Ecuador: Wafungwa 68 wauawa katika mapigano ya magenge hasimu

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
603
1,760
Takriban wafungwa 68 wameuawa kwenye mapigano mapya katika gereza la Ecuador.

Ghasia katika gereza la Litoral katika mji wa Guayaquil inasemekana zilianza Ijumaa jioni.

Ripoti zinasema Polisi ambao wameingia kwenye majengo ya magereza wamekuta bunduki na vilipuzi.

Zaidi ya wafungwa 100 walikufa katika mapigano kati ya magenge hasimu mwezi Septemba, na takriban wafungwa 300 wamefariki kufikia sasa katika magereza ya nchi hiyo ndani ya mwaka huu.

Vurugu za Septemba zinazohusiana na genge zilikuwa mbaya zaidi katika historia ya Ecuador.

Wakati huo, wafungwa kutoka upande mmoja wa gereza walitambaa kupitia shimo ili kufika upande mwingine ambapo walishambulia genge pinzani. Mamia ya maafisa na askari wa jeshi walitumwa kurejesha udhibiti wa eneo hilo.

Mapema mwezi huu, Rais Guillermo Lasso alisisitiza kuwa serikali yake inarejesha udhibiti sio tu wa magereza bali pia maeneo ya Ecuador ambako walanguzi wa dawa za kulevya wamejidhihirisha.

Maafisa wanasema Magereza ya Ecuador kwa sasa yanachukua wafungwa wapatao 9,000 zaidi ya idadi stahiki. Gereza la Litoral liliundwa kwa ajili ya wafungwa 5,300 lakini kwa sasa lina wafungwa 8,500.

=========
_121547395_gettyimages-1236540650.jpg

At least 68 prisoners have been killed in new fighting at an Ecuadorean prison where more than a hundred inmates died in clashes between rival gangs in September, officials say.

The riot at the Litoral Penitentiary in the city of Guayaquil reportedly began on Friday evening.

Police tactical units who have entered prison buildings have found guns and explosives, reports say.

Nearly 300 inmates have died so far this year in the country's prisons.

September's gang-related violence was the worst in Ecuador's history.

At the time, inmates from one wing of the prison crawled through a hole to gain access to a different wing, where they attacked rival gang members. Hundreds of officers and army soldiers were deployed to regain control of the complex.

The deadly fight, which saw some inmates decapitated, drew attention to the growing influence in Ecuador of transnational crime gangs such as the Mexico-based Sinaloa and Jalisco New Generation cartels.

The latest fighting has also left 25 people injured and follows a smaller armed clash earlier this month in which three inmates were shot dead.

In a short statement posted to Twitter, President Guillermo Lasso offered his condolences "to the families who have lost loved ones" and said new measures were needed to "fight the mafias that profit from chaos".

Earlier this month in a BBC interview, Mr Lasso insisted that his government was regaining control not only of the prisons but also of areas of Ecuador where drug traffickers had gained a foothold.

He accused previous governments of being "passive" about drug trafficking but warned that rising drug use in the country would take "more than a decade" to tackle.

And he said Ecuador would need international support from neighbouring Colombia, the US and the EU to strengthen its armed forces and police to combat the growing influence of crime gangs.

Ecuador's prisons are currently accommodating about 9,000 more prisoners than they were designed to hold, officials say. The Litoral Penitentiary was designed for 5,300 inmates but currently holds 8,500.

Source: BBC
 
Jela za South America na Latin America hua ndani ya jela unakuta kuna makundi ndio yanatawala,

Mara nyingi ni magenge ya uuzaji wa dawa za kulevya,uhasimu wao huanzia nje ya jela ambapo mara nyingi hua wanauana ili kucontroll eneo husika kwa ajili ya biashara ya Drugs,ndani ya jela magenge hujuana kwa alama zao za tattoo.
 
hapa duniani kuna watu wakiambiwa kua kuna na pepo na mto wanakua na shaka na hilo ila kama umeshawahi kukaa hata katika hizi lock up za kawaida utapata taswira ya motoni acha gerezani ...
 
Jela za South America na Latin America hua ndani ya jela unakuta kuna makundi ndio yanatawala,

Mara nyingi ni magenge ya uuzaji wa dawa za kulevya,uhasimu wao huanzia nje ya jela ambapo mara nyingi hua wanauana ili kucontroll eneo husika kwa ajili ya biashara ya Drugs,ndani ya jela magenge hujuana kwa alama zao za tattoo.
Huenda hata hayo magereza hutumika kama maeneo ya kuendesha Biashara haramu ya mihadarati.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom