Ebay

Ebay

Wana jf naombeni kuuliza, niliagiza mzigo flani kutoka ebay na kesho natarajia nikafanye payment, kuna mtaaram anaye jua makato ya TRA, afu mzigo ukishafika na dhl unapigiwa cm kwa ajili ya malipo ya tra au, naomba msaada cpo shwali kwenye hayo mambo, pls

Kama ulichagua na kulipia kusafirisha mzigo kwa DHL, aliyekuuzia anakutumia tracking number ambayo itakuwezesha kufuatilia na kujua mahali mzigo wako ulipofika na nini kinafanyika juu ya huo mzigo. Ukishapata tracking number unaenda website ya DHL unaingiza tracking number sehemu ya ku-track mzigo halafu unabonyeza track. Taarifa zote zinazohusiana na mzigo zitaonekana , muda, mahali ulipo na nini unafanyiwa. Kwa DHL, mzigo wowote ambao ni Non-document, lazima upitie taratibu za ushuru wa forodha mara tu unapoingia Bongo(DHL Head Office-Dar), ambako wataangalia kama unastahili kulipiwa kodi au la. Kama unastahili,DHL Agents watakupigia simu kuomba TIN (Tax-payer Identification Number) yako ili watu wa customs waitumie kufanya clearance.Gharama zote za kodi zinalipwa na agent wa DHL kwa niaba yako, na wakati wa kupokea mzigo ukishafika mjini kwako, unajulishwa na kwenda kulipa hizo gharama na zingine za DHL ndipo unachukua mzigo na kusaini.

Kiwango cha kodi kinatgeana na mzigo wenyewe na declared value, japokuwa watu wa customs kwa sasa wana-search kwenye internet kuangalia wastani wa thamani ya mzigo iwapo watahisi declared value ni ndogo. Kuna baadhi ya bidhaa hazilipiwi ushuru km PC na accessory inazoambatana nazo etc.
NB: Kabla hajatuma mzigo, muuzaji ataomba namba zako za simu kama haziko kwenye anuani yako.
Haya maelezo ni kwa mujibu wa ufahamu wangu.
 
Nshukuru saana wana jf, hatimae mzigo umeingia, ebay wanaship huku tz bt inategemea na huyo muuzaji kk
 
kiongozi, umesema pc haulipii ushuru ukimaanisha pc ya computer au?? naomba kuelezwa hapo mkuu
 
Mzigo wako umechukua siku ngapgpg?
Kama umeupokea vipi kuhusiana na kodi?

kiongozi, mzigo wangu umetumia cku kumi kunifikia, na kuhusu kodi DHL wamenilipi mm ndo nikawalipa DHL ( importing duties 13% na tax 25%)
 
mkalenda, naomba unisaidie jinsi ya kupata tax duties na VAT kwenye bei ya mzigo wangu. Hivi ukiagiza simu au laptop utalipia kodi?
 
Last edited by a moderator:
mkalenda, naomba unisaidie jinsi ya kupata tax duties na VAT kwenye bei ya mzigo wangu. Hivi ukiagiza simu au laptop utalipia kodi?

kama nilivyo andika hapo juu mkuu, unapiga asilimia ya mzigo wako wote, unachua 13+25=38% so kama mzigo wako ni wa sh. million moja unatakiwa kulipa asilimia 38 za hiyo million moja kama tax na importing duties, kitu kama laptop cjui kama wanalipia kodi ndo maana nikamuuliza mdau hapo juu alivyo sema pc haulipii kodi cjui anamaanisha pc ya computer au?
 
Back
Top Bottom