Leo ni siku ya Saba (Jumatatu) ya maandamano ya kumtoa Mubarak katika madaraka,kuna utulivu wa uvunjwaji wa sheria kama uizi (looting),na utupaji mawe hovyo mitaani,pia kumekuwa na milio michache ya risasi si kama ilivyokuwa siku za nyuma.Maandamano makubwa yanaelekea tena Tahir Square kutoka katika kila pande za mji wa Cairo.Ndege za Jeshi zimekuwa zinaruka chini chini karibu maeneo yote ya mjini haswa Tahir Square ambako baadhi ya waandamaji wamelala hapo.Habari kutoka Al-Jazeera zinasema Rais Hosni Mubarak bado yupo Cairo na Jana Jumapili akifuatana na VP mteule Omar Suleiman alitembelea kambi za Jeshi zilizopo karibu na Mji wa Cairo.Mke wa Rais Suzzane Mubarak pamoja na Mtoto mkubwa wa Rais Gamal Mubarak wamekimbilia London.Kuna taarifa kuwa Rais anaandaa utaratibu wa kukimbilia uhamishoni Riyadh (Saudi Arabia) au Tel Aviv (Israel)...Jumapili mchana jumla ya ndege binafsi 17 zimeondoka Cairo kuelekea UAE na inasemekana zilikuwa zimechukua familia za matajiri kutoka Cairo.Miongoni mwa walioondoka ktk msafara huo yupo Mohammed Al Amoudi ambaye yupo katika forbes billionnaire wa 2010.
Serikali ya Marekani imefunga Ubalozi wake mjini Cairo na Balozi wa Marekani Nchini Misri Mama Margaret Scobey amewataarifu raia wote wa Marekani wanaotaka kuondoka Misri wawasiliane na Ubalozi huo na kuanzia Leo (Jumatatu) mchana kuna ndege zitakazowasafirisha watu kuelekea Washington na New York,inasemekana kuna Jumla ya Waamerika 50,000 Nchini Misri.Waziri wa Ulinzi wa US,Robert Gates amekuwa kwenye simu na Mkuu wa Majeshi wa Misri na Israel kwa karibu masaa manne siku ya Jumapili,kwa vyovyote itakavyokuwa,ni wazi kwamba Rais Mubarak ataachia madaraka na kutaundwa serikali ya mpito kuelekea Uchaguzi.Maamuzi yoyote yatakayombakisha Rais Mubarak madarakani yatazidi kuleta maafa.Jumla ya watu 120 wamekufa katika miji ya Cairo,Alexandria na Suez.
Wamisri wanaoishi katika Nchi za Marekani,Canada,Uingereza na Ujerumani wamekuwa wanazishikiza Nchi hizo wamuombe Rais Mubarak aachie uongozi ili apishe uchaguzi huru na wa haki.
Kumekuwa na maandamano katika nchi za Jordan,Yemen na wanafunzi wa Nchini Sudan wameandamana kuunga mkono maandamano ya Misri.Vuguvugu hili la maandamano lilianzia Tunisia ambako mhitimu wa chuo kikuu alijichoma moto baada ya kubugudhiwa na askari wa mji alipokuwa anauza mboga mboga bila kuwa na kibali.Wimbi hilo limepita pia Algeria ambako bei ya mkate imepanda sana.Nchini Libya kumetolewa onyo kali kuhusu namna yoyote ya mkusanyiko wa watu,matumizi ya simu,na intaneti yamekuwa yakisikitishwa kila wakati katika Nchi hiyo iliyopo karibu na Misri na Tunisia.