Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

Tumeshuhudia akiidumaza Monduli kuwa miongoni mwa wilaya duni kuliko hata Longido, achilia mbali Karatu. TUMEMSHUHUDIA AKINYANYASA MAAFISA WATENDAJI WAVIJIJI BILA UTARATIBU HUKU AKIFANYA URAFIKI NA MAFISADI NA YEYE AKIITWA GAMBA KUU. KWA KWELI MTU HUYU HAFAI

Uko duniani au Kaburini maana unachoandika kama marehemu
 
SAFARI ya matumaini kuelekea ikulu imewadia. Tulianza pamoja kwa umoja na tutamaliza pamoja kwa umoja. Tumaini letu ni kwa mgombea mwenye maamuzi.

Njoooni hapa wana LOWASSA tupeane update kwa yanayojili tangu sasa mpaka magogoni. TAREHE 30 mei 2015 Mr Edward Ngoyai lowasa kwa kishindo kikubwa azindua safari ya matumaini jijini arusha. Maelfu wamiminika. Mzee msukuma, kangi lugola na Mzee Kingungwe wasababisha mtikisiko taifa.

Endelea kufahamu kidogo kidogo kuhusu Lowassa

Lowassa alizaliwa tarehe 26 August 1953 mkoani Arusha. Ni waziri wa 8 wa JMT akipokea kijiti kutoka kwa Mh Fredrick Sumaye kutoka 30 Desemba 2005 hadi 7 Februari 2008 na kumuachia Mh Mizengo Pinda ambaye hadi tunavyooandika hapa ndie waziri mkuu wa JMT nae ametangaza nia ya kugombea urais kwa tiketi ya ccm mwaka 2015!


Kabla ya kuwa waziri mkuu, Lowassa alikuwa waziri wa Maji na Maendeleo ya mifugo kuanzia mwaka 2000 hadi 2005 akiwa chini ya rais Mkapa. Wizara hii alimuachia Mh Stephen Wassira baada ya yeye kuteuliwa kuwa waziri mkuu mwaka 2005. Aliingia bungeni kama mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM mnamo Novemba, 1995.

Lowassa aliwahi kuwa waziri katika ofisi ya waziri mkuu kipindi cha pili cha urais wa Mh Ali Hassan Mwinyi. Mwaka 1995 alianza harakati zake za kuwania urais wa JMT ndani ya CCM. Hakufanikiwa kupata ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM mwaka huo wa 1995 hivyo aliamua kugombea ubunge wa jimbo la monduli na kushinda kwa zaidi ya 90%.

Mnamo mwaka 1997 aliteuliwa kuwa waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais - mazingira na umaskini. Lowassa alidhihirisha uwezo wake wa kiongozi zaidi akiwa waziri wa Maji na Mifugo kuanzia mwaka 2000 hadi 2005.

Mwaka 2005 Lowassa aliacha harakati zake za kuusaka urais badala yake akaanza harakati za kumuunga mkono Mh Jakaya Kiwete kwenye mbio zake za urais. J Kikwete alikuwa ni rafiki yake wa muda mrefu sana, naye Lowassa alikubali kuwa campain manager kwenye mbio zake urais, ambapo Mh Jakaya Kikwete alishinda urais wa JMT kwa zaidi ya 80% chini ya menejimenti ya Lowassa

Elimu ya Edward Lowassa

Lowassa alipata shahada yake ya sanaa na elimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Shahada ya uzamili ya Maendeleo ya jamii kutoka Chuo Kikuu cha Bath kilichopo UK.

Elimu yake ya sekondari alipata kutoka shule ya Ilboru moja ya shule maalum kwa ajili ya wanafunzi wenye vipaji maalum darasani wakati huo; na kumalizia elimu yake ya kidato cha 5 na 6 kutoka shule ya sekondari Milambo mwaka 1977. Lowassa anapozungumzia maendeleo anajua anachozungumzia, habahatishi.

General summary kuhusu utumishi wa Lowassa


  • Mkurugenzi Mtendaji, AICC, 1989 - 1990
  • Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais (Sheria na mambo ya bunge), 1990 - 1993
  • Waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi, 1993 - 1995
  • Waziri wa nchi, makamu wa rais - mazingira na umaskini, 1997 - 2000
  • Waziri wa maji na mifugo, 2000 - 2005
  • Waziri Mkuu, 30 Desemba, 2005 - 7 Februari 2008

Alianza kuwa mbunge tangu mwaka 1990, na kuteuliwa kuwa waziri kama tulivyoonyesha hapo juu! Hadi sasa bado ni mbunge alietia nia kuwania urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2015

Kauli mbiu yake: Safari ya matumaini.



[Poleni sana mafisadi team, mtachungulia tu magogoni. Sisi watanzania tunaenda kumshangaa kwenye majukwaa kwani tunamfahamu kuwa ni FISADI, JIZI, MZEE WA VISASI (Ole Moloimiet, Mama Teveli), MWONEVU(waulize kina Hendri-Mtowambu, Sironga, Sanare, Late Diwani Ramadhani-Mtowambu, late Diwani Pello-Makuyuni, MTUMIA MADARAKA VIBAYA(waulize kina Lekule Laiser, Elisa Mollel, Mam Teveli(mkurugenzi aliyemfukuza kazi kwa kisingizio cha kutokugawa chakula cha msaada) n.k.
Hapo Kwenye redi: unampa sifa ambazo hana hajasoma Ilboru kasoma Arusha sec. Halafu unasema alikuwa campaign manager wa Kikwete na Kikwete kashinda kwa asilimia zaidi ya 80 sawa kabisa, lakini walitumia mbinu hizihizi chafu za kuwahadaa watanzania na kuwachafua watu (eg. Mz. Salim na Sumaye) kiasi kwamba jamii ikawaona kama kinyaa. na matokeo yake ni kupeana nafasi kishikaji na kulipa fadhila na mwisho walishindwa kufanya kazi kabisa ni wizi mtindo mmoja then baada ya miaka 5 jamaa akadrop from 80% to 60% kwanza za magumashi). MNATAKA MTURUDISHE HUKO???????????? HATURUDI NG'O!!!!!!!!!!!!!!!. TUMEJANJARUKA. HAYO MLIOVUNA YANAWATOSHA, BASI.]
 
Hii kauli aliitoa jana lowasa akiwa morogoro kuhusu matatizo ya watu wa morogoro, kauli hii imenipelekea kuuliza maswali yafuatayo,

1, kweli tunaitaji rais wa kutegemea msaada wa tume kufanaya maamuzi?

2, kweli tunaitaji rais wakutengemea tume kuongoza nchi?

3, tume ambazo zimekuwa zikiundwa na hazijibu matatizo ya wananchi lowasa anaona ndo njia sahihi ya kutumia ?

4, maamuzi magumu anayotuaminisha kuwa atayafanya yako wapi? Kama anategemea msaada wa tume?

5, tume zilizoundwa zimeleta majibu kwa wakati mwafaka kwa wananchi?

Kwa maswali haya naona lowasa sio rais anayeweza kutusaidi kama mpaka sasa anajpanga kutumia tume kufanaya maamuzi ya msingi na kuongoza nchi bali tunamtaka rais anayeweza kusimama yeye mwenyewe na kufanya maamuzi kwa wakati mwafaka,

wanajif rais anayejipanga kutumia tume ili kufanya maamuzi ndo rais anayetakiwa kwa sasa ili kututoa mahali tulipo kwenda tunapotaka kwenda?
 
Mungu akikuinua nani anaweza kukuzuia..!?
Lowassa kainuliwa na Mungu wa mbinguni, mtashaaa...!!! Tatizo nyotaaaa...!!!!
 
Tunatoa shukrani za dhati kwa wote waliojitokeza kumdhamini na kumsikiliza Mh. Edward Lowassa katika mikoa yote aliyofika. ASANTENI SANA.

"Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu"
 
Mbwembwe zote wadhamini kiduchu hivyo, hama kweli hakika huyu atakiwi, kutumia bil 200 kuambulia wadhamini 870,000!!!
 
kaambiwa atafute wadhamini mikoa 15 yeye akenda mikoa 31,akaambiwa watu 450 yeye maelf, je alielewa amelekezo ya chama chake? mtu asiyefata maelekezo ya viongozi wake hana sifa ya kuwa kiongozi.
 
bado hana jipya wala sio kuwa anakubalika na hakuna neno zito,uzito wake uko wapi? nenda kuria unaenda kushoto then unasema neno zito? hatahivyo watu wanaotakiwa kupiga kura ni 24 mil waliojitokeza kwa njia za magumashi hata 1mln haifiki je hao wengine wako wapi? na anajua wako nyuma ya nani?
 
Walitakiwa 450 tu kwa mikoa 15, hao wengine wanini? Mwambie aache sifa za kijinga.

Mkuu mi sioni kama kuna tatizo japokuwa mbegu inayosababisha MIMBA ni ile ya kwanza tu lakini MUNGU akafanya zikawa zinatoka na nyingine nyuma yake unadhani kakosea kwenye UUMBAJI wake.................tunaweza tusijue kwa nini lakini yeye kama MUUMBA anajua na inaweza kuwa na maana kubwa tu pengine zaidi ya unavyofkiria kiongozi sidhani kama kuna tatizo juu ya hilo mkuu.
 
Kama ameshindwa kuelewa maelekezo ya chama je katiba ya nchi itakuwaje, je siataendesha nchi kibabe
 
Unajua mie hadi sasa sijaelewa kama CCM walitoa maagizo ya wagombea kukusanya wadhamini wengi kadiri iwezekanavyo. Lowassa amekuwa akilitumia sana hili, na kuliweka mbele sana magazetini nk. Lakini najiuliza, ina mana wagombea wengine walishindwa kuonyesha wingi wa wadhamini wao au walichukua tu idadi inayotakiwa ya wadhamini kila mkoa, kulingana na maagizo ya CCM?

