Edward Lowassa anaitumia vizuri degree yake ya maigizo!

Edward Lowassa anaitumia vizuri degree yake ya maigizo!

Anakuchanganya wewe mwenye akili kama zako keshakatwa hana jipya tena.

Hata inayokufa haiachi kurusha miguu anamalizikia tu.
igp hivi vitu huwa mwamuzi mzuri ni muda, hizi zako ni kejeli za kawaida mno kwenye mambo kama haya ila niamini nikwambiacho ukimya wa EL ni sio volcano mfu
Post zote na habari zote za tangu uteuzi kwa asilimia 80 zinamhusu EL kwahiyo haihitaji akili toka kuzimu kujua EL ni mtu wa aina gani, kumbuka yeye sio nzi kuwa unaweza kumuua kwa gazeti au mbu kuwa utaweza kumwangamiza kwa dudukiller...!
 
Last edited by a moderator:
Hii sio kweli kuwa Lowassa and degree ya usanii (Theatre Arts), bali Lowassa ana degree ya Arts, yaani degree ya mambo ya jamii toka UDSM na Masters ya maendeleo ya jamii toka UK. Tukubaliane tu kuwa Lowassa hafai kwa sababu ya ulaji wake rushwa lakini tusiongezee na uongo unaofanya yote yanayoongelewa kukosa thamani.

Munatuchanganya!!! Kwa nini musiende kwenye personal website zake alizoandika yeye mwenyewe au marafiki zake zilizoko kwenye public domain mujiridhishe???

(1) http://www.elowassa.com/education.php?Active=Bio
(2) http://elowassa.com/admin_login.php
(3) http://www.karugendo.net/2013/01/maamuzi-magumu-ni-pamojana-kudhibiti.html
 
Ng'wamapalala you should know better. Unajua kabisa kwamba kitendo cha madiwani, wenyeviti wa vijiji etc huko Arusha kuhama CCM kwenda Chadema is a real consequence of the flawed CCM nomination processes that recently took place in Dodoma. Sasa unaposema haya ni maigizo una maana gani, wakati unajua kwamba hili tu la viongozi wa CCM kukikimbia chama chao kinawagarimu CCM kifedha na kisiasa big time. No wonder people call you "mpumbavu" kwenye hii thread yako.
 
Lowasa is the best loser ever,na political calculations and benefits haziruhusu yeye kutoka CCM
Mkuu,
Lowassa alipuuza strength za CCM badala yake akawa amejikita kwenye weakness za CCM.

While Mr Lowassa was busy building an institution within CCM, his party was monitoring all his actions.

While he was beaming with confidence given the level of support from within the party, little did he know that he was providing his detractors an ammunition for his downfall.

Ninasikia kwa sasa safari ya matumaini imebadilika na kuwa safari ya uhakika kwa kutumia barabara nyingine!
 
Hatushangai kwa sababu ccm na serikali yake ni kawaida kuigiza, igizo kubwa lililovunja record ni lile la jk kuwasamehe wezi wa epa
Mkuu,
Ndiyo maana nikasema, wenzake walikuwa wanafahamu kile alichokuwa anakifanya!

Wamefanya kile ambacho Rais Kagame alikisema, ''I will wait for you at the right place and I will hit you''.
 
Mkuu umeelezea vizuri sana...ni kweli kitengo kilishafanya Cost/Benefit analysis za kugeuza mtungi...tukaona benefits ni kubwa zaidi...tumefanya maamuzi sahihi... waacheni UKAWA wafanye maamuzi magumu ya kukinga hilo bakuli la panya na makapi...
Mkuu,
Lowassa atahama CCM kama anadhani CCM haichaguliki tena lakini kinyume cha hivyo, hawezi kuhama kwa sababu anafahamu CCM itaendelea kubeba madhambi yake kama akiendelea kuwepo ndani ya chama.

Baadhi ya wapambe wake wa karibu wameanza kumpa ushauri ili aendelee kubaki ndani ya CCM.
 
Ng'wamapalala

Kwasasa yanaweza kuonekana ni maigizo na blah blah nyingi nyingi tuu lakini trust me ndugu LOWASSA ni nextlevel na hii ngoma bado mbichi sana
Na kwakuwa ameamua kukaa kimya kiwewe ndio kinaongezeka ccm wanatamani aseme, kusema kunasaidia kujua nini kinaendelea.....jamaa yuko kimya, kimya kabisa na kumbuka kimya kingi kina mshindo mkuu....huu mshindo mkuu ndio homa ya ccm
Kadiri LOWASSA anavyozidi kukaa kimya ndio sintofahamu inavyozidi kutawala ndani ya ccm.....
Mkuu Mshana Jr

Ukimya wa Lowassa unawatisha wale ambao hawamfahamu au hawafahamu kile ambacho anakifanya/atakifanya baada ya jina lake kupitiwa na panga la Wazee wa CCM.

