Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

hilo nikweli kabisa na hawaaki kusema kwa kuwa wanajua kabisa kuna wimbi la wanachama wao wengi wameamia upinzani
 
Naona bwana Ngoyai anaitendea haki shahada yake ya Fine & Performing Arts kutoka chuo kikuu cha Dar-es-salaam.
 
Last week nilikuwa mkoani Iringa, Sumbawanga na Mbeya.

Mbeya ndiko nilikaa zaidi, nilitembelea karibu wilaya zote. Nilipokuwa Sumbawanga nilishuhudia Mhe. Lowassa akitua kwa Chopa na kuchukua maandamano hadi ofisi za CCM. Mmoja wa rafiki zangu pale alinieleza kuwa vijana wa bodaboda wanapewa buku10 kila moja kwa kupamba maandamano. Chopa aliyotua nayo naambiwa ni ya Askofu mkuu Gwajima wa Ufufuo na Uzima. Nilipata picha fulani.

Mbeya - tangia Tunduma nilishuhudia gari Suzuki carry ikitangaza na kutafadhalisha wananchi wenye mapenzi mema kwenda kumpokea na kumdhamini Lowassa siku mbili baadaye, barabara nzima hadi Mbeya kulikuwa na gari 3 tofauti zikihimiza watu, wengine wakisema nauli siyo tatizo.

Jijini Mbeya nilishuhudia pia gari 2 zikitangaza ujio wa EL. Kesho yake tulikwenda Kyela hadi Kasumulo, kote kulikuwa na matangazo magari yakizunguka, tulirudi kupitia Mbarali na kutokea Chunya kwenda Singida, kote watu wanaitwa kwenda Mbeya!!!

Ahaaaa! nilitambua Lowassa ni nani, amejitambulisha kwa fedha, fedha za kumwaga, kama ni zake au marafiki sijui, ila nachosema ni kuwa hakuna chengachenga kuwa utafutaji wake wa nfasi ya kwenda magogoni umetawaliwa na matumizi makubwa ya fedha. Narejea hotuba ya mwalimu kuhusu wanaotafuta urais kwa fedha!

Kwa maoni yangu, nasema aheri Lowassa kajidhihiri, wengine je? The floor is open....
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Wadhamini WAnachama wanaotakiwa ni 450 tu na uandikishaji wake haufanyiki uwànjani au kwenye ofisi za chama bali ni kàzi ya kamati maalum yatia nia

Fomu inayotembezwa nyumb ba kwa nyumba na kwenye mikutano ya hadhara ni siasa tu .,.

Ni presha
Ni vitisho

Hakuna mtu msafi ndani yA kitambaa cha kijani na rangi ya njano
 
kwa hili umechemsha ma elfu na ma elfu wengine walikua wanakaa mikoa mingine wamehamia mbeya wamelipia ada zao za uanachama kwenye matawi ya mbeya na mkoa ulioutaja umechemshaa kwa uongo wako
 
Ni kweli lowasa kajidhirisha kuwa ana nia ya dhati kuingia Ikulu, muda huu 8:25 napita maeneo ya Tengeru Arusha, kuna gari inatangaza ujio wa Lowasa leo, huku wanapiga mziki munene ukiimba nyimbo za kumsifu Lowasa. Je wanatangaza bure? hii sio kampeni? Na kama ni dampeni kanuni za ccm hazijakiukwaa? na kama kanuni zimevunjwa ccm wana ubavu wa kulikata jina lake? Yangu macho liwalo na liwe
 
Kisha choka huyo babu anasumbuka na anajua wazi hakuna kichaa wa kumpitisha.
 
Safari ya Matumaini inazidi nawiri, shauku na kiu ya watanzania kuondokana na Umasikini chini ya Balozi wa 4U inakata makasia Kupita Maelezo.

Lowassa anazidi kujijenga ndani na nje ya chama, hili linajidhihirisha Kupitia vuguvugu la mabadiliko la 4u movement. Vuguvugu hilo kwa majibu wa takwimu zilizo tolewa na kiongozi wa vuguvugu hilo ni zaidi ya Milion 5.

Kinacho jidhihirisha sasa ni yale ya baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere kuwa wakati wa mabadiliko ukifika Watanzania watayadai Ndani ya CCM na wakikosa watayadai nje ya ccm, sasa ni wakati wa ccm kuamua kuwa washika dola chini ya Lowassa au kuwa wapinzani.

Source:
Gazeti la Mtanzania.
 
Hata kama ana kura milioni 20, Lowasa hafai kuwa kiongozi wa nchi
 
Hata angepata kura milioni 30 hafai kuwa raisi wa tanzania .
 
Acha utapeli wewe Fisadi awe na kura million tano zitoke wapi? labda hao wachumia tumbo wanaomdhamini hawafiki hata laki tano.
 
safari ya matumaini inazidi nawiri, shauku na kiu ya watanzania kuondokana na umasikini chini ya balozi wa 4u inakata makasia kupita maelezo.

Lowassa anazidi kujijenga ndani na nje ya chama, hili linajidhihirisha kupitia vuguvugu la mabadiliko la 4u movement. Vuguvugu hilo kwa majibu wa takwimu zilizo tolewa na kiongozi wa vuguvugu hilo ni zaidi ya milion 5.

Kinacho jidhihirisha sasa ni yale ya baba wa taifa mwl julius kambarage nyerere kuwa wakati wa mabadiliko ukifika watanzania watayadai ndani ya ccm na wakikosa watayadai nje ya ccm, sasa ni wakati wa ccm kuamua kuwa washika dola chini ya lowassa au kuwa wapinzani.

Source:
Gazeti la mtanzania.

they have a choice
 
Back
Top Bottom