Edward Lowassa anaitumia vizuri degree yake ya maigizo!

Edward Lowassa anaitumia vizuri degree yake ya maigizo!

Habarini wanaccm
Nianze kwa kutanguliza samahani kwa nitakaowakwaza kwani ni bora nizungumze kuliko kukaa kimya nitakuwa mjinga wa ajabu na nitakuwa sijaitendea haki democracy,
Nasikitika kuona wanaccm hawapendi kuambiwa ukweli kisa wanalinda maslahi yao na hii in miongoni mwa mambo yanayofanya chama hiki kiende mrama maana ukisema ukweli baadhi yetu kulingana na Uwezo wa kufikiri basi huona wewe ni mpinzani kwa chama#
Ndg zangu Nchi yangu ni bora kuliko chama hvyo Mara nyingi naweka mbele maslahi ya Taifa kuliko chama,Leo hii tunapoona watu wanakihama chama chetu sio wajinga na sio suala la kuwabeza bali twatakiwa tujiulize kwann watu wanakihama,
Kumetokea mambo mengi sana ndani ya chama ambayo kimsingi yanasababisha wananchi wakichukie chama cha mapinduzi#
Maneno ya wananchi wanasema tatizo sio magufuli bali tatizo ni mfumo wa kulindana,kubebana na kushughulikiana ndani ya ccm ni miongoni mwa sababu zinazowakera wapiga kura.
Tujipange ila kiukweli mtaani hali ni mbaya.
Leo hii atatambulishwa rasmi James lembeli kwa wanakahama lakini pia kunatukio la madiwani wa Simiyu Na madiwani Na wachama wa ccm monduli kukihama chama cha mapinduzi,Huu sio mtikisiko mdogo in mkubwa sana hebu fikiria Hawa watu wanawatu wangapi nyuma na watakieneza nini kwa watu wao lakini pia baada ya kukaa tukatafakari kwa makini tukiohili sisi tumekalia kujipa ushindi wa whatsap na pale mtu anapoamua kufunguka kwa kusema kweli basi atachukuliwa kama unakipinga chama ila tuamini kuwa wananchi wa leo sio wale wa Mwl Nyerere ,Tanzania ya leo sio ile ya Mwl hii ya leo iko tofauti kabisa,Watanzania wanahitaji mabadiliko hivyo wasipoyapata ndani watayatafuta nje,
Watanzania wamechoshwa na umaskini uliokithiri,Wamechoshwa kuona keki ya Taifa wanafaidika nayo wachache,Wamechoshwa na kuhudumiwa chini ya miti,Wamechoshwa kuona rushwa imekithiri,Wamechoshwa na mishahara duni,mikopo hakuna vyuo vikuu,Elimu isiyoendana na hitaji la MTU, Tunahitaji Tanzania mpya yenye fursa sawa kwa wananchi wake .
Niwasihi vijana wezangu tusiwe daraja la wanasiasa tufanye maamuzi sahihi kwa kiongozi sahihi bila woga,Kura moja inathamani kubwa saana kwako mtanzania .
Tukiona nyeusi tuseme nyeusi na tukiona nyeupe tuseme nyeupe bila woga kwa miaka mitano au kumi ni mingi kwa kweli hivyo binafsi sitokuwa tayari kusema nyeusi kwenye nyeupe.
Tuweke maslahi ya taifa mbele.
Ahsanteni.
 
Tatizo letu watanzania ni kuongea kishabiki badala ya uhalisia!
Walio upande wa Lowassa na wasiomshabikia mtabishana kwa kauli za kubashiri!!!!
Kama kuna wakati utafika Lowassa afungue mdomo wake kuelezea mikakati yake tutasikia.
Hakuna sababu ya kuumba yasiyokuwepo!!!!
Tumekuwa Taifa la kusubiri matukio, skendo, kashfa, mipambano, mipasho!!!
 
Tusubiri yatokee ndipo tutapata majibu sahihi.who is who in local politics.
Mkuu,
Unasubiri yatokee mambo gani tena zaidi ya yaliyotokea Dodoma?

Kuna wananchi wengi tu waliaminishwa CCM haina ubavu wa kulikata/kuliondoa jina la Lowassa lakini kilichotokea tunakifahamu.

CCM wamefanya tathmini zao kabla ya kufikia uamuzi wa kulikata jina lake.

Haya mengine ni maigizo tu katika kuitumia fani yake.
 
Kudhihirisha kama Lowassa ni nguli wa maigizo, taarifa zimeanza kupatikana zikionyesha madiwani waliohama kwenda CHADEMA ni watatu tofauti na idadi ya madiwani 18.

Kama haya maigizo pia yatashindikana, kuna uwezekano hata wale walitangaza kuhama tukasikia wamerudi tena CCM.

Video inayoonyesha ufafanuzi kuhusu sakata la Madiwani wa Jimbo la Monduli waliodaiwa kuhamia CHADEMA.

 
Last edited by a moderator:
Uigizaji wa el,ccm na wananchi wamesha mjua,kumbe alikuwa anawanunua watu kupata umaarufu.inasikitisha hata kijana wa chuo kikuu eti anashabikia kwa kupewa elfu 10,Jamani.sigawe hizo kwa miaka mitano ijayo,ndipo utaona alichokupa leo mtu huyu.serikali inayoingizwa kwa rushwa ni katili sana kwa watu masikini.hamjui hilo
 
Back
Top Bottom