Nevertheless, bunge la mwaka 2015, ataunguruma sana kumbomoa JK na mtandao wake, atahakikisha walomtundika msalabani kwa Richmond, wanasulubiwa!, yeye atasafishwa, atatakatishwa, atakaswa, atapakwa mafuta tayari kwa 2015, kama ni kweli yuko fit, basi mkae mkijua, kama CCM watamsimamisha Lowassa, 2015, ni CCM Tena!.
Mkuu Nyunyu, hakika wewe uu miongoni mwa ma great thinkers wachache sana tulionao humu jukwaani, keep on reading me in between the lines, we'll finally reach there, japo jina la jf ni home of great thinkers, hawa ma great thinkers wengi tulio nao humu, I doubt, if some have even that brain to think, let alone thinking great!.Mkuu Pasco,
Najua wewe ni mfagiliaji wa El toka zama! Nakuhakikishia hapo kwenye red, "over JK's dead body" Hawa jamaa wamekwisha patanishwa na ikashindikana, kisa unafiki na ukigeu geu wa JK. JK ameshajulikana msimamo wake si kumuunga mkono EL, and this is very open to themselves! At the same time, EL anaapa it is either him or CCM dies! Hapa ndipo ninapoungana na wewe kwenye post yako juu kuwa kwayo EL, upinzani utaingia madarakani!!!
My opinion is, EL ni mgonjwa na kwa hali ile hawezi kabisa kugombea 2015, ninachoweza sema anaweza kuweka kijana wake muaminifu, possibly Dr. Nchimbi.
Henge,
Mtandao wa Lowasa serikalini ni kama vile umemalizika sasa baada mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, maRC na hivi karibuni maDC. Tatizo limebaki BUNGENI tu ambako wakati uchaguzi linavunjwa na kila mbunge kulilia nafsi yake zaidi baada ya hapo.
Kwenye CCM nako huu utaratibu mpya wa kuwapata wajumbe wa NEC toka ngazi ya wilaya nako kumeharibu sana mitandao sugu ya akina Lowasa. Wagombea wa NEC-CCM wametakiwa kikanuni wasiwe wanashikilia nafasi nyingine za kudumu kama UBUNGE.
Sekretarieti ya akina Mukama, Nape, January, Mwigulu,..., nayo haitabiriki na kuingilika kirahisi kama ile ya Mzee Makamba.Nguvu kubwa aloobaki nayo Lowasa na washirika wake ni PESA ambayo watapata taabu sana kuitumia kwa taratibu na kanuni za sasa ndani ya chaguzi za CCM zinazoendelea sasa.
PascoWanabodi,
Mtanzania, vinginevyo kama ni Lowassa ndie angekuwa rais, Tanzania isingekuwa hapa ilipo, na kusingalikuwepo hata hilo hitaji la ukombozi wa pili wa Mtanzania maana Tanzania ingeshakuwa peponi!.
Hivyo wale wote wenye kulitakia mema taifa hili, mshukuruni sana EL na JK, vingenevyo 2015, ingekuwa ni hadithi ile ile tulioizoea!.
Pasco.
Rais wangu 2015 ni Shamsi Vuai Nahodha kama tutalazimika kuendelea na CCM. Amekuwa WaziriKiongozi SMZ; akawa waziri wa Mambo ya Ndani na sasa ni Waziri wa Ulinzi na JKT. Atapata mtu kama Dr Asha Rose Migiro kumsaidia kama Makamu wa Rais au Waziri wa Mambo ya Nje
Hiyo ni haki yako na huo ni msimamo wako, nakubali.ipo siku watu wataelewa kuwa EL hausiki na richmond? sisi wachache ndio tunaojua fact za richmond, tunamlaumu sana EL kwa nini alijiuzuru. Wenye kumbukumbu siku EL alipojiuzuru Bungeni alihojiwa na Tido mhando wa TBC kwenye mazungumzo ambayo yalirekodiwa akiwa kwenye nyumba ya waziri mkuu ya Dodoma. yale mazungumzo yalikuwa yarushwe na TBC alhamisi usiku. Tido alitaka airushe kama ilivyo bila kuedit. wapambe wa JK walizipata taarifa very late kwamba EL anamwaga mboga, kipindi kilipotaka kwenda hewani tu yaani tido anamtambulisha EL, kikakatwa hapohapo. anayetaka kujua Ngoyayi aliongea nini amuulize Tido atamweleza vizuri, kwa kuwa Tido hayupo tena kifungoni(TBC) yupo huru (mwananchi).
