Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,521
- 96,267
wenye kujua nini wanafanya wameshamaliza kukusanya hizo saini za wadhamini wao na kabaki yeye tu akitafuta umaarufu wa kitoto huku akijichelewesha kurudisha ili azidi kujipatia umaarufu kwa mgongo wa watu wengi wanaojitokeza ambao hata hivyo wengi wao ukiwaangalia tu kwa jicho la tai utagundua kuwa ni watu wanaofanana nae kiakili na wasiojua tanzania inataka nini na kiongozi gani. ataruka sana na hiyo private jet yake na hiyo chopper na ningeshauri hata akiweza atumie hadi spacecraft ila nawahakikishieni huku nikiwa na jeuri, kiburi na nyodo ya 100% kuwa edward ngoyai lowassa hatopitishwa na ccm kugombea urais 12 july 2015. nayasadiki maneno yangu haya na nitakuwa nayasadiki kwenu kila siku hadi ikifika siku ya 23 kutoka leo. ccm haijaenda likizo kihivyo hadi kufikia hatua ya kusahau nini yalikuwa mawazo ya hayati baba wa taifa na watu hawataki kulaaniwa na mzimu wa mwalimu nyerere hivyo watamfurahisha kwa kumpa nchi mtu ambaye hana hata chembe ya rushwa, wizi na umafia. rais akikosekana kati ya hawa dr. magufuli, jaji augustino na professor muhongo huku makamu wao ( mgombea mwenza ) akiwa makongoro nyerere mnitahiri kwa mara ya pili.
Hivi jk hakuwahi kukataliwa na mwl nyerere?