi yanayohusu mchango huo.

6. Kila chama cha siasa, taasisi ya kiraia, taasisi ya kidini au taasisi ya kijamii itakayohusika katika kuchangia shughuli za uchaguzi, inayo wajibu wa kutunza taarifa za fedha zinazoelezea mapato na matumizi yao....

Na pia,
Ndugu Wananchi;
Sheria imeainisha vizuri mambo yanavyokatazwa kwa upande wa matumizi ya fedha za uchaguzi. Sheria inakataza, kwa mfano, vitendo vifuatavyo visifanyike pamoja na matumizi ya fedha kwa ajili hiyo kuzuiliwa:
1. Kufanya malipo kwa wapiga kura ili wamchague mgombea fulani;

2. Kuahidi kazi au cheo au wadhifa kwa mpiga kura ili amchague mgombea;

3. Kutoa zawadi, ahadi, mkopo, au makubaliano yoyote kwa mpiga kura ili amchague mgombea;

4. Kukubali kurubuniwa kwa mambo yoyote yaliyotajwa hapo juu ili ampigie kura mgombea yeyote;

5. Kufanya vitendo vyovyote kati ya hivyo wakati wowote kabla au hata baada ya uteuzi wa mgombea;

6. Kutoa malipo kwa ajili ya takrima ya chakula, vinywaji au starehe yoyote kwa ajili ya kuwashawishi wapiga kura wamchague mgombea;

7. Kuwasafirisha wapiga kura ili wamchague mgombea. Hata hivyo Sheria inaruhusu wapiga kura wenyewe kujilipia nauli kwenda kupiga kura au Serikali kuwasafirisha wapiga kura pale ambapo kuna shida ya usafiri;

8. Kuweka mkataba wowote ule wa pango kwa niaba ya wapiga kura ili wamchague mgombea;

So.. unakubaliana naye?
 
Mku Mwanakijiji,

Kama kweli hataki watu watoe ahadi basi hata Ilani ya uchaguzi ya CCM isiwepo...

naona anajichanga na maneno.
 
Mku Mwanakijiji,

Kama kweli hataki watu watoe ahadi basi hata Ilani ya uchaguzi ya CCM isiwepo...

naona anajichanga na maneno.

siyo yeye.. ndiyo sheria yao inavyosema. Yaani kuanzia sasa wagombea hawaruhusiwi kutoa ahadi yoyote kwa wapiga kura ili wachaguliwe!
 
Unfortunately swali halijatulia, sheria imetungwa na bunge, Rais anafafanua.... sasa why do i have to agree or disagree with him?

Are we serious or we just trying to push our agenda for all means possible?
 
unajua mimi namuoneaga huruma sana huyu mzee sijuini nani anamshauri mambo haya..lakini ndo shida ya kuwa na rais wa nci mwenye upeo finyu wa kupambanua mambo
 
Unfortunately swali halijatulia, sheria imetungwa na bunge, Rais anafafanua.... sasa why do i have to agree or disagree with him?

Are we serious or we just trying to push our agenda for all means possible?

Ndio maana nimeuliza kuhusu Rais sikuuliza kuhusu sheria kwa sababu najua sheria inasema nini. Tatizo ni yeye alichokisema alikuwa anajua anamaanisha nini? Au alikuwa anarudia kama kasuku?
 
Nashangaa kidogo;

Niliambiwa kuwa sheria ya madini imefadhiliwa na kama sikosei EU,hivi hii imefadhiliwa na nani?

Mwenyewe sio mwadilifu maana kuna mengi aliaahidi ijapokuwa hayakuwa kwa ilani yao. UDOM kwa kuanza tu.

Kumbe hata yeye hana ushirikiano wa brain na moyo?
 
Kutoa zawadi, ahadi, mkopo, au makubaliano yoyote kwa mpiga kura ili amchague

Wapendwa,

Tunahitaji kuwa makini zaidi tukisoma mabadiko au sheria... haiwezekani unataka ubunge unaenda kumuahidi mtu mmoja... sheria imesema mpiga kura... "singular" kiswahili "mamoja".

Usually ahadi za mbunge ni kwa huduma zinazokumba jamii nzima sio mpiga kura mmoja. hivyo ingesema ahadi kwa wapiga kura that is different.
 
Mzee Mwanakijiji,

1.Sijaisoma sheria hiyo ila naona kuna haja ya kuipitia,itakuwa imeandikwa kimakosa sana coz si rahisi wananchi kumchagua mgombea wa chama flani bila ya kujua atafanya nini akichaguliwa kuwa Mwakilishi(mbunge).

2.Duniani kote sifa za mtu hazitoshi kuwa kiongozi mpaka aoneshe mpango mkakati wake katika kuwasaidia wananchi na kuleta maendeleo chanya.Tunafahamu wananchi wamekuwa wakipata matatizo mengi na lengo la kuchagua ni kupata viongozi bora ambao watatelekeleza shughuli za maendeleo.

3.Kama hawataki wananchi wapewe ahadi basi hakuna haja ya kuwa na uchaguzi,tunachagua nini sasa?sura?au chama? na hii inaonesha au imeamuliwa na Chama kuwa mambo mengi ambayo wamekuwa wakiyahidi hayatekelezeki hivyo wameamua kuwaamisha wananchi kuwa wanweza kutawala kwa kuwa wana uzoefu.

4.Kwanza kwanini hii sheria haikushilikisha wadau wake?au kama walishirikishwa(viongozi wa vyama vingine) walikubaliana vipi na mambo haya?hili si suala la mambo ya serikali bali ya kisiasa zaidi na ingekuwa vyema wadau wangeshiriki kikamilifu(hapa wakiwamo wananchi wenyewe).

Gembe

 
Wapendwa,

Tunahitaji kuwa makini zaidi tukisoma mabadiko au sheria... haiwezekani unataka ubunge unaenda kumuahidi mtu mmoja... sheria imesema mpiga kura... "singular" kiswahili "mamoja".

Usually ahadi za mbunge ni kwa huduma zinazokumba jamii nzima sio mpiga kura mmoja. hivyo ingesema ahadi kwa wapiga kura that is different.

wrong. kwani kuna mtu anapiga kura zaidi ya moja. Wagombea hawaombi kura nyingi, wanaomba kura moja moja tu! ndio maana ya kusema "mpiga kura"..
 
si uweke ile nyingine?mm kidole kikitoka mdomoni ntakiweka wapi bana?


koh koh koh.. haya tuyaache. Naitafuta picha ya jembe sijui wajukuu wameiweka wapi. Mama nanino amenilalamikia hataki anione na picha ya shambani tena..
 
Rais hajakosea wala sheria haina matatizo, matatizo mumesoma hayo maneno mkiwa na agenda zenu...

Someni tena vizuri mkiwa na open minded.

2. Kuahidi kazi au cheo au wadhifa kwa mpiga kura ili amchague mgombea;

3. Kutoa zawadi, ahadi, mkopo, au makubaliano yoyote kwa mpiga kura ili amchague mgombea;

Hapa rais anazungumzia mbunge mtarajiwa kumuahid kasheshe cheo, etc. kosa wapi wandugu... mbona mnaturudisha nyumba?
 
koh koh koh.. haya tuyaache. Naitafuta picha ya jembe sijui wajukuu wameiweka wapi. Mama nanino amenilalamikia hataki anione na picha ya shambani tena..

nimeipenda t-shirt yako......inaelekea ulivyokuwa kijana ulikuwa model...jinsi ulivyoivaa I mean
 
wrong. kwani kuna mtu anapiga kura zaidi ya moja. Wagombea hawaombi kura nyingi, wanaomba kura moja moja tu! ndio maana ya kusema "mpiga kura"..

Mzee Mwanakijiji is this the so called great thinking... then tumechosha na spinning zako... Ili uelewe jambo lazima uangalie contest gani mtu huyo anaongelea.. ndio maana ukisoma vitabu vitakatifu ukitoka na mstari mmoja bila kusoma mistari ya kutosha unaweza toka na maana ambayo haijakusudia.

Would you please stop your bad intent of trying to justify everything president talk is wrong please.... wewe mkubwa sasa mkuu.
 
Kwa sheria hiyo maana yake mgombea haruhusiwi kutuahidi ajira milioni moja kama alivyofanya Kikwete mwaka 2005,maana wapo waliomchagua wakiamini kwamba kumchagua kikwete kutawafanya wapate kazi.

Halafu msisahau kwamba ameshaahidi kuwapa vijana vyeo katika serikali yake ijayo,sasa sijui hiyo sheria itatekelezwaje kama hata anayetakiwa kuisimamia anaivunja mapema.
 
Rais hajakosea wala sheria haina matatizo, matatizo mumesoma hayo maneno mkiwa na agenda zenu...

Someni tena vizuri mkiwa na open minded.



Hapa rais anazungumzia mbunge mtarajiwa kumuahid kasheshe cheo, etc. kosa wapi wandugu... mbona mnaturudisha nyumba?

Kasheshe.. yawezekana uko sahihi.. lakini let see kama ina mantiki.

Mgombea wa Urais anaweza kuahidi watu wangapi vyeo wampigie kura na wakasababisha matokeo ya yeye kuchaguliwa. Lakini la pili ni kuwa, siasa ni ushawishi na kuwafanya watu wakubaliane na wewe.

Sehemu mojawapo ya kupata support ni uwezo wa kushawishi baadhi ya watu wawe upande wako na sehemu yake ni kuwa wao watapata nini. Kama kinachobadilishwa ni kura na siyo fedha kwanini hilo liwe kosa?

Balozi wa US Tanzania sasa hivi amepata nafasi hiyo kutokana na mchango wake kwa kampeni ya Obama, na hilo linaenda kwa nafasi nyingine mbalimbali na hasa wakati wa primaries..

Mgombea atapata vipi watu wa kufanya naye kazi kama hawako loyal kwake? Kuondoa hilo analosema rais si ndiyo kuua siasa kwenye na demokrasia?
 
Back
Top Bottom