Egypt will honour ‘veil martyr’ with street name | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Egypt will honour ‘veil martyr’ with street name

Discussion in 'International Forum' started by Junius, Jul 16, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  The hometown of a pregnant Egyptian woman stabbed to death in a German courtroom is to honour the ‘veil martyr’ with a street in her name, Egypt’s official Mena news agency reported yesterday. Alexandria governor Adel Labib “agreed to give the name of martyr Marwa al-Sherbini” to a street in the northern Egyptian Mediterranean city, Mena quoted Labib as saying during a commemoration ceremony. Sherbini, 31, died in a courtroom in the east German city of Dresden after being stabbed at least 18 times in front of her three-year-old son and her husband, allegedly by a Russian-born German man.
  source: GULF TIMES
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Why stabbing her?!!!!

  What was she doing in the courtroom anyway?
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Jul 25, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Maelfu ya Waislamu walikutana nchini Ujerumani kumkumbuka na kumsomea dua Marwa al Sherbini, mwanamke Muislamu wa Kimisri aliyeuwa kwa kudungwa kisu na raia Mjerumani katika mahakama ya mji wa Dresden tarehe Mosi Julai mwaka huu.
  Marwa alikwenda mahakamani kuwasilisha mashtaka dhidi ya jirani yake mbaguzi alipigwa kisu mara 18 na kuuawa shahidi mbele ya baraza la mahakama, mume na mwaname mwenye umri wa miaka 3.

  Marwa al Sherbini ametambulia na Waislamu katika nchi nyingi za Kiislamu kuwa ni Shahidi wa Hijabu kutokana ma kuuawa kwa sababu ya vazi lake la hijabu ya Kiislamu.

  Serikali ya Ujerumani inalaumiwa mno kwa kutoonyesha msimamo madhubuti wa kulaani mauaji hayo.

  MwenyeziMungu amtunukie Janatul Firdaus Insha'Allah.


  NB:'Dunia ingekumbwa na vilio na makelele mengi lau kama angeuawa Myahudi au Mkristo badala ya Bibi Marwa al Sherbini.'

  Hakika tungesikia mengi sana!
   
  Last edited by a moderator: Jul 25, 2009
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hiyo ingekuwa kinyume kuwa aliyeuawa ni wa Dini nyingine zaidi ya Uislam, na muuaji ni Muislam. Tena mbele ya Mahakama, vyombo vyote vya habari vingegeukia hilo na hata Serikali ya Ujerumani ingetoa tamko kali mno, lakini kwa kuwa ni wale kwao halali kuuliwa Dunia imekaa kimya.

  Mfano tu Waislam wa China walio wechache wa kabila la Uyghur walipopambana na kuuliwa na Wachina walio wengi wa kabila la Han. Tena mpaka Polisi walishirikiana na hawa wa Han kuuwa Waislam, lakini Dunia kimya kama hakijatokea kitu. Ila chukulia waTibet nao ni wachache wakishughulikiwa wanavyotetewa na Dunia nzima sababu si Waislam.
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Jul 25, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Siku ya Kimataifa ya Vazi la Hijabu

  Mwili wa Marwa al Sherbini, mwanamke wa Kimisri aliyedungwa kisu mpaka akafa shahidi katika mahakama ya Ujerumaji umezikwa katika mji wa Alexandria nchini kwao. Shughuli ya mazishi ya mwanamke huyo ambaye sasa amekuwa mashuhuri kwa jina la "Shahidi wa Vazi la Hijabu", imehudhuriwa na maelfu ya watu wakiwemo mawaziri wa serikali na wabunge.

  Hadhirina waliokuwa na hasira katika mazishi hayo walipiga nara wakilaani siasa na msimamo usiokuwa wa kimantiki wa serikali ya Cairo kuhusu mauaji hayo ya kinyama. Vilevile Waislamu wa Misri wamechukizwa mno na kutohudhuria balozi wa Ujerumani mjini Cairo katika mazishi hayo na kimya cha vyombo vya habari vya nchi za Magharibi kuhusu mauaji hayo ya kigaidi.

  Watumiaji wa mtandao wa Islamonline wametoa pendekezo kwamba siku ya kuuawa shahidi Marwa al Sherbini ipewe jina la Siku ya Kimataifa ya Vazi la Hijab

  Jinai hiyo ya kutisha ilitokea baada ya Mjerumani mwenye umri wa miaka 28 kwa jina la Alex W. kumshambulia kwa maneno Marwa al Sherbini na kumvunjia heshima kwa matusi kutokana na vazi lake la Kiislamu la hijabu. Mjerumani huyo alimrukia mwanamke huyo na kumvua hijabu huku akimwita kuwa ni gaidi. Bibi al Sherbini aliwasilisha mashtaka mahakamani ambako Mjerumani mchokozi alihukumiwa kulipa faini ya Euro 750. Mhalifu huyo alikata rufaa mahakamani na hapohapo akamshambulia mwanamke huyo aliyekuwa na mimba ya miezi mitatu na kumuua shahidi kwa kumdunga kisu mara 18. Mjerumani huyo pia alimjeruhi mume wa mwanamke huyo. Maafa hayo hayakuishia hapo, bali polisi wa Ujerumani pia alimpiga risasi mbili mguuni mume wa Marwa kwa madai kwamba alidhani ndiye aliyemshambulia raia wa Ujerumani.

  Maelfu ya Waislamu wameandamana mbele ya ubalozi wa Ujerumani mjini Cairo wakilaani mauaji hayo na kutaka kuchukuliwe hatua kali dhidi ya mhalifu huyo. Waandamanaji hao wamesisitiza kuwa ugaidi ni mwana aliyezaliwa huko Magharibi na kwamba mauaji ya kikatili ya Marwa, mwanamke Muislamu ambaye kosa lake pekee ni kuvaa vazi la hijabu, ni maafa ya kibinadamu. Tariq al Sherbini, kaka yake marehemu Marwa amesema kuwa mauaji ya mwanamke huyo yameonyesha kwamba ugaidi halisi uko katika nchi za Magharibi. Mwendesha Mashtaka wa mji wa Dresden nchini Ujerumani Christian Avenarius ameyataka mashambulizi hayo kuwa yanatokana na hisia za kibaguzi.

  Mhariri Mkuu wa gazeti huru la al Shuruq ameandika kuwa:
  'Dunia ingekubwa na vilio na makelele mengi lau kama angeuawa Myahudi badala ya Bibi Marwa al Sherbini.'

  Mauaji ya mwanamke huyo Muislamu nchini Ujerumani tena mbele ya polisi na ndani ya jengo la mahakama yamezidisha wasiwasi kwamba hisia za kupiga vita dini ya Kiislamu na ufashisti vimeanza kukita mizizi barani Ulaya.
   
 6. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hakika Allah (SW) alishasema, hawataacha wasioamini kuwatia katika misukosuko mpaka mfuate mila zao. Mungu amlaze mahala Pema Peponi Marwa al Sherbini, na vilevile ampe afuwa ya haraka mme wake.
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Jul 25, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Uzuri wa Uislam unajisimamia, na kila hatua wanayo piga ili kuumaliza ndio kama wanamwagilia maji na mbole, kila kukicha mti wa rehma unazidi kushamili na kunawili.
   
 8. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #8
  Jul 25, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135

  X-PASTER,

  kinachonishangaza na hii ishu ni kua Marwa al Sherbini alidungwa kisu mara kumi na nane inside a court room. Yaani hakuna mwera wa kuzuia kitendo hiki ama mwera wenyewe ni wabaguzi kama jamaa aliyekua anashtakiwa?

  Rabana ailaze roho yake mahali pema peponi.
  Amin.
   
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Jul 25, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mbaya zaidi polisi wa Ujerumani pia alimpiga risasi mbili mguuni mume wa Marwa kwa madai kwamba alidhani ndiye aliyemshambulia raia wa Ujerumani.

  Inasikitisha sana.
   
 10. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #10
  Jul 25, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Duh!...that makes it even more painful to imagine what this woman had to
  go through.
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Jul 25, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ja ajabu zaidi, vyombo vya habari vya kimagharibi vinavyojifanya vinatetea sana haki za binadamu hasa wanawake viko kimya...! Hakuna cha NGO's wala nini wote wanafiki watupu.
   
  Last edited by a moderator: Jul 25, 2009
 12. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #12
  Jul 25, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ...hapa ushamaliza mchezo bro!
   
 13. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa huu ni zaidi ya ugaidi kumbe ni wazi kabisa jinsi Islam and society being traslated.

  Tunaomba humu janvini wenye kujua watupe ufafanuzi juu ya Islam and modern society na Islam and changing society. P{lz ufafanuzi
   
 14. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #14
  Jul 25, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Mkuu Malyamungu,

  tukileta mijadala kama hio humu ndani basi itakua kasheshe.
  Ishu kama hizo zinapelekwa kule Jukwaa la Dini.

  Shukran.
   
 15. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Roger nimekupata.
   
Loading...