East Africa Fibre Optic Cable: Connectivity, issues & progress

We do appreciate for the technological advancement and its arrival in our region, but the only problem with us is timely and prompt maintenance of what we have.
 
Tanesco ina benefit namna gani na hii? Wao si users to kama sisi!!

Mtoto,

wanaposema wana-benefit wanamaanisha simply kua they are
using the new fibre optic connection. Ni kama tu vile weye unapotumia
mtandao na kuona maswala yanakwenda faster basi you also are
benefiting in that context.

Shukran.
 
Meanwhile mlioko Bongo, hii kitu mnaionaje maana kuna washkaji kule
Kenya wanalalamika kua mtandao umekua more slow than earlier times.
Je ukweli uko wapi?
 
Kitu imesha ingia bongo tayari tunasubili kuanza kwa implementation yake kwa watanzania...
 
Mtoto,

wanaposema wana-benefit wanamaanisha simply kua they are
using the new fibre optic connection. Ni kama tu vile weye unapotumia
mtandao na kuona maswala yanakwenda faster basi you also are
benefiting in that context.

Shukran.

Okay.... I though the term benefit within this context lingekuwa limebeba maana zaidi kwa sababu ya hizo institution walizozitaja hapo. TTCL would 'benefit' kwa sababu wao kwa sasa ni mmoja wa internet providers nchini. So hii fibre itakuwa fresh katika biashara yao ya uuzaji wa MB. Institutions kama universities, well their use is obvious - knowledge sharing. Na railway company pia utumiaji wao unaweza kueleweka kutokana na area yao ya practice - package tracking, etc. Lakini sioni sababu ya kuweka Tanesco kwenye hilo kundi. Sioni kama wao wana special use ya hiyo internet zaidi ya mtanzania wa kawaida. Hili ndilo lililonifanya niulize hilo swali. Inaelekea muandishi hakutathmini vizuri alichoandika au utumiaje wake wa maneno.
 
Changamoto kubwa ninayoiona mimi ni kuwa mtandao huu utaishia kua siasa tu. Mpaka leo hii kuna mlolongo mrefu sana wa mambo yanayokwamisha wadau kutandaza fiber jijini na kwingineko nchini. Tunashukuru fiber ipo silver sand leo, lakini, ni lini tutapata huduma hizi majumbani na maofisini mwetu?
Wajameni, hivi hakuna wawekezaji wa kupitisha pay TV kwenye hiyo fiber? Tumechoka na foreni na huduma mbovu za DSTV. Kwa mtoa huduma kama DSTV walitakiwa wawe na "engineers/technicians on call" 24x7, leo hii ukipata tatizo saa nne usiku, shauri yako!!
 
Last edited by a moderator:
Kitu imesha ingia bongo tayari tunasubili kuanza kwa implementation yake kwa watanzania...

Naona implementation yake itachukua hata mwaka maana rais asipo wapush itachukua hata miaka 3 si unajua kibongo bongo kamati zikae.
 
Swali je, gharama zitafikishwa kwa watumaiji wa mwisho wa mtandao wa internet au zitashuka kwa ISP (Internet service providers) na wataendelea kuwanyonya watumiaji na wateja kwa nguvu zote ili kujifaidisha wao wenyewe?? Maswali yapo mengi, lakini kwa sasa naweza kusema mi yangu macho.... Kila la kheri kwa Afirika na tuendelee kuchapa kazi ili kuleta mabadiliko katika bara letu hili heshimika.
 
Kwa TZ, unaweza usikute gharama zisishuke kabisa. Na wataanza toa sababu kwa nini gharama hazishuki. Hakuna wasimamizi TZ, wakiwepo wanapewa hongo (10%) nao kwisha.
 
Naamini gharama zitashuka tu, maana kuna competition kubwa kwenye mitandao ya simu. Tena kuna mtu Tigo amenitonya kuwa wanakuja na Internet karibuni!!
 
