Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

Maamuzi yameshatolewa ndo hayo kubaliana nayo tu hata kama hukujiandaa kisaikolojia. Japo ulijiapiza kuwa huwezi kukatwa kwa vile eti upo CCM tangu kuanzishwa kwake lakini ndo hivyo tena yamekuwa hata wenzako pia walikuwemo vile vile.

Ulizua misemo mingi kipindi hiki kama vile HAKATWI MTU, PATACHIMBIKA, HUWEZI KUZUIA MAFURIKO, yote hiyo ilikuwa ni mikwara yako ambayo labda kwa namna moja ama nyingine imekuponza kwa vile ulikuwa kama unaitishia CCM na ngazi zote za juu za maamuzi na uteuzi.

Najua imekuuma sana kutokana na jinsi ulivyokuwa umeikamia nafasi hiyo ya juu kabisa kitaifa lakini kumbuka asiyekubali kushindwa si mshindani. Siasa ndo zilivyo hata wewe unazijua.

Kwa heri mzee wa safari ya matumaini amini tu kuwa umeshakatwa na hakuna rufaa.
Pole sana pia wapambe na wafuasi wake wote.

Bado unayo nafasi ya kuondoa umasikini katika nchi kwa vile ulisema unakerwa nao.

Ni mimi mpiga kura wa kawaida nisiyefungamana na chama chochote. Nasubiri October nimkate mmojawapo kati ya CCM au UKAWA.
 
Misingi 10 ya ACT - Wazalendo na ahadi 5 za mwanachama hazimpi nafasi lowasa kujiunga nacho lakini pia atakibomoa chama maana wanachama wote wa ACT - Wazalendo wanaamini nchi inatakiwa kurejeshwa kwenye misingi. Pole lowasa na team lowasa
 
Raisi hawezi kupatikana CCM. na kama si hivyo Tutegemee udhaifu mkubwa kwenye Taasisi hii nyeti.
 
Kikao chao cha sasa hivi EL amekubali kushindwa na bashe ametangaza nia ya kugombea ubunge nzega mjini hajasema chama ila chadema kuna dalili zote.

Hawezi (Bashe) gombea via cdm maana amekuwa akishambulia chama kupitia kigazeti chake
 
panachimbika hapachimbiki? updates yoyote kama kunachimbika jamani..cc kingunge

Nasikia lowasa alikuwa Katimu bilioni 50 mpaka kufikia usiku wa kuamkia leo km mtaji wa urais.
Watu hawana tatizo. Wanataka hela zake tu. Wengi wanaona kukatwa mapema yake mafungu ya mabilioni yaliyokuwa yametengwa itakuwa ndo basi tena
 
Hahahahahaahha mlijitahidi kuja kwa mbwembwe sasa mmeona Tsunami ilosambaratisha mbwembwe zenu eeenh? Next time nawashauri mpunguze mbwembwe na msidhani fedha ndo kila sehemu inapenya, sehemu nyingine zinafeli kama zilivyofeli kwenu, oneni sasa mzee wenu alivyomwaga fweza lukuki kila kona kuhonga ilimradi apite, kaambulia kufuatwa na watu tu kila kona ya nchi lkn kapewa Total Ban, naamini huko alipo haamini kilomtokea lkn ndo basi tena, sisi hatununuliwi kwa hela zake yeye sasa akanywe supu na hizo hela zake pamoja na wale wanaomfata kama inzi. Hahahaha pole mzee Lowahaswa! Kubali matokeo Welcome again!
 
maamuzi yameshatolewa ndo hayo kubaliana nayo tu hata kama hukujiandaa kisaikolojia. Japo ulijiapiza kuwa huwezi kukatwa kwa vile eti upo ccm tangu kuanzishwa kwake lakini ndo hivyo tena yamekuwa hata wenzako pia walikuwemo vile vile.

Ulizua misemo mingi kipindi hiki kama vile hakatwi mtu, patachimbika, huwezi kuzuia mafuriko, yote hiyo ilikuwa ni mikwara yako ambayo labda kwa namna moja ama nyingine imekuponza kwa vile ulikuwa kama unaitishia ccm na ngazi zote za juu za maamuzi na uteuzi.

Najua imekuuma sana kutokana na jinsi ulivyokuwa umeikamia nafasi hiyo ya juu kabisa kitaifa lakini kumbuka asiyekubali kushindwa si mshindani. Siasa ndo zilivyo hata wewe unazijua.

Kwa heri mzee wa safari ya matumaini amini tu kuwa umeshakatwa na hakuna rufaa.
Pole sana pia wapambe na wafuasi wake wote.

Bado unayo nafasi ya kuondoa umasikini katika nchi kwa vile ulisema unakerwa nao.

Ni mimi mpiga kura wa kawaida nisiyefungamana na chama chochote. Nasubiri october nimkate mmojawapo kati ya ccm au ukawa.

kwa heri mzee wa safari ya matumizi
 
Back
Top Bottom