Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,569
- 34,698
Mwandishi mmoja kwa jina la Warigi amekuwa anatumiwa na serikali ya Kenya kuandika habari mbaya za Tanzania...kuna waandishi wa habari wa Kenya who make a living and have specialized kuandika mambo mabaya dhidi ya Tanzania.
..The East African magazine limezoeleka kwa kuandika mambo mabaya-mabaya dhidi yetu huku nchi nyingine wanachama wa EAC zikiandikwa vizuri.
..hebu soma hapa uone aliyeanzisha habari za Tanzania kuwa isolated ni waandishi wa habari wa Kenya:
EAC states pull in different directions as Dar is isolated - News - www.theeastafrican.co.ke
..hapa pia unaweza kuona kwamba badala ya kusisitiza ushirikiano baina ya mataifa yetu, waandishi wa Kenya wamekuwa wakiandika habari ambazo zinaashiria kwamba kuna ushindani na upinzani na wakati mwingine uadui baina ya mataifa yetu.
Watch out Kenya,Tanzania is catching up | Zitto na Demokrasia
cc Nguruvi3, Masonjo
Kila anapotoa makala huo ndio umekuwa msimamo wa Kenya.
Nakumbuka hadi ubalozi uliingia kati na JK alipokwenda Nairobi aliongelea hilo.
Warigi amekuwa anaandika katika gazeti la the economist, baada ya kujulikana siku hizi economist haiandiki jina lake bali columnist.
Huyu Warigi kwa ushirikiano na Kagame, walianzisha timbwili la kuondoa EAC kutoka Arusha kwenda Nairobi.
Ni mwandishi huyo huyo kaandika kuhusu suala la Ardhi akisema ''Tanzania is dithering''
Kila linapotokea jambo la EAC Warigi amekuwa msemaji wa serikali ya Kenya si kama ofisa bali msimamo wake ndio unakuwa wa serikali. Ushahidi upo.
Waandishi wa Kenya hawaandiki mambo mazuri ya Tanzania hata siku moja.
Juzi Membe alikwenda kukutana na Kenyatta kumweleza jitihada zilizofanywa hadi kufutiwa kesi. Hakuna anayeandika hilo.
Kenya walipoleta MoU ya utalii hakuna mwandishi aliyeandika hilo.
Kenya wakija kuomba msaada wa chakula hakuna anayeandika hilo.
Wao ni kuhusu ubaya wa Tanzania tena kwa kutengeneza.
Waandishi ambao kidogo wamekuwa impartial ni wa Uganda.
Kuna gazeti la the monitor liliandika vema sana kuhusu kwanini Tanzania inachukua tahadhari.
Ilionyesha makosa ikaonyesha na hoja. Na gazeti likaweka wazi kuwa kwa mwendo wa kuitenga Tanzania, ni hatari kwa mustakabli wa eneo zima.
Gazeti liliandika kuhusu umuhimu wa nchi zote bila kupendelea na kuongeza kuwa kinachofanywa sasa hivi ni kuua EAC kwa njia ya CoW
Ukisoma Rwanda Times, hilo ndilo uchafu kabisa. Hawana jingine bali kuiandamana Tanzania.
Wasichokijua ni kuwa katika ukanda huu, Tanzania ni muhimu sana.
EAC ilishangilia baada ya hotuba ya JK kwamba Tanzania haitajitoa.
Hii maana yake ni kuwa wananchi walikuwa na wasi wasi kuhusu mstakabali wa EAC
Katibu mkuu alipokuwa Mkenya, Mganda, Mtanzania kila kitu kilikuwa kwa mujibu wa mkataba.
Baada ya Ssezibera kuingia, yeye kaamua kufanya kazi kwa maagizo ya Kagame.
Kagame hajawahi kuwa katika jumuiya yoyote zaidi ya hii na CoW.
Hajui matatizo ya 1967-1977 na wala hajui matatizo ya muungano kama inavyojua Tanzania.
Kuendesha jumuiya kwa mawazo kutoka Kigali ni jambo la hatari sana.
Watanzania walikataa hawa jamaa wasiingie kwasababu walijua Kagame ni tatizo la ukanda huu.
Leo imekuwa proved walikuwa right, jumuiya inakufa kwa maagizo ya Kagame.
Kagame ndiye tatizo, kwa jinsi anavyowaswaga Wanyarwanda left right, anadhani anaweza kuswaga EAC