Sijui kama unaelewa unachokisema, kwani hizo machine hua zinaangalia kinachonunuliwa dukani? Si ni muuza duka ndio anaeingiza DATA? Kwamfano nimenunua shati la Tsh 25,000/= hivi muuzaji akiamua kuandika Tsh 18,000/= machine itakataa? Yaelekea unaishi ulimwengu mwingine na sio hu, hizo machine sio suruhisho hata kidogo, twende hata kwenye mishahara kwafano, mishahara ya Wabunge, mawaziri ni ya kawaida sana tu (ambayo inastahiri kukatwa PAYE) lakini angalia miposho (hua haiandikwi kwenye salary slip) mafuta lita
50@2500 kila siku, posho za kukaa, 200k, matengenezo ya gari, dereva na mfuko wa jimbo, ukijumlisha vyote vinaleta kama Tsh 12,000,000/= lakini mshahra wa Mbunge kwa maana ya basic salary 1,800,000/= tu na hizo ndizo zinazokatwa kodi. Kwa kusema hivyo hata mfanya biashara nae akitaka anafanya tu hivyo hivyo!