Najua EL hawezi kuongea tena hii issue mpaka JK atakapomaliza uraisi wake, ila issue ya richmond itampa tabu sana katika harakati za uraisi. Haitoshi tu kusikia kuwa EL amemweleza JK kwenye vikao vya kamati kuu dodoma kwamba yeye JK ndio aliyekuwa anampa maelezo kuhusiana na Richmond, wananchi wanataka wamsikie yeye EL mwenyewe.
I WILL ALWAYS BE THE TRUTHFUL DISCIPLE OF NGOYAYI
Bro, hivi nikweli mwalimu alimkataa au chumvi imetiwa ktk hili, naomba nijulishwe huyu jamaa namkubali sana.kwa misimamo yake.Nimeipenda hii...ha ha ha, hata mimi the same, kimoja kinachonikumbusha huyu mtu ni kuwa Nyerere alimkataa
Kwa hiyo,EL akiwa Rais Tanzania itakuwa peponi?
Au motoni?
EL aliwahi kuwa no.2 hapa Tz na kweli tulionja utamu wa pepo yake!!! Alijiuzulu kwa tuhuma ipi vile?
Mkuu hapo kwenye red bold kuna siri kubwa sana. Na nina kuhakikishia wajuayo siri hii ni watu watatu tu, EL,JK na RA. Pasco aliwahi sema kwenye tundiko lake humu ndani kuwa and I quote "...kwa yeyote yule anayesema EL ni fisadi ataje ufisadi wake..." That time nakumbuka wengi tuiishia kusema "Richmond"
Hakika nakwambia haya hatuyajui ni usiku wa giza! Mwenye makshfa mengi Nishati na Madini si EL ni mwengine kabisa na RA na EL wanamjua! Sema kwa usalama na heshima plus weledi, linabaki kuwa "fumbo la imani" Kati ya mambo yanampa EL drive ya ku-fight mpaka kielewe, hili ni moja wapo, ili siku ile aje awahakikishie waTZ si yeye!!
Hakika mnyukano wa 2015 utakuwa mkali kuzidi maelezo!!
Huyu anatambulika hata kwa utendaji wake pindi akiwa waziri mkuu maana hata alipokuwa akitembelea halmashauri za wilaya wakurugenzi walikuwa hawalali kwa either kukemewa jukwaani au hata kusimamishwa asiendelee kusoma utekelezaji hewa( wa kubumba) ila kwa sasa hivi hakuna kiongozi hata huyo aliyepewa nafasi yake hana lolote tofauti na kufungua mawe ya msingi pamoja na kutoa maagizo yasiyotekelezwa na wasaidizi wake wa chini.
Mkuu hapo kwenye red bold kuna siri kubwa sana. Na nina kuhakikishia wajuayo siri hii ni watu watatu tu, EL,JK na RA. Pasco aliwahi sema kwenye tundiko lake humu ndani kuwa and I quote "...kwa yeyote yule anayesema EL ni fisadi ataje ufisadi wake..." That time nakumbuka wengi tuiishia kusema "Richmond"
Hakika nakwambia haya hatuyajui ni usiku wa giza! Mwenye makshfa mengi Nishati na Madini si EL ni mwengine kabisa na RA na EL wanamjua! Sema kwa usalama na heshima plus weledi, linabaki kuwa "fumbo la imani" Kati ya mambo yanampa EL drive ya ku-fight mpaka kielewe, hili ni moja wapo, ili siku ile aje awahakikishie waTZ si yeye!!
Hakika mnyukano wa 2015 utakuwa mkali kuzidi maelezo!!
Mimi si mshabiki sana wa siasa za tz ila ni mfuatiliaji mzuri ingawa sina mrengo wa chama chochote,ki ukweli mzee wetu EL kwa muda mfupi aliokuwa PM alithubutu kuwanyoosha watendaji wazembe,labda kila mmoja ajaribu ku-recall namna alivyowakimbiza wakuregenzi wazembe wa halmashauri,ni mtu wa KUTHUBUTU na akiamua kusimamia jambo anaweza,labda wadau mjaribu kufananisha uwezo wake wa maamuzi na aliyemtangulia kisha mtaelewa ninamaanisha nini,mzee EL hakuwa mtu wa ''kulia lia'' katika utendaji wake, all in all akiamua jambo he has that courage to push it forward!