CCM wanafahamu kile ambacho Lowassa anataka kukifanya, na kwa maana hiyo, ngoma ya Lowassa haiwezi kuwatisha CCM kwa sababu wamejiandaa ili asiipige.

Kama Lowassa angekuwa ni next level, hata jina lake lisingekatwa.

Nguvu ya Lowassa ilikuwa inakuzwa kimaigizo na vyombo vya habari.
 
Munatuchanganya!!! Kwa nini musiende kwenye personal website zake alizoandika yeye mwenyewe au marafiki zake zilizoko kwenye public domain mujiridhishe???

(1) Edward Lowassa Official Online Office
(2) Edward Lowassa Official Online Office
(3) Karugendo Blog

Awe kaandika yeye au mwingine bado ni makosa kusema Lowassa ana digrii ya Theatre Arts. Kwanza, hadi anahitimu mwaka 1977, hapakuwa na digrii hiyo UDSM, ingawa somo lilikuwepo. Pili, hata sasa huwezi kuwa na digrii moja hiyo hiyo ikaitwa Theatre Arts na Bachelor of Arts with Education. Ukweli ni kuwa digrii yake ya kwanza ni B.A. with Ed, ambayo itakuwa na masomo mawili ya kufundishia, moja kubwa, lingine dogo. Lowassa ni mmoja wa walioendelea na somo muhimu la combination za Milambo High hadi Chuo, ambalo ni Kiswahili, lililokuwa kubwa. Pia alifanya vizuri ktk somo mtambuka la Dev Studies, ambalo alilichukulia digrii ya umahiri baadaye Bath, Uingereza. Kitaaluma, amebobea hasa ktk Elimu, Kiswah na Dev Studies
 
Hii sio kweli kuwa Lowassa and degree ya usanii (Theatre Arts), bali Lowassa ana degree ya Arts, yaani degree ya mambo ya jamii toka UDSM na Masters ya maendeleo ya jamii toka UK. Tukubaliane tu kuwa Lowassa hafai kwa sababu ya ulaji wake rushwa lakini tusiongezee na uongo unaofanya yote yanayoongelewa kukosa thamani.
Mkuu,
Pitia kwenye tovuti ya vijana wa Lowassa wanaojiita 4umovement ili apate historia yake.
Katika tovuti hiyo, imeandikwa ‘’Born in Monduli August 26, 1953,a leader and a patriot who has always put his country above everything else. Renowned for his ability and tendency of taking decisions in difficult situations,he goes by the name of Edward Ngoyai lowassa.

Lowassa did his secondary education at Ilboru Secondary School and concluded his high school studies at Milambo Secondary School in Tabora in 1973 he then received his degree in theatre arts at the university of Dar es salaam and later completed a masters degree in development studies in United kingdom’’.

Tembelea hapa,
 
Uchambuzi wako ni hafifu na wa upendeleo.

Hata mtu kama mimi nisiyeipenda CCM niliona kuwa utaratibu wenu wa kumpata mgombea Urais ulikuwa, at best, shambolic.
Hata kama mlikuwa mnataka kupitisha "watu wenu" at least mngefanya huku haki ionekane imetendeka ki-CCM CCM!

Kuhusu Lowassa, nadhani kumekuwa na manung'uniko toka kambi yake kuliko kwa wengine simply kwa sababu "aliwekeza" kuliko hao walionyamaza. Hivyo ni budi kuangalia hoja ya msingi badala ya kwanini Lowassa au vijembe na makala za kuganga kidonda kwa juu juu. In fact hao walionyamaza kimya il hali hawajaridhika ni wanafiki tu (another common mark of you).

Mchakato wenu wa kumpata mgombea Urais, kwangu mimi umeakisi na kuwakilisha 100% CCM ilivyo. Kama mnasigina, mnakiuka, mnavunja kanuni, sheria na taratibu mlizojeweka kwa hila na jeuri (ni desturi yenu iwe kwenye Serikali au Bungeni, Mahakamani nk) kwanini mpewe nafasi ya kuendelea kuharibu?

