Sikuwa msikilizaji sana wa Clouds. Yapata kama mwaka na kidogo hivi nikashawishika kuisikiliza hasa vipindi vya asubuhi kabla sijaingia mzigoni. Kwa kiasi nilianza kupenda pale walipokuwa "Critique" kwa watumishi wa uma au watu walioshika dhamana. Ukosoaji wao ulinishawishi kuamini kuwa ni sauti au radio ya watu. Nika-extend my hearing mpaka vipindi vya jioni. Huko nikakutana na kibonde. Haikunichukua muda mrefu kuwa fade-up na radio hiyo na kuacha kabisa kuisikiliza. Ilikuwa ni Kibonde, kama ambavyo nimesoma baadhi ya maoni hapo juu, ilikuwa dhahiri huyu mtu ameingia kwenye pay roll ya Mafisadi. Bila aibu wala haya, utamsikia akisifa vilivyooza na kunuka, na kuponda vinavyong'ara. Haihitaji akili nyingi kuacha kumsikiliza. Ndio maana huo utumbo ambao ameufanya leo nimeusoma humu jamvini. Siwezi kumpa hata sekunde yangu moja kumsikiliza. Hata pale anapojipendekeza kuwa MC kwenye matukio fulanifulani. Sio tu KUMPUUZA, bali KUTOKUMSIKILIZA kabisa. HANA ANCHOWEZA kukuelimisha.