Ee Mungu iweke roho yake mahali pema peponi

mediaman

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
451
687
Ooh, ni huzuni, ni majonzi, ni maombolezo. Mwenzetu ametutoka akiwa bado kijana. Alikuwa mwema sana, tena mkarimu. Hakupenda ugomvi, fitina wala chuki. Hakuwa mchoyo wala bahili. Wote waliokuwa wakimuomba awakopeshe pesa, walipewa mikopo tena bila masharti. Na wale walioshindwa kurudisha mikopo aliwasamehe bure tu. Akisikia jirani anaumwa, haraka sana alikuwa anaenda kumuona na kumpa pole.

Akiombwa kuchangia sherehe, ujenzi au gharama za misiba, hakusita kutoa mchango. Alikuwa anamiliki nyumba nzuri ya kisasa na magari ya kifahari lakini hakujivuna wala kuwa na kiburi. Unyenyekevu ilikuwa sehemu ya tabia yake. Akialikwa arusini alikuwa anakaa viti vya nyuma. Alikuwa msomi mwenye shahada ya uzamivu. Hata hivyo hakupenda kujikweza wala kuonekana mtu mkubwa. Akisikia ndugu wamefarakana alikuwa wa kwanza kwenda kuwapatanisha. Akisikia mtu amekatishwa tamaa na jambo fulani anamtia moyo kwa maneno mazuri ya faraja. Kinywa chake kilikuwa hakitoi matusi wala maneno ya kashfa au dharau. Alikuwa anampenda sana mke wake. Hakuwahi kumpiga kofi wala ngumi tangu walipooana. Hakika alikuwa mtu mwema sana. Ee Mungu iweke roho yake mahali pema peponi.

Hakukosea aliyesema ‘duniani sisi wanadamu ni wasafiri na wapitaji.’ Magonjwa, ajali, vita nk vinatuondoa duniani hata kabla ya wakati wetu kufika. Hakuna anayeweza kukwepa kifo. Kuna takwimu fulani zinasema kwamba takriban watu 150,000 wanaaga dunia kila siku kwa sababu ya magonjwa tu! Kwa sababu hiyo, misiba imekuwa ikishuhudiwa kila siku pia. Na kila mara wakati wa maziko/mazishi huwa tunawasikia viongozi wa dini au wafiwa wakimuomba Mungu aiweke mahali pema peponi, roho ya mpendwa wao aliyeiaga dunia.

Hapa JF, ‘members’ wanajulikana pia kama ‘Great Thinkers.’ Great Thinker, sio mwepesi wa kuamini au kukubali jambo fulani, bila kulitafakari au kulichunguza kwa makini jambo hilo. Na mimi ni miongoni mwao; nimejaribu kuchunguza Maandiko matakatifu kuhusu sala au maombi hayo tunayomuomba Mungu kwamba awaweke mahali pema peponi wenzetu waliotutoka. Je, Mungu anasikia maombi hayo na kufanya kama tunavyomuomba? Kwa utafiti wangu mdogo, nimegundua Mungu hafanyi kama tunavyomuomba. Mtu akifa, sekunde ile ile roho yake ama inaingia mahali pema peponi au inaingia kuzimu kwenye mateso. Maombi yetu hayawezi kamwe kubadili mahali roho ya mtu inapowekwa. Nimehakikisha hilo kwa kusoma Luka 16:19-31. Kwa sababu hiyo tufanye bidii kuishi maisha mema/matakatifu(Waebrania 12:14) ili siku tukiondoka duniani tuwe na uhakika kwamba Mungu atatuweka mahali pema peponi na kutupatia pumziko na raha ya milele.
 
Maua hunyauka, story huisha na kumbukumbu pia husahaulika. Hii inamaanisha sote dunia tunapita.

Ni kweli, mkuu.

1 Pet 1:24-25​

Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka; Bali Neno la Bwana hudumu hata milele.
 
The gods envy us. They envy us because we’re mortal, because any moment may be our last. Everything is more beautiful because we’re doomed. You will never be lovelier than you are now. We will never be here again.
 
Ooh, ni huzuni, ni majonzi, ni maombolezo. Mwenzetu ametutoka akiwa bado kijana. Alikuwa mwema sana, tena mkarimu. Hakupenda ugomvi, fitina wala chuki. Hakuwa mchoyo wala bahili. Wote waliokuwa wakimuomba awakopeshe pesa, walipewa mikopo tena bila masharti. Na wale walioshindwa kurudisha mikopo aliwasamehe bure tu. Akisikia jirani anaumwa, haraka sana alikuwa anaenda kumuona na kumpa pole.

Akiombwa kuchangia sherehe, ujenzi au gharama za misiba, hakusita kutoa mchango. Alikuwa anamiliki nyumba nzuri ya kisasa na magari ya kifahari lakini hakujivuna wala kuwa na kiburi. Unyenyekevu ilikuwa sehemu ya tabia yake. Akialikwa arusini alikuwa anakaa viti vya nyuma. Alikuwa msomi mwenye shahada ya uzamivu. Hata hivyo hakupenda kujikweza wala kuonekana mtu mkubwa. Akisikia ndugu wamefarakana alikuwa wa kwanza kwenda kuwapatanisha. Akisikia mtu amekatishwa tamaa na jambo fulani anamtia moyo kwa maneno mazuri ya faraja. Kinywa chake kilikuwa hakitoi matusi wala maneno ya kashfa au dharau. Alikuwa anampenda sana mke wake. Hakuwahi kumpiga kofi wala ngumi tangu walipooana. Hakika alikuwa mtu mwema sana. Ee Mungu iweke roho yake mahali pema peponi.

Hakukosea aliyesema ‘duniani sisi wanadamu ni wasafiri na wapitaji.’ Magonjwa, ajali, vita nk vinatuondoa duniani hata kabla ya wakati wetu kufika. Hakuna anayeweza kukwepa kifo. Kuna takwimu fulani zinasema kwamba takriban watu 150,000 wanaaga dunia kila siku kwa sababu ya magonjwa tu! Kwa sababu hiyo, misiba imekuwa ikishuhudiwa kila siku pia. Na kila mara wakati wa maziko/mazishi huwa tunawasikia viongozi wa dini au wafiwa wakimuomba Mungu aiweke mahali pema peponi, roho ya mpendwa wao aliyeiaga dunia.

Hapa JF, ‘members’ wanajulikana pia kama ‘Great Thinkers.’ Great Thinker, sio mwepesi wa kuamini au kukubali jambo fulani, bila kulitafakari au kulichunguza kwa makini jambo hilo. Na mimi ni miongoni mwao; nimejaribu kuchunguza Maandiko matakatifu kuhusu sala au maombi hayo tunayomuomba Mungu kwamba awaweke mahali pema peponi wenzetu waliotutoka. Je, Mungu anasikia maombi hayo na kufanya kama tunavyomuomba? Kwa utafiti wangu mdogo, nimegundua Mungu hafanyi kama tunavyomuomba. Mtu akifa, sekunde ile ile roho yake ama inaingia mahali pema peponi au inaingia kuzimu kwenye mateso. Maombi yetu hayawezi kamwe kubadili mahali roho ya mtu inapowekwa. Nimehakikisha hilo kwa kusoma Luka 16:19-31. Kwa sababu hiyo tufanye bidii kuishi maisha mema/matakatifu(Waebrania 12:14) ili siku tukiondoka duniani tuwe na uhakika kwamba Mungu atatuweka mahali pema peponi na kutupatia pumziko na raha ya milele.
Kwanza kabisa, thibitisha huyo Mungu yupo.
 
pepon ni wap mkuu?
 
Unajuaje aliyewaumba ni Mungu?

Yani hapo ni sawasawa na kusema Toyota imeumbwa na Mjerumani, kwa sababu Toyota ni lazima iwe na muumbaji.

Sasa unajuaje muumbaji ni Mjerumani na si Mchina au Mjapani?
Mwenye uwezo wa kuumba binadamu ni Mungu Mwenye Enzi pekee. Unamjua Mungu Mwenye Enzi?
 
Unaweza kuthibitisha huyo Mungu mwenye enzi yupo kweli na kwamba habari za kuwepo kwake si za kutungwa na watu tu?
 
Back
Top Bottom