East African Federation (EAF) public Views

Tanzania bado haijafikia kiwango cha kufaidika na muungano huo wa nchi za Afrika Mashariki kwa kuwa kuna wasomi wachache ukilinganisha na Kenya na Uganda. Pia, maendeleo ya viwanda ni madogo na hivyo kuna uwezekano wa kuwa soko la Kenya wakati wao Tanzania wakiwa na nafasi ndogo sana ya kuuza bidhaa Kenya.

Pia migogoro ya nchi za Kenya na Uganda itaweza kuhamia Tanzania, endapo kutakuwa na muingiliano.

Nashauri tusubiri kwanza

Nkwangu
 
Lakini wananchi wa mpakani wanasemaje?

Maombi ya kujiunga EAC Watanzania wawakataa Wanyarwanda,Warundi

*Waliohojiwa wahofia ukabila, silaha haramu
*Wengine wasema historia za nchi ni tofauti

Na Prosper Kwigize, Kibondo

WATUMISHI wa idara mbalimbali za Serikali na watu binafsi wilayani hapa wamepinga moja kwa moja nchi za Burundi na Rwanda kuingizwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wakizungumza juzi na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Diodorus Kamala, aliyefanya ziara katika mikoa ya Kigoma, Kagera, Mara na Mwanza hivi karibuni, waliitahadharisha Serikali ya Tanzania dhidi ya jitihada za nchi hizo.

Baadhi ya sababu zilizotolewa na wananchi hao ni pamoja na nchi hizo kutokuwa na mikakati endelevu ya kudumisha amani, kuwa na ubaguzi wa kikabila na kuzagaa kwa silaha haramu mikononi mwa raia wa nchi hizo.

Aidha, wengine walielezea kuwa kutawaliwa na makoloni tofauti kunaifanya Tanzania kuwa tofauti sana kiitikadi na kiuendeshaji na Serikali za nchi za Afrika ya Kati, kitu ambacho kimedaiwa kuwa ni sababu tosha ya kutoungana nao.

Akitoa hoja ya kupokea mapendekezo hayo, Dkt. Kamala alieleza kuwa yeye na wizara yake wanaendesha mpango wa kuitangaza wizara na kupata maoni ya wananchi kuhusu Burundi na Rwanda kukubaliwa au kukataliwa kujiunga na Jumuiya.

Alileza kuwa Serikali inatarajia kuunda Tume ya kuratibu maoni ya Watanzania, ili kupata mtazamo wa walio wengi juu ya uamuzi mkubwa kama huo na kuepusha utata.

Hadi juzi asilimia 49.3 ya Watanzania waliotoa maoni yao kupitia mtandao wa tovuti ya www.habaritanzania.com, uliofunguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita walikuwa wakipinga nchi hizo kukubaliwa.

Aidha asilimia 50 ya kura 141 zilizopigwa na wasomaji wa mtandao huo walikubali nchi hizo kuingizwa katika Jumuiya wakati asilimia mbili wakipiga kura ya kutaka kwanza zifikiriwe.
 
Katika pepesa pepesa yangu nimekuta hii leo asubuhi..sasa mbona mbona watu hawakuulizwa kama kuna mtu anataka kurudi kwenye EAC in the first place?

anyway links ndio hizi...


Piga Kura kujiunga kwa Burundi na Rwanda EAC.

Piga Kura yako kuhusu kujiunga kwa Burundi na Rwanda Katika Jumuiya ya Africa Mashariki

http://www.habarita nzania.com/ articles/ 1227/1/ - Click hapa
Tuma Maoni yako kuhusu kujiunga kwa Burundi na Rwanda Katika Jumuiya ya Africa Mashariki

Chagua nchi uliyopo

Uganda
Tanzania
Kenya

Tuma SMS kuhusu kujiunga kwa Burundi na Rwanda katika Jumuiya ya Africa Mashariki

+255 786 171 757
(SMS ONLY)



Regards,
HabariTanzania. com Management
Visit our website at http://www.habarita nzania.com
Email: info@habaritanzania .com
 
Kama binadamu, kuungana ni jambo jema, kama wanasiasa suala la kuungana linahitaji utambuzi utokanao na muungano, lakini pia kama mataifa huru muungano ni lazima usimame katika msingi madhubuti wa kisheria.
Sasa mimi kama mtanzania najiuliza, je hawa jamaa wamekwishatuakikishia kwamba hawatakuwa na tabia ya ubaguzi tutakapokuwa wamoja? je tutawaamini vipi kama si wabaguzi na wakabila tena, Je kujiunga kwao nasi kutawabadilishaje tabia zao za kujiona bora kuliko wengine?

Mimi binafsi ningedhani muda bado wa wao kujiunga nasi. Ni juu yao kutuomba sis(kenya,Tanzania na Uganda) turatibu mienendo yao kwa muda maalum na kisha tuwaeleze kama wanaweza kujiunga au wafanye lipi litakalokuwa halijafanyika kwa wakati huo.

Hivyo, enyi viongozi wetu msituletee watu ambao bado wanadamu za wenzao mikononi mwao. KAMA HATUNA UAKIKA BORA KUSUBIRI
 
Hizi naunga mkono ziingie katika umoja huu, hasa utasaidia eneo letu la EA kuwa na nguvu kiuchumi. Ila napendekeza nchi hizi zipewe muda kidogo kabla ya kukubaliwa rasmi ziweze kuweka mambo yao ya ndani sawa, kama miaka 10 hivi.

Asante
 
Laizer M said:
I think we should allow them to join EAC because of the following reasons:
- This could be a good chance of advising them to stop their fighting.
- It may ease the reconciliation going on.


i dont believe in that .these people will bring trouble in our countries. they must have peace first before joining us.
 
Emanuel Mwampashe said:
Kila kitu kina faida na hasara zake, tukiangalia kwa undani, Rwanda na Burundi wakijiunga nasi wataleta hasara gani? ukabila wao?, sidhani maana wao ni sehemu ndogo sana ya jumuia, hivyo si rahisi kupenyeza dhana ya ukabila maana sisi hatukuizoea. Faida ni nyingi wakijiunga nasi, pamoja na masuala ya biashara tutakuwa tunawasaidia wajifunze kutoka kwetu kuwa ukabila ni dhambi kubwa. tuwakaribishe ili waone sisi tunawezaje kuishi pamoja bila kugombana ilhali tu mamia ya makabila.

Waruhusiwe ili waanze kuongelea maswala yao kama wanyarwanda na warundi, na si kama wahutu na watutsi.

Emma


Safi sana Emma!!....tuache ubaguzi!!
 
Museveni atoboa siri yake moyoni

*Atangaza kuutaka urais Afrika Mashariki
*Akataa kulinganisha Tanzania na Uganda
*Adai si jambo baya kukaa zaidi madarakani
*Asema mbona Nyerere aliongoza miaka 24!

KAMPALA, Uganda

RAIS Yoweri Museveni wa Uganda hatimaye ametoboa siri ambayo ameihifadhi moyoni mwake kwa miaka mingi, ya kutaka kuwa Rais wa Kwanza wa Shirikisho la Afrika Mashariki linalotarajiwa kuanza kufanya kazi kuanzia mwaka 2010.

Kiongozi huyo wa Uganda aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka takriban 20 sasa, amesema hana sababu yoyote ya kuiga mfano wa kisiasa wa Tanzania, unaozingatia haja ya kikatiba ya kupokezana uongozi kwa sababu nchi hizo mbili zimejengwa katika misingi miwili tofauti ya kihistoria.

Akizungumza katika mahojiano na redio moja ya Uganda, Museveni aliyeitawala Uganda kuanzia mwaka 1986, alisema anao uhakika kwamba iwapo shirikisho hilo litaanza wakati akiwa madarakani, anayo nafasi kubwa ya kuwa rais wake wa kwanza kutokana na ukweli kwamba atakuwa kiongozi aliyekaa madarakani kuliko yeyote mwingine katika ukanda huu wa mashariki mwa Afrika.

Akirejea siasa za ndani za Uganda, alisema akiwa ni kiongozi anayelitakia mema taifa lake lililokua katika misingi ya uhasama kwa miaka mingi, anao wajibu wa kuijengea nchi yake misingi imara ya kiuongozi kwanza, kabla ya kuamua kuondoka.

Museveni alisema: "Kuendelea kukaa madarakani si jambo baya. Kwa kweli ni sehemu ya misingi ya mabadiliko kwa sababu serikali zilizopita zilianguka kila baada ya miaka mitano."

Akijibu swali la mmoja wa wasikilizaji aliyetaka kujua lini atastaafu, Museveni alisema kwamba ataisaliti Afrika iwapo atajiuzulu kabla ya mtoto wake, Shirikisho la Afrika Mashariki halijazaliwa.

Aliwataka watu waache kufananisha siasa za Uganda na za Tanzania katika masuala ya uongozi wa kisiasa akisema, mataifa hayo mawili yana historia tofauti za siasa.

"Ni kweli Tanzania ni mfano mzuri, lakini wao (umma) wanatakiwa waonyeshe sura yao halisi. Wanatakiwa wakumbuke kwamba (rais wa zamani) Julius Nyerere aliiongoza nchi kwa miaka 24 na kuiacha akiwa amepandikiza misingi mizuri ya siasa na maadili," aliongeza kwamba, ugonjwa wa Uganda utaponywa kwa kutumia njia yake yenyewe.

Pia alisema kwamba muda utafika atakabidhi madaraka, na kuongeza kwamba iwapo atajiuzulu kabla ya kuijenga Jumuiya ya Afrika Mashariki, ataisaliti Afrika nzima.

Kamati inayohusika na uundaji wa Shirikisho la Afrika Mashariki imependekeza Januari 2010 kuwa wakati wa uzinduzi wa shirikisho hilo.

Kipindi kati ya miaka 2010 - 2012 ni kipindi ambacho kinahesabiwa mchakato wa kupokezana urais utaanza kati ya nchi tatu. Kati ya Januari na Machi 2013, uchaguzi wa Rais na Bunge la Shirikisho utafanyika.

Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete, leo anazindua mchakato wa kupata maoni ya wananchi kuhusu uharakishwaji wa Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki.

Uzinduzi huo utafanyika katika viwanja wa Mnazi mmoja, Dar es Salaam kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 5:00.

Uzinduzi huo utakwenda sambamba katika nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Kenya na Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Katibu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, S. Mollel, rais pia atazindua kamati ya kitaifa itakayokusanya maoni ya wananchi katika mikoa na wilaya zote za Tanzania Bara na Visiwani.

Kwa mujibu wa Mollel, wanakamati walioteuliwa na Rais Kikwete ambao watafanya kazi hiyo kuwa muda wa miezi sita ni Profesa Samwel Wangwe ambaye ni Mwenyekiti na Ali Ameir Mohamed atakuwa Makamu Mwenyekiti.

Wajumbe wa kamati hiiyo ni Nestory Ngulla, Hazara Pindi Chana, Ibrahim Kaduma, Christine Kilindu, Joseph Butiku, Amina Shaaban, Mariam Shaba na Mariamu Juma Mabodi.

Wajumbe wengine ni Ali Mzee Ali, Elvis Musiba, Hamisi Sued Kagasheki, Khalifa Suleiman Khalifa, Kabwe Zuberi Zitto na Omar Bendera ambaye ameteuliwa kuwa katibu wa kamati huyo ambaye atakuwa na wasaidizi wawili; mmoja kutoka Tanzania Bara na mwingine Visiwani.
 
Ninafikiri ni jambo muhimu sana kwa Burundi na Rwanda kwa kujiunga na EAC, kwa mambo yafuatayo:

1. Kujiunga kwao kutawasaidia kuacha mambo ya vita kwa kuangalio wanachama wenzao wanavyoishi.

2. Kwa kuacha kwao vita kutawapa nafasi ya kuangalia/kuchangia maendeleo ya nchi zao zaidi.

3.Ni jambo la muhimu sana kwa kila mtu kuwa huru katika nchi yake, na sio kuwa mkimbizi katitka nchi nyingine.

Ninashukuru kwa kupata mafasi hii, ya kuchangia mawazo yangu kwakweli ni jambo zuri sana.
 
Ni jambo la busara kukaribisha nchi nyingine katika shilikisho la nchi za Afrika mashaliki hususani majilani zetu wa Rwanda na Burundi.

Tukumbuke ule msemo usemao umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu.Jumuia hiyo inaweza kusaidia kiuchumi, kisiasa na kijamii
 
kwa upande wangu suala la rwanda,burundi kujiunga na jumuia ya east africa ni suala muwafaka kwa nchi wanachama kwani mgogoro wa nchi zote mbili hizo kwa kiasi kikubwa ulichangiwa na nchi wanachama wa east africa any how wakitaka wasitake na ni wajibu wao kutafuta kila njia iwezekanavyo ili kufuta makosa yao ikiwemo kuwapa nafasi na kushiri katika jumuia africa mashariki thank you
 
Geographical-Rwanda na Burundi ni sehemu ya East Africa, Lakini kuna tofauti kubwa ya Kisiasa kati ya hizo nchi na Nchi nyingine za east africa kama Tanzania, Kenya na Uganda.Hazipaswi kuingia kwenye Jumuia ya Africa Mashariki mpaka hapo zitakapokomaa kisiasa zaidi.Tusisahau ni Nchi ambazo zimetoka Vitani mda si mrefu na hazina serikali za uhakika mfano mzuri Burundi.
Viongozi wa Burundi kila kukicha wapo Dar es salaam kutafuta amani nchini kwao.Je watawezaje kuwa makini na jumuia ya Africa Mashariki.

Pili tujiulize Tanzania, Kenya na Uganda zimefanikiwa vipi tangu ianzishwe tena Jumuia ya Africa Mashariki, Je wananchi wamenufaika nayo? na Je imeweza kutatua matatizo yake yanayowakabili wanachama wake( Tanzania, kenya na Uganda. Nguvu za Jumuia hii zinapaswa kwanza zielekezwe Uganda hili kumaliza Mgogoro wa serikali ya Uganda na LRA.Na suala la wakimbizi wa Burundi na Rwanda wanaohishi Tanzania. Na matatizo ya forodha yanayoikabiri nchi zote tatu(Tanzania, Kenya na Uganda).

Tutakapomaliza hayo matatizo yetu ya msingi ndio tuangalie jinsi ya kuziingiza Rwanda na Burundi. na sharti la kwanza zinaitaji serikali za uhakika:
 
muungano ulikuwepo kabla kwa juhudi za makusudi kabisa majirani zetu wa kenya wakuvunja muungano wetu,walishiriki kuvunja muungano bado wako hai watupe maelezo yao wazi kwani watanzania ndio tuliyumba na kunyanyasika zaidi kutokana na hali mbaya ya kiuchumi serikari ilishindwa kulipa mafao ya baba zetu waliokua wafanyakazi wa jumiya hiyo

Watanzanio waliotembelea kenya wamenyanyaswa sana na vyombo vya dola vya kenya,vipi leo jira zetu wanamiminika kwetu na kuja na kasi ya muungano hii nikutokana na mabadiliko ya maisha na kuona watanzania tunaishi kwa matumaini ya maisha bora ya kizazi kijacho baada ya kuvumilia miezi 18 ya dhiki na dhiaka,kabla ya kuungana na majirani zetu hawa serikari itie mkazo kwa nchi za kusini mwa afrika ambako damu yetu imemwagika katika vita vya ukombozi

Baada ya ukombozi wao watanzania tulobaatika kwenda nchi za kusi tumepokelewa kwa heshima na taadhima na wananchi wa kusini ili mradi uvunji sheria za nchi zao,hawa ndio ndugu zetu wa kweli awa wengine awaamiki,M7 ameshatamka bayana wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita uganda anata kua rais wa kwanza wajumiya hiyo inaonyesha jumuiya haitodumu kwa udikteta.

Baba wa taifa alisononeka sana kuvunjika kwa jumiya alitumia ushawishi wake kuiimarisha ikashindikana,ninaimani kizazi kijacho kitakuja kupiga nia ukombozi wa taifa la tanzania kama ilivokua bosnia na muungano wa urusi hii nikutokana na hulka za majirani zetu hawa,tatizo la ukabila na ubinafsi katika nchi zao lmekithiri wamalize matatizo hayo kwanza ndio tuwafikirie,KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI ZIDUMU FIKRA ZA BABA WATAIFA MWALIMU NYERERE,wantanzania tanaunga mkona sera za pan african lakini atutaki kuanzia east africa tunataka muungano na nchi za kusini kwanza.

MR M.KAUNGU
email;africanebony2003@excite.com
 
i think its a good idea to stablelize economy and securiry for the country involved, say jerry from chicago,
 
i am completely against these 2 countries to be invited to join East a africa.How can a country as tiny as rwanda and bururndi never have an understanding among themselves being part and parcel of the East-Africa?They will spread their hatred to us and we are not ready for us.It is of importance for them to show the world love and joined other countries.What is wrong with Africa countries we have enough problems to invite more.Have u got a chance to look into Africa map these countries are very tiny but huge problem .

They have ego and cruelty so why insteady of helping them to be one ,u want to bring them in the lands of harmony,and about uganda also i dont understand them ,they have also something going on because some of ugandas are rwandese then there is congo ,rwandese want to control congo so what's up with allthse mercy and mind u rwanda is a landlocked countries that's why it is craving for land everywhere and not in a nice way they just want to own the land so let tuts and hutu solve their issue then u can invite em.as far as my research i hear tusti came from Ethiopia and hutu are chads so go and figure out these are two ethinic that came to rwanda for whatever reason and now they both want to claim a tiny landlocked country as of one ethinic!?

I hope my points will have a voice into the decision.
 
Rwanda and Burundi should not have been countries on their own in the first place. This was poison planted by the Europeans; if these countries remained as part of Tanganyika all these killings would not have taken place. Putting two territorial boundaries around two tiny tribes and mixing them up unproportionately around these boundaries is one of the biggest "mistakes" that the Europeans made in Africa. It just wouldn't work.

Now these people need the help of their fellow Africans and accepting them in EAC would go along way towards solving their tribal rivalry. The only problem lies with EAC itself and the dream that it could become a federation. With the mentality of Kenyans as we witness it - Hiyo sahau.
 
There are two things that we must consider before accepting Rwanda and Burundi in the EAC. Do we want to help them or we want to help ourselves? If we want to help them, then EAC will be the solution as once they will enter the EAC, their tribal identities that was created by the Europeans will weaken as they will identify themselves as Rwandans or Rundis, this will lead to national unity in their country...however, this is not a one day thing....we need half a century for it to happen!!!

Another thing is that by leaving them outside the EAC, we will be planting the seeds of our own destruction as they will obviously be against us and no body knows what they are capable of doing!



Jizaledo said:
Rwanda and Burundi should not have been countries on their own in the first place. This was poison planted by the Europeans; if these countries remained as part of Tanganyika all these killings would not have taken place. Putting two territorial boundaries around two tiny tribes and mixing them up unproportionately around these boundaries is one of the biggest "mistakes" that the Europeans made in Africa. It just wouldn't work.

Now these people need the help of their fellow Africans and accepting them in EAC would go along way towards solving their tribal rivalry. The only problem lies with EAC itself and the dream that it could become a federation. With the mentality of Kenyans as we witness it - Hiyo sahau.
 
Sasa haya ndiyo mmbo ya maana kuchangia, siyo mambo ya udini, ukabila ... mtu anayechangia mambo kama hayo ananyesha alivyofilisika ...
______________________
Hivi tujiulize sana kuna sababu gani kwetu sisi watanzania kuingia kwenye muungano huu?

Labda:
- Wananchi wetu watapata kazi huko kenya na uganda?
- Viwanda vyetu vitapata soko la bidhaa zake huko kwa wenzetu?
- Tutakuwa na uwezo wa kupata ardhi ya kulima huko kwa wenzetu?
- Je, tutakosa nini kwa kutokujiunga?
- Je, tutapata nini kwa kujiunga?
- Kwani sasa hivi tunakosa nini?

Katika kujibu maswali hayo, ni wajibu wa kila mtanzania kutafakari kwa undani (not superficially), akiangalia historia ya nchi hizi tatu.
Nitachangia kidogo, wengine mtanisaidia:
EAC iliyovunjika iliweka malengo kadhaa ya ushirikiano, moja kuu likiwa ni kuwepo kwa usawa kwa nchi zote katika faida itokanayo na umoja huo, kwa mfano mgawwanyo wa viwanda. Kwa mfano iliamuliwa kwamba viwanda vya matairi ya magari viwe Tanzania tu. Tukajenga kiwanda cha General Tyre. Kabla wino wa mkataba huo haujakauka, Kenya iliamua kujenga kiwanda cha matairi cha Firestone.​

Kumbe wenzetu walitaka sisi tuwe soko lao.
Je dhamira hiyo ya wenzetu sasa imekwisha? Au nia yao bado ni hiyo, sisi tuwe soko lao?

Kumbe wanataka kututawala hawa. Watawale uchumi wetu toka Nairobi!! Watanzania gundueni hilo haraka ...

Wakati sisi tunapigania ukombozi wa Afrika, ikiwa ni pamoja na Afrika Mashariki (Uganda) wakenya walikuwa wanafanya biashara na kutengeneza utajiri. Baada ya kupatikana kwa amani, limekuwa ni soko zuri kwa mitaji ya wakenya.
Ni muhimu kwa wakenya kuchangia kwa njia moja au nyingine kwenye gharama za kuwepo kwa amani katika eneo hili. Gharama ambayo ilikuwa ni ya watannzania pekee.

Tuanzie hapo kwanza ...

Nasema Shirikisho Hapana, Hapana, Hapana kwa sasa.

Wakaenya wanasema tanzania inahitaji miaka 20 kuwafikia kiuchumi. Namimi nasema tunahitaji miaka 25 kabla hatujafikiria kuwa na federation!#

tutaendelea ...
 
Hakuna federation hapa. Watu wanashabikia madaraka (Museveni) na kuilalia Tanzania (Wakenya). Sisi mbinu zetu ni zipi? Au ndio hivyo tutakwenda kichwakichwa tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom