Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

Maamuzi yameshatolewa ndo hayo kubaliana nayo tu hata kama hukujiandaa kisaikolojia. Japo ulijiapiza kuwa huwezi kukatwa kwa vile eti upo CCM tangu kuanzishwa kwake lakini ndo hivyo tena yamekuwa hata wenzako pia walikuwemo vile vile.

Ulizua misemo mingi kipindi hiki kama vile HAKATWI MTU, PATACHIMBIKA, HUWEZI KUZUIA MAFURIKO, yote hiyo ilikuwa ni mikwara yako ambayo labda kwa namna moja ama nyingine imekuponza kwa vile ulikuwa kama unaitishia CCM na ngazi zote za juu za maamuzi na uteuzi.

Najua imekuuma sana kutokana na jinsi ulivyokuwa umeikamia nafasi hiyo ya juu kabisa kitaifa lakini kumbuka asiyekubali kushindwa si mshindani. Siasa ndo zilivyo hata wewe unazijua.

Kwa heri mzee wa safari ya matumaini amini tu kuwa umeshakatwa na hakuna rufaa.
Pole sana pia wapambe na wafuasi wake wote.

Bado unayo nafasi ya kuondoa umasikini katika nchi kwa vile ulisema unakerwa nao.

Ni mimi mpiga kura wa kawaida nisiyefungamana na chama chochote. Nasubiri October nimkate mmojawapo kati ya CCM au UKAWA.
Hahahahaha umempa vipande vyake, hujamkopesha, umempa hamsini zake hahahahaha haya maneno aliwahi kuyasema Mchungaji Gwajima alipomtukana Kadinali Pengo, tatizo alijigamba sana huyu mzee akatuina watnzania ni wenye njaa sana kana kwamba fedha zake ndo kila kitu hata kununua urais sasa kaipata fresh yake
 
Hivi KWA Akili YA Kawaida LOWASSA Kweli. ...!!! Common sense lowasa apite.
 
Haiwezekani mafuriko yakazuiwa na kiganja lazima yatatokea upande mwingine! Take it from me
 
Akubali tu,kundi lao ndio lililowafanyia vituko Salim Ahmed Salim na John Malecela.Sasa zamu yake,malipo hapa hapa duniani ameze tu maumivu wenzake pia waliumia kama anavyoumia yy sasa mkuki kwa.......:banghead:
 
Kuna mtu alikuwa ananikela sana FB alikuwa amejipaka masinzi usoni.

Sasa haone sauti ya wengi ni ya Mungu. EL ana dharau sana. Utafikiri alitufuga.
 
Kuna uwezekano mkubwa wa watu kuzurumika.Ambao mlikuwa hamjalipwa imekula kwenu.
 
Inaumiza kusalitiwa aisee..

Kwa hiyo JKM umeamua kumsaliti msela wako kabisa kabisa yani..Yani umesahau faulo mlizowafanyia wakina Salim kipindi kile mzee hadi ukapitishwa yani umesahau kabisa

Ha ha ha ha....kinachomuumiza zaidi Lowasa ni kumuona Joka la Mdimu kwenye top 5 aisee,ikakera hadi basi

Yote kwa yote,tukutane October,pole mzee EL ha ha ha
 
Lowassa tuletee balali na pia kigawe chama hicho,ondoka na wabunge wanaokuunga mkono.
 
Back
Top Bottom