Eh! kumbe madaktari mshahara kiduchu hivi!

dopeboy

Senior Member
Sep 22, 2014
121
100
Kati ya siku iliyonisikitisha ni Leo. Kina rafiki yangu, namuadmire sana, toka tukiwa wadogo alikuwa so bright, mpaka akafanikiwa kuwa daktari.

Mimi binafsi huwa napenda sana kila weekend au nipatapo muda kuwa nae sehemu tunapiga story, naye hupenda kuniambia vitu vya kazini kwake kama wagonjwa na matukio anayokutana nayo. Ila ni kama weekend moja tu kwa mwezi ninaweza kumpata nyingine yeye huwa busy sana.

Sasa Mimi nimesoma mambo ya finance na nilifanikiwa kupata exposure nje kwa muda tu. Sasa kwa assumption zangu jinsi huyu rafiki yangu anavyokuwa busy na kutoa muda wake ata kukesha na kuwa mbali na familia nikajua na angalau salary yake itakuwa safi. Ila chakushangaza Leo alipata salary slip yake na kunionesha , oh my imenisikitisha kiukweli, ni around 1.48m take home yake ni kama laki 4 baada ya kukatwa na bodi na bank. Yani ninamzunguka karibu Mara 5 na sijawahi kukesha hats Mara Mona kazini. Yani kwa kifupi effort zake na zangu hazilingani. Sisemi kwamba kazi yangu haina challenges isipokuwa sifikii za kwake.

Nimejifunza kitu Leo. Maisha ni ushuzi mtupu, nimeamua nitampatia million 10 amalize shida zake ndogondogo rafiki yangu sana. This is not fair.
 
Ufisadi ndio unaowafanya vijana wengi wa PCM, PCB na hata ENGINEER wakimbilie finance, accountant, business administration nk kwani huko Kuna mwanya mkubwa wa kupiga ela za kifisadi ndio ukweli wenyewe. Mimi nina washkaji watatu mmoja engineer, mhasibu na mwingine kapiga maswala ya taxation. Jamaa wa engineer anakula 2.1m, mhasibu 1.2 m na huyu wa tax 900000 cha ajabu jamaa wa tax ndani ya miaka mitatu ana nyumba na gari, huyu mhasibu ndani ya miaka mitatu ana gari na anapaua ,jamaa yangu wa engineer ndani ya miaka mitatu ndio nae aapaua (na jamaa si mtu wa starehe kama wenzake hao wawili). Mwisho namalizia udaktari ni fani iliyotukuka, yoyote mwenye kuisoma lazima awe na huruma, upendo na mcha mungu, asiendekeze sana ela, akisema aendekeze ela kama ww ulio leta uzi huu, roho nyingi zisizokuwa na hatia zitaangamia na nyie ndugu zangu wa finance nyinyi hamna mishahara mikubwa ila wizi na ufisadi ndio unao wafanya muwe na ela.
 
1.48 mbona mshahara mkubwa sana tu huo. Sema labda makato yamekuwa makubwa lakini kiasi cha mshahara sio kidogo. Jamani issue nyingine ya msingi nikwamba kwenye ajira hakunaga utajiri kama unatak kutajirika jiajiri
Watu wanataka kutumia akili za wasaka hela kupatia hela!! [HASHTAG]#ThinkAndGrowRich[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom