Ee mama yangu Tanzania ni lini watoto wako watapata furaha ya maisha kama wengine!!

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Ndugu zangu,

Nikitafakari mwenendo wa nchi yetu kisiasa, kiuchumi na kijamii katika kipindi cha uongozi wa JK, nashawishika kuhitimisha kuwa pengine kuna laana fulani inayoitafuna nchi hii. Hivi sasa, wakati wenzetu waganda, wakenya na warwanda wakiendelea kujenga uchumi wao kwa kasi nzuri, sisi ndiyo tunazidi kudidimia. Hali ya maisha imeendelea kuwa ngumu kwa wananchi wa kawaida. bidhaa mitaani hazishikiki kwa bei kubwa. Jambo linalosikitisha ni kwamba kati ya nchi nilizotaja hapo juu, hakuna hata moja yenye rasilimali nyingi kama Tanzania.

Mwishoni nimeishia kulia tu moyoni mwangu"Ee mama yangu Tanzania ni lini watoto wako watapata furaha ya maisha kama wengine!!".
 
CCM kuendelea kutawala nchi hii ndiyo laana yenyewe, kuipa CCM madaraka ni sawa kuwakabidhi nguruwe walinde shamba la mihogo.Tukatae tukubali chanzo cha madhila yanayotukumba watanzania ni utawala wa kishetani na kifisadi wa CCM, tukishindwa kulielewa hili hakuna muujiza unoweza kufanyika kutuondoa katika dhiki hii kuu.
 
Kwa nini tusiende sambamba na libya au algeria au bahrain kuuondoa utawala dhalimu wa ccm?
 
Back
Top Bottom