Edward Lowassa special thread


Maneno mengiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii hayavunji mfupa. Tusubiri July.
 

Hivi Lowasa atakuwa na ilani yake au ilani ya CCM!?
 
Hivi Lowasa atakuwa na ilani yake au ilani ya CCM!?

Ilani ya CCM ni bora siajabu klk zote Duniani tatizo liko kwenye Utekelezaji na usimamizi na hapo ndipo Bw.Lowasa anapoziba pengo lililopo CCM!
 
Hivi ni kweli kua bado hajatimiza idadi au ndo kaanza kampeni kimtindo CCM tuambieni!!!!!!!
 
Labda hajatimiza idadi yake yeye hatujui ni wadhamini wangapi. Ila wa CCM ni 450 Tanzania nzima ambao karibia waliochukua fomu wote wametimiza. Labda aulizwe kwake yeye idadi ya wadhamini ni wangapi pengine tutamuelewa.
 
Nikweli ndani ya ccm hakuna wa kumkemea mwenzake kwani mfumo unawalinda lakini kwa mamvi imezidi kiburi jeuri fisadi HAFAI KUWA RAISI.
 
Nafikiri ungekuja na ufafanuzi zaidi pengine wengi tusingekuwa na maswali, lkn kusema tu eti jeuri imemzidi hafai kuwa rais, hapo lazima uzue maswali na pengine tuseme umetumwa au ni chuki binafsi.
 
hivi kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuthubutu kumsimamisha FISADI MKUU kuwania nafasi ya urais??
 
vipi kuna kikao cha dharura kiliitishwa jana na mwenyekit taifa ccm.je kuna mwenye habari
 
I am sure pamoja na matusi yote hapa Lowasa he won't make it . Hakuna wa kumkemea lakini he will be told in the open kwamba hafai na hata amini . Matusi si bisara na haiwezi msaidia Lowasa .
Lowasa ana hasira na amejawa na umimi, hana vision hawezi kujieleza .Kashindwa hata kusema why he stepped down as a PM , kama hahusiki na kashfa then why did he step down ?

Wana CCM wana mheshimu late Mwalimu , so kwa kuwa alisha kataliwa mapema kwa matendo yake nina hakika they are ready to be a cursed political party .Lowasa hana la kutueleza sisi watanzania la kunifanya nimwelewe hana hata mfano kuanza Monduli hadi alikpokuwa Waziri Mkuu . Hana na nasema hana . Tujenge hoja tuone ukweli upi matusi si faida wala msaada kwa a soon ditched Lowasa .
 
Ee Mungu, Wewe Ndo utuchagulie Rais..maana Wewe watizama mioyo na nia Ila Sisi tunatizama kwa macho..Mungu atuchagulie Rais..Wote tuseme Amiin
 
Eti anasema tusiomtaka tuhame, anashindwa kujiuliza
1. Tukishahama yeye atabaki Ikulu kumtawala nani?
2. Ni nchi gani na lini aliona rais anaomba watu awaongoze ila anawatahadharisha wahame kwanza?
3.Tukisema kwa kusema hivyo tayari mgombea kavunja katiba kwa kutangaza mapema vita ya ndani ( civil war ) hats kabla hajawa rais tutakuwa tunakosea?
 
Kama tuliweza kumshitaki Pinda kwa kuvunja katiba akisema wapigwe kwanini isifungiliwe kesi ya kikatiba kwa Lowassa kutishia amani ya nchi hata kabla hajawa rais, huyu akiwa rais si atataka kuichezea katiba yetu ambayo Mwl Nyerere alituhasa asiichezee mtu?
 
Wakuu,

Msafara wa lowassa umepita sasa hivi hapa magomeni mataa wanatokea kariakoo wanaelekea ilala.

Mwanzoni nilizani kuna bodaboda kagongwa na gari maanaa group kubwa la madereva bodaboda wamepita kwa mbwembwe (walikuwa wakipiga honivna kuinua matairi ya mbele ya bodaboda zao).ilinilazimu nisogee nione vizuri ndipo nilipoona msafara wa magari nyumba ya hizo bodaboda.

Huyu mheshimiwa anatisha sana. Yuko vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…