Ehhh hata leo sina kazi

Ehhh hata leo sina kazi

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,301
Reaction score
9,847
Ehhh, hata leo sina kazi, sina hata nafasi,
Nimezunguka mjini, natafuta mafanikio na nafasi,
CV zangu zimejaa, lakini majibu hayaji,
Kila nikifungua simu, ni madeni yanayokuja wazi.


Ehhh, hata leo sina kazi, maisha yamenibana,
Mwenye nyumba anadai, sina pa kujificha tena,
Mama anataka hela, namwambia subiri kidogo,
Nimebaki na matumaini, hata kama mfuko mtupu.


Ehhh, hata leo sina kazi, lakini bado napambana,
Wenzangu wanapanda juu, mimi bado najikongoja,
Wanasema uwe na connection, ndipo upate nafasi,
Bila mjomba mwenye cheo, unazunguka kutafuta kazi.


Ehhh, hata leo sina kazi, ila sitapoteza dira,
Nimepitia mengi sana, maisha yamenipa hasira,
Siku yangu ikifika, nitawalipa kwa mafanikio,
Leo wananiona chini, kesho watasikia simulizi yangu!
 
Wachana na michano ya hip-hop. Weka nyimbo za maombolezo maana tunategemea msiba soon
 
Back
Top Bottom