Nakumbuka Muhongo alipeleka DVD akaambiwa hazitakiwi kwenye kurudisha form za ugombea, sasa vipi Lowassa na hii 870,000?

Mie nadhani kwa jinsi Lowassa alivyotumia hili suala la wadhamini ni sababu mojawapo tosha ya kumwambia ana silka ya kukiuka utaratibu, na kwamba alikuwa akifanya kampeni badala ya kutafuta wadhamini. Mwache akaangwe kwa mafuta yake mwenyewe. Maana kufanya kampeni kwa kutumia mgongo wa kutafuta wadhamini ni kutowatendea haki wagombea wengine wa CCM, hasa ukiangalia kwamba sasa anajinadi kwamba alipata wadhamini 870,000 tofauti na wagombea wengine wa CCM. Kwani CCM iliweka ushindani wa kuwa na idadi kubwa ya wadhamini kwa wagombea?

Huyu jamaa kweli mara nyingine haoni mbali juu ya athari za mambo anayofanya. Amekuwa so blinded na kutaka kuwa raisi kiasi kwamba yuko tayari kufanya lolote ili aupate. Kwani Ikulu kuna nini kwa mtu kama Lowassa?

Mtu mwenye obsession ya Ikulu namna hii ni wa kutilia shaka sana.

acha wivu wa kike kila mtangaza nia amezidisha idadi coz sheria inaruhusu! mwenye wachache ana 650!
Nimeongelea kuona mbali, sijui kama umefikiria mbali. Wewe unadhani kwa jinsi Lowassa anavyotumia hili suala la udhamini wa watu 870,000 kujinadi, linawaweka wapi wagombea wengine wa CCM? Unfair playing ground. Huwezi kutambia kitu ambacho hakipaswi wala hakikuwa sehemu ya makubaliano ya utaratibu wa kutafuta mgombea. Hata kama alipata 870,000 kwa kuwa hukukuwa na zuio juu ya idadi kubwa, na kwenda mikoa 31 badala ya 15, alipaswa kukaa kimya sio kuanza ku-jipromote kwa namna anayotaka kuielezea jamii kwamba yeye ni bora zaidi ya wagombea wengine wa CCM kwa sababu alipata wadhamini 870,000 na kwenda mikoa 31.

Pia fikiria uteuzi ujao wa wagombea uchaguzi wa 2025. Kama Lowassa akipita kuwa Mwenyekiti wa CCM na Raisi kipindi hiki, basi kutakuwa na ushindani mkubwa kwa wagombea wa CCM nao kutaka idadi kubwa na kwenda mikoa yote ya Tanzania, wakijua kwamba hicho ni kigezo muhimu kwa Lowassa. Fedha nyingi itabidi zitumike kwenye kutafuta udhamini, ambapo tayari unabagua wagombea wa CCM ili wawe wale tu wenye uwezo wa kifedha. Lowassa atakuwa ameweka "precedent" na sasa itakuwa ni vurugu tupu suala dogo tu la kutafuta wadhamini.

Kwani CCM waliposema angalau mikoa 15 hawakujua Tanzania ina mikoa zaidi ya 30? na waliposema wadhamini 450 hawakujua CCM ina wanachama zaidi ya milioni 4? Kwa ujumla, alichofanya Lowassa kinaonyesha wazi hana uwezo wa kufikiria mambo kwa umakini kabla ya kutenda.

Ninakata shauri kwamba Lowassa ni aina ya watu ambao wanadhani mtu akiwa na pua kubwa basi atatoa kamasi nyingi!
 
Kama ni kweli wanachama hai wa CCM Tanzania nzima wapo mil 6, basi jamaa kajizolea 14.4%.
 
kaambiwa atafute wadhamini mikoa 15 yeye akenda mikoa 31,akaambiwa watu 450 yeye maelf, je alielewa amelekezo ya chama chake? mtu asiyefata maelekezo ya viongozi wake hana sifa ya kuwa kiongozi.

Ni kuanzia Watu 450 na Siyo Mpaka watu 450!

 
kaambiwa atafute wadhamini mikoa 15 yeye akenda mikoa 31,akaambiwa watu 450 yeye maelf, je alielewa amelekezo ya chama chake? mtu asiyefata maelekezo ya viongozi wake hana sifa ya kuwa kiongozi.

sheria inasema mikoa kuanzia 15 sio mwisho ndo 15 na pia wadhamini angalau 450 hiyo ni minimum so unaweza zidisha ! acha wivu wa kike
 
Hivi babu dr. Bilali kapata wadhamini jumla wangapi?
Naomba kujuzwa .....
attachment.php
 
Back
Top Bottom