CCM hata mngempitisha huyo Lowassa bado ni CCM tu, mmeoza wote na hamfai kupewa tena dhamana ya kuongoza nchi, imetosha. Wananchi wanatakiwa kuikata CCM "jumla" kwenye sanduku la kura Oktoba.
Mkuu ni umetoa Ushauri mzuri watanzania kuikataa ccm hapo October, wasi wasi wangu ni mmoja tu nao ni hivi NEC imeshajitoa Kuwa taasisi ya ccm
 
Ieleweke Edward Lowassa ana degree in Theatre Arts from the University of Dar es Salaam.

Baada ya uigizaji wake kushtukiwa na Wazee wa CCM (Kitengo) ambao waliamua kulikata jina lake, kwa sasa ameanza maigizo mengine ili kuishinikiza CCM ikae naye kwenye meza moja ili kulinda maslahi yake na wapambe wake.

Tuliona maigizo ya kununua makundi ya vijana, viongozi wa dini na viongozi wa kisiasa wakimiminika nyumbani kwake eti kumuomba akachukue fomu za kugombea Urais. Wengine walifikia mpaka hatua ya kumuita Joshua wa Tanzania ambaye Mungu amemtuma kuwavusha Watanzania mpaka kwenye nchi ya ahadi.

Malengo ya haya maigizo ilikuwa ni kutaka kuishinikiza CCM isiliguse jina lake kwa sababu eti anakubalika ndani na nje ya chama.

Kwa sasa ameanza tena maigizo yale yale katika mtazamo mwingine huku akitumia makundi ya vijana, wanasiasa na viongozi wa CCM ili kuishinika CCM ikae naye meza moja ili kulinda maslahi yake na wapambe wake.

Alianza Mzee Kingunge kwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari katika malengo ya kuitisha CCM. Eti bila Lowassa kuwepo kwenye kampeni za CCM, ushindi haupo na kwa maana hiyo, CCM lazima ifanye maridhiano na Lowassa. Wenye fikra pevu wakajiuliza, kwani CCM iko kwenye mapambano na Lowassa?. Kama Lowassa anahisi yuko kwenye mapambano na CCM, basi ni jukumu la Lowassa kukubali yaishe na siyo jukumu la CCM.

Baada ya CCM kumpuuzia Mzee Kingunge, kwa sasa amekuja tena na igizo lingine la kutumia baadhi ya wanchi kama kafara wa kisiasa ambapo tumewaona baadhi ya vijana na madiwani wanajiunga na CHADEMA eti kwa sababu CCM imekata jina la Lowassa. Yaani wanataka kuonyesha CCM itakufa kama haitampigia magoti Lowassa na wapambe wake kwa sababu Lowassa ni mafuriko!

Lowassa na wapambe wake wanatengeneza mazingira ili kupata political bargaining power ndani na nje ya CCM.

CCM inayoongozwa na Mzee Kinana haitishiki kwa sababu imeishazifahamu mbinu na maigizo yote ya Lowassa na wapambe wake.

Kabla ya kulikata jina lake, CCM ilifanya homework kuhusu faida na hasara zake na ikajiridhia kulikata jina lake ni faida kuliko kulibakiza kwenye vikao vya chama. CCM wanafahamu hata faida na hasara ya yeye kuchukua kadi ya chama kingine.

Wakati Lowassa na wapambe wake wanapiga kelele na kusema hakatwi mtu, wenzake ndani ya CCM walikuwa wanafanya kazi ili kufahamu chanzo, sababu na nguvu ya kuweza kuishinikiza CCM katika maamuzi yake.

Hata haya maigizo ya sasa aliyoanza kuyaigiza yatagonga mwamba kama ilivyo kwa maigizo ya mwanzo.

una gubu wewe
 
Mkuu ni umetoa Ushauri mzuri watanzania kuikataa ccm hapo October, wasi wasi wangu ni mmoja tu nao ni hivi NEC imeshajitoa Kuwa taasisi ya ccm
Mkezwag, NEC haitabadilika mpaka pale (sisi wananchi kwa wingi na nguvu zetu) tutakapoamua ibadilike. Tukiamua Oktoba NEC haitatuzuia, ingawa ni ukweli NEC 100% bado ni tawi la CCM.
 
Kinana anastaafu au bado anaendelea kuwa katibu mkuu....???????kama atastaafu mikoba apewe Nape.
 
Back
Top Bottom