Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

acha wivu wa kike kila mtangaza nia amezidisha idadi coz sheria inaruhusu! mwenye wachache ana 650!

Nimeongelea kuona mbali, sijui kama umefikiria mbali. Wewe unadhani kwa jinsi Lowassa anavyotumia hili suala la udhamini wa watu 870,000 kujinadi, linawaweka wapi wagombea wengine wa CCM? Unfair playing ground. Huwezi kutambia kitu ambacho hakipaswi wala hakikuwa sehemu ya makubaliano ya utaratibu wa kutafuta mgombea. Hata kama alipata 870,000 kwa kuwa hukukuwa na zuio juu ya idadi kubwa, na kwenda mikoa 31 badala ya 15, alipaswa kukaa kimya sio kuanza ku-jipromote kwa namna anayotaka kuielezea jamii kwamba yeye ni bora zaidi ya wagombea wengine wa CCM kwa sababu alipata wadhamini 870,000 na kwenda mikoa 31.

Pia fikiria uteuzi ujao wa wagombea uchaguzi wa 2025. Kama Lowassa akipita kuwa Mwenyekiti wa CCM na Raisi kipindi hiki, basi kutauwa na ushindani mkubwa kwa wagombea wa CCM nao kutaka idadi kubwa na kwenda mikoa yote ya Tanzania, wakijua kwamba hicho ni kigezo muhimu kwa Lowassa. Fedha nyingi itabidi zitumike kwenye kutafuta udhamini, ambapo tayari unabagua wagombea wa CCM ili wawe wale tu wenye uwezo wa kifedha. Lowassa atakuwa ameweka "precedent" na sasa itakuwa ni vurugu tupu suala dogo tu la kutafuta wadhamini.

Kwani CCM waliposema angalau mikoa 15 hawakujua Tanzania ina mikoa zaidi ya 30? na waliposema wadhamini 450 hawakujua CCM ina wanachama zaidi ya milioni 4? Kwa ujumla, alichofanya Lowassa kinaonyesha wazi hana uwezo wa kufikiria mambo kwa umakini kabla ya kutenda.

Ninakata shauri kwamba Lowassa ni aina ya watu ambao wanadhani mtu akiwa na pua kubwa basi atatoa kamasi nyingi!
 
Mwe!

For real, Tanzania is completely tired of Lowasa's drama.

Yaan kila mtu anatupia #snitching tu kwa uyu MWIZI. Navishauri vikao vya chama vimwondoe mapema ili aibu iwe ndogo kuliko baadae zaid.

Kila Mtanzania hapendi kusikia jina hili. **unless kwa wale #wanufaika tu!** Maybe be nakwa wale wasiojua vizuri UHUNI aloifanyia nchi.
 
Hivi babu dr. Bilali kapata wadhamini jumla wangapi?
Naomba kujuzwa .....
attachment.php

... Naona Jambazi Anacheka
 
Huyu jamaa ni kama fisi mwenye njaa kali aliyeona mzoga uko mbele yake na kuna vizuizi hapa katikakti kwahiyo anataka kufanya liwalo na liwe ili apate mzoga huo. Hafai kabisa
 
Jamaa linapiga kampeni kwa mgongo wa kutafuta wadhamini.

Hao wadhamini 870,000 ni wengi kwa wapi wachache ili hadi wawe sauti ya Mungu?

Nani alimwambia anatakiwa kushindana na wenzake kwa idadi ya wadhamini kwamba atakayepata wengi ndiye Sauti ya Mungu?

Kanuni ilikuwa mikoa 15 wadhamini 450. Huko kote mikoa 30 na watu 870,000 ni maelekezo ya nani kama siyo mwendelezo wa hila zake za kisanii kuwatishia ccm?


Wapiga kura wa Tanzania ni zaidi ya 25,000,000. kati yao 3,000,000 ni wanachama waliosalia ccm. sasa yeye anaposema 870,000 ni wengi kwa hesabu ipi? Wengi kuzidi wapi, kwa hesabu gani?

Kweli huyu jamaa ni mwehu!.

Ni kwei kwamba ccm haituhusu Watanzania. Lakini jamaa linaudhi kinoma pale lilnapozidi kuonhesha dharau kwa Watanzania kwamba ni majuha hawana uwezo wa kulinda maslahi wala kuliadhibu kwa ufisadi wake.

Sasa ni hivi Ccm walipitishe tu kama walivyofanya kwa jk. Liambulie hizo kura 780 Tanzania nzima. Hata kama wanaccm wote wakiogopa ku Kolimbwa waamue kumuunga mkono, wapike pilau wavae sare wacheze mchezo wowote wachezao lakini hatavuka nje ya kura za wanacch wasiozidi 3,000,000.

The rest tutasimama na taifa letu, tunapigia kura UKAWA na kwa wingi wetu, tunalinda kura zetu. Hawa ccm kwa kuwa wamezoewa ufisadi, hata wakitusliti waungane na fisadi Lowasa, watapiga kura ambazo hazizidi 3,000,000.

Ccm bye bye!.
 
Walitakiwa 450 tu kwa mikoa 15, hao wengine wanini? Mwambie aache sifa za kijinga.

Ha ha ha...
Mtajuaje sasa kama ana marafiki kibao wanampenda na anakubalika na watanzania wengi kuliko wengine wote?
Na je huoni kama wakati wake wa kufanya kampeni ndo ulikuwa sasa ili atakapotangazwa ye amalizie kiduchu tu ?
 
Jamaa linapiga kampeni kwa mgongo wa kutafuta wadhamini.

Hao wadhamini 870,000 ni wengi kwa wapi wachache ili hadi wawe sauti ya Mungu?

Nani alimwambia anatakiwa kushindana na wenzake kwa idadi ya wadhamini kwamba atakayepata wengi ndiye Sauti ya Mungu?

Kanuni ilikuwa mikoa 15 wadhamini 450. Huko kote mikoa 30 na watu 870,000 ni maelekezo ya nani kama siyo yake binafsi?


Wapiga kura wa Tanzania ni zaidi ya 25,000,000. kati yao 3,000,000 ni wanachama waliosalia ccm. sasa yeye anaposema 870,000 ni wengi kwa hesabu ipi? Wengi kuzidi wapi, kwa hesabu gani?

Kweli huyu jamaa ni mwehu!.


Kuna upishi mwingi na mbwembwe ila ndo mwisho wa siku chakula kinaweza kutolewa jikoni aidha kibichi au ladha-less
 
acheni kukulupuka kama.chafya
kwan kowassa kupata wadhamini wote haoo na pia kumaliza mikoa yote sauti ya wengi ni sauti ya mungu na ambaliki mtu huyuu aende magogoni

... Labda Aende Kukata Gogo Porini.
 
Jamani katika zoezi lolote la ushindani ni kawaida na ni akili kwa washiriki wote kuonyesha umaarufu na ubora wao kwa mbinu/njia zozote halali. Kitendo cha Lowasa kupata wadhamini wengi na mapokezi makubwa kuliko wenzake ni kielelezo tosha kwamba yeye ni front runner kama kweli Tanzania tunaamini katika utawala wakidemokrasi. Wamarekani hufanya hivyo katika mchujo wa primaires. Kumbe wengine mlitakaje? Tumpate Rais kwa kupiga ramli au tufuate maelekezo ya watu 20 kama tawala za kikomunisti na kupuuza chaguo la malaki na mamilioni?
 
Tabby!! Umesema wapiga kura Tz ni zaidi ya 25 m, lakini unajua wangapi wataandikishwa! Na kati yao wangapi watapiga kura! Unaweza ona ni kati ya hao chini na 3m waliobaki. Mtazamo wangu tu!
 
Hoja yenu dhaifu wananchi wameichoka hakuna atakaye kuelewa sikuhizi ukisema LOWASSA ni fisadi. Pia tumeanzisha uzi huu tutiane moyo, tuufaamishe UMMA wa JF na watanzania kwa ujumla kwamba E.L ni nani hasa cha kushangaza unaingia kichwa kichwa na point zako dhaifu
EL ni msalaba kwa ccm sio nchi mkuu
 
kutokana na spidi aliyonayo huyu "mchukia umaskini"ni wazi anachukua nchi.kumzuia haiwezekani,so naomba anayeweza kuniunganisha na mtandao wake anisaidie ili baada ya uchaguzi nami niwe pema peponi.
 
Umetisha mpiganaji. mimi uchaguzi ulioisha niliwahi kuongea na wasira akatoa nje, hawa jamaa hawatoi mpunga kirahisi
 
Back
Top Bottom