Siku ya udhamini 19/6/2015 mkoani kwa E. Lowassa.
Majira ya saa nane, EL ametinga ofisi za CCM mkoa akiambatana na marafiki zake na amekutana na umati mkubwa uliojitokeza kumpokea.
YALIYOJIRI:
1. Wakati anaingia ofisini, alishindwa hata kutoa mkono kwa wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa. Alikuwa akivuta mguu wake wa kulia na mara alipoketi kwenye kiti chake alionekana kabisa kuwa ana tatizo la kiafya. Aliomba kupumzika kwanza kabla hajatoka nje huku akisema, "naombeni tupumzike kidogo nimechoka sana."
2. Wakati anatoka ofisini kwenda nje kuhutubia watu, alicheleweshwa kidogo akasimama na hapo ndo tulipata kushuhudia namna mzee EL alivyo. Mikono ilikuwa inatetemeka na ikabidi aifiche mfukoni. Ni ukweli usiopingika kuwa mzee Lowassa afya yake si nzuri kwa nafasi ya urais.
3. Sasa baada ya kuwasalimia wana Mbeya, la kushangaza ni kuwa hawakuondoka, wakijua kuwa kuna pesa waliyokuwa wameahidiwa na wafuasi wa EL. Umati wa watu ulibaki eneo la tukio wakisubiri pesa.
Mara mzee akaondoka. Ikabidi wafanye vurugu wakitaka kuvunja mlango wa ofisi ya CCM mkoa ili wapewe pesa, hadi kiongozi mmoja ikabidi awatishie kutoa bunduki kama watavunja mlango wa ofisi. Ilikuwa tafrani kweli.
4. Pamoja na udhamini wote wa watu 53,000, lakini fomu muhimu ya udhamini ilikuwa inapungukiwa na wadhamini 3 hadi jana saa moja, jambo lililopelekea Guninita kuchukizwa na 4U movement waliokuwa Mbeya kuwa hawajafanya lolote. Lakini fomu za udhamini wa Lowassa zimekua mkoani hapa kwa siku 15 sasa wakitafuta wadhamini, sasa wanashindwa kujua kwanini haikukamilika.
5. Mwisho, hadi sasa wana Mbeya wanajuta kwa kudanganywa kuwa watapewa pesa ambazo mwisho wa siku hawakupewa na wanasema kama isingekuwa hizo pesa wasingekuja kabisa.
Hapa wa kulaumiwa ni familia ambayo imekubali kumwacha mzee kutafuta majukumu makubwa ya kuongoza nchi huku wakijua kuwa afya yake si nzuri. Ingefaa familia kukataa ili kumtunza mzazi wao, kadhalika kumlindia heshima yake.
Pia naomba tuanze kuchunguza vizuri majina yaliyoandikwa kwenye fomu hizi na uhalisia. Maana mkoa wa mbeya hauna wanachama wengi kiasi hicho. Yaani kwa lugha nyepesi, huyu bwana anagushi watu na hata saini zao.
Huenda vitabu vya zamani ambavyo vina majina hata ya watu waliokufa vinatumika, na hili linaonekana sana katika wilaya zote ambazo amepata wanachama wengi waliomdhamini.
Chukulia mfano Mbeya ambapo alipata umati wa watu wengi. Ndipo hapo CCM ilishindwa kupata kura japo elfu 10. Nenda Moshi Mjini na Arusha Mjini pia.
Ni muda mzuri sasa kwa chama kuangalia vyema hili zoezi, maana haya matumizi makubwa ya hela na Nguvu ili kuonyesha ulimwengu kuwa anakubalika ni mazingaombwe ambayo lazima yatafutiwe majawabu.
Maana CCM inaweza kuangalia kuwa zoezi hili linakipa nguvu chama, kumbe kuna mtu anatembea na kadi zake na kuwasajili wanachama hewa.
Nimecopy na kupaste hapa kwa mtazamo sahihi.