Kwa TZ, unaweza usikute gharama zisishuke kabisa. Na wataanza toa sababu kwa nini gharama hazishuki. Hakuna wasimamizi TZ, wakiwepo wanapewa hongo (10%) nao kwisha.

hilo nalo neno.Jana nilimsikia prezda akisema"siku ya leo kwangu ni ya faraha sana,kwani hii ni atua moja wapo ya kimaendeleo,tatizo la kuambiwa server iko slow itakuwa ni historia.sasa hivi yahoo inafunguka mara moja."

Nilicheka sana,kwani sio watu wote ambao wataweza kupata huduma hiyo,na mpaka fibre isambae nchi nzima itachukua muda sana.lingine ni swala la Gharama kuendelea kuwepo juu kwani sioni jitiada zozote zinazo fanywa na tcra kuakikisha watumiaji wa hizi huduma wanapata huduma sahihi na kwa bei ya alali na sio wizi wizi wao ambao tumeuzoea siku zote.
 
Meanwhile mlioko Bongo, hii kitu mnaionaje maana kuna washkaji kule
Kenya wanalalamika kua mtandao umekua more slow than earlier times.
Je ukweli uko wapi?

Bongo bado hatujapata fursa ya kutumia hiyo huduma labda wapo wachache!
 
Hatimaye Mkonga wa Chini ya Bahari wa SEACOM Uko LIVE.

Sasa ni nini kinafuata? Unaweza kupata huduma kwa sasa kupitia Local ISP ambazo tayari zimeshajiunga.

Tusahau Siasa zote tulizosikia juu ya bei nk. Je, Bei halisi zikoje?

- ISP lazima zinunue SEACOM Minimum ya 1 pair of Fiber ambayo ina Capacity ya 155 Mbps (Full Duplex). SEACOM wanauza 1 Mbps Full Duplex (1024 Kbps) kwa USD 750.00 Kwa Mwezi Full Duplex au $ 375 Kwa Half Duplex ambayo SEACOM Hawauzi. Originally bei ya 1 Mbps full duplex kupitia VSAT (Best Price Wholesale from Satellite Operators) ilikuwa ni USD 5120.

- Kwa hiyo ISP inahitaji kununua SEACOM 155 Mbps kwa USD 116,250.00. Mkataba wa chini ni Mwaka Moja. So, total amount ni USD 1,395,000/=, Bila ya shaka hiki ni kiasi kikubwa sana kuwekeza kwa mara moja. Hii ni mbali ya gharama za Inland Fiber utakayotumia kuunganisha SEACOM Hub Station na Network Operating Centre (NOC) yako pamoja na Equipment zingine.

- So, what next?

- ISP nyingi sasa zina woga wa kujua watafanya vipi biashara kwa kuwa mara moja mapato yao yatapungua sana kutokana na bei kushuka sana kwa kama asilimia 60%. Pili kuuza capacity yote ya 155 Mbps kwa mwaka si kazi rahisi sana.

- Biggest ISP kwa sasa kwa miaka yote at best inaweza kuwa imeuza si zidi ya 100 Mbps.

- Sasa je ISP ziwauzie wateja kiasi gani?

- Na wafanye nini ili wasiingie katika loss na waendelee kutoa huduma na kuwalipa wafanyakazi wao vizuri?

- Je wataweza kuuza volume kubwa na kwa wateja wengi ili warudishe gharama zao na faida?

Kwa uzoefu na maoni yangu, huenda bei ikawa kama ifuatavyo:

- Kwa wateja Wakubwa yaani ISP na makampuni ambayo hayawezi kununua 155 Mbps lakini wanaweza kununua zaidi ya 50 Mbps bei kwa 1 Mbps huenda ikawa $ 850 kwa mwezi. Je wao watauza Retail kwa kiasi gani?

- Kama Watanunua pungufu ya 50 Mbps bei kwa 1 Mbps huenda itakuwa $ 950. Je wao watuza retail kwa kiasi gani?

- Bei hizo ni mbali ya mteja kuunganishwa kutoa NOC kwenda kwa huyo Mteja mkubwa. Say Installation itakuwa $ 5000 kwa Cable ya Fibre na Backup Link yake. Maintenance itakuwa $ 1000 kwa mwezi. Je bei za rejareja zitakuwaje?

- Bei za Rejareