Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

kaka unatumiwa si bure! nitajie kiasi alichoiba lowassa na ushahidi tuwekee hapa!!
 
Alikuibia wapi? Na kama alikuibia uliwahi kumshitaki? Wewe ndiwe unavutiwa na hela zake sio mimi nachovutiwa na utendaji wake wa kazi na uwajibikaji na sio vinginevyo usiwe unaongea vitu usivyo na uhakika navyo pia umegusia kuhusu uchawi wa TB Joshua mimi siamini ktk uchawi na siujui we endelea kuvutiwa nao

Utendaji gani wa firauni lowasa?Au wa kuleta Richmond?
 
huyu jambazi alikuja mwanza akatulaghai tukajitokeza nyomi.Mpaka sasa hela yetu hatujalipwa na Laurence Masha.El ni laghai tulipeni hela zetu au tutatoa siri zake zote
 
Nimesikia tayari yuko mikoani. Ni lini atatia timu Dar ili nijue niombe ruhusa kazini mapema kabisaaa!
 
Matimaini yenu ni kuendelea kugawiwa visenti unyonge huu utaisha lini Tz
 
mnakataaa lowasa hagawi pesa. mby wamevuna kinoma huu mwaka wa née ma coz mazao juu. il à lowasa urais no. waulize ccm walichofanywa kata ya iyela licha ya kugawa pesa.

Mbeya ccm no
 
* Ya Mbeya sio gharika wala mafuriko bali ni MARAMZAMISI...

* Kwa mara nyingine Lowassa avuna wadhamini zaidi ya elfu hamsini na tatu (53,000+)...

* Aweka historia Mbeya...

Baada ya ile gharika ya jana mkoani Kilimanjaro leo hii yaliyotokea mkoa wa Mbeya yamenifanya nikose jina sahihi. Ndipo nilipompigia babu yangu kisha kumueleza na kumuuliza haya yaliyotokea Mbeya tuyaiteje?, manake naona ni zaidi ya gharika ama mafuriko..

Babu akaniambia mjukuu wangu hayo yaliyotokea Mbeya ni maramzamisi, akimaanisha (Maporomoko ya mvua za radi yaliyokuwa yanatokea katika mlima SINAI)...

Ni wazi jiji la Mbeya limefanya kile ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya nchi hii... Lowassa kwa mara nyingine kavunja rekodi kwa kuvuna maelfu na maelfu ya wadhamini kutoka katika mkoa huo (zaidi ya wadhamini 53,000+)....

Pamoja na hilo umati mkubwa sana umejitokeza kutoka pande na viunga vyote vya jiji hilo ili kumlaki na kumsalimia Lowassa, ambaye ameonekana akiwa na nyuso ya furaha alipoona wananchi walivyo na matarajio makubwa ya kuanza safari ya matumaini...

"Hii haijawahi kutokea na sijawahi kuona tokea nizaliwe, huyu ndio mkombozi wetu wa maendeleo tunayemtarajia. Nafikiri hapa ni suala la muda tu ndio linasubiriwa mafuriko haya yanatoa picha halisi ya nguvu ya Lowassa" amesikika Mzee Mole akiongea...

My take: Hii ndio safari ya matumaini, mchakamchaka wa maendeleo...

Asante Mbeya


View attachment 261709

View attachment 261710

View attachment 261711


Yafuatayo ni mhimu sana:
(1)Ni kweli kabisa kuna umati mkubwa unamfuata Lowasa kwa Ushahidi tulio ona
(2)Ni Historia kwa kuwa CCM hawajawahi kupata umati kama huo isipokuwa ni CCM ya Lowasa.
(3)Kama umati huu ungekuwa wa Kweli basi CCM wasingehaha na CHADEMA.
(4)Jambo la Kushangaza idadi ya watu wanaomdhamini Lowasa katika eneo moja ni zaidi ya Wana CCM walioeneo hilo.
Kwa mfano Mbeya Mjina hapo ni vigumu kuamini kuwa kuna wana CCM 53,000. Kumbuka eneo hilo SUGU alishinda kwa Kishindo
(5) Taarifa zilizopo ni kwamba Lowasa anakadi zake za CCM ambapo anagawa siku yeye anapoingia eneo husika
(6)Watu wanajiandikisha kabla hajafika na wakati akifika wanajitokeza kufanya usanii
(7)Hivi ni kweli watu wanaochukua kadi za CCM kwenye kampeni za Lowasa wanaweza kuwa wanachama hai wa CCM??
 
Leo ilikua ni zamu ya watu wa mbeya kuvuna mapesa ya Fisadi mkuu.

Mkuu, acha wavune maana ukweli wenyewe anarudisha pesa alizowaibia watanzania. Wenye bodaboda wana uhakika wa lita tatu za petroli pamoja na Shs elfu 10 kwa mapokezi ya saa moja tu. Mwenye bodaboda anaweza kukaa kijiweni saa kadhaa asipate hiyo hela.

Mwaka itakuwa kula kwa Lowassa, kura kwa UKAWA!
 
Back
Top Bottom