MTARAJIWA RAISI
Member
- Jun 16, 2015
- 84
- 30
Unajua mie hadi sasa sijaelewa kama CCM walitoa maagizo ya wagombea kukusanya wadhamini wengi kadiri iwezekanavyo. Lowassa amekuwa akilitumia sana hili, na kuliweka mbele sana magazetini nk. Lakini najiuliza, ina mana wagombea wengine walishindwa kuonyesha wingi wa wadhamini wao au walichukua tu idadi inayotakiwa ya wadhamini kila mkoa, kulingana na maagizo ya CCM?
Nakumbuka Muhongo alipeleka DVD akaambiwa hazitakiwi kwenye kurudisha form za ugombea, sasa vipi Lowassa na hii 870,000?
Mie nadhani kwa jinsi Lowassa alivyotumia hili suala la wadhamini ni sababu mojawapo tosha ya kumwambia ana silka ya kukiuka utaratibu, na kwamba alikuwa akifanya kampeni badala ya kutafita wadhamini. Mwache akaangwe kwa mafuta yake mwenyewe. Maana kufanya kampeni kwa kutumia mgongo wa kutafuta wadhamini ni kutowatendea haki wagombea wengine wa CCM, has ukiangalia kwamba sasa anajinadi kwamba alipata wadhamini 870,000 tofauti na wagombea wengine wa CCM. Kwani CCM iliweka ushindani wa kuwa na idadi kubwa ya wadhamini kwa wagombea?
Huyu jamaa kweli mara nyingine haoni mbali juu ya athari za mambo anayofanya. Amekuwa so blinded na kutaka kuwa raisi kiasi kwamba yuko tayari kufanya lolote ili aupate. Kwani Ikulu kuna nini kwa mtu kama Lowassa?
Mtu mwenye obsession ya Ikulu namna hii ni wa kutilia shaka sana.
acha wivu wa kike kila mtangaza nia amezidisha idadi coz sheria inaruhusu! mwenye wachache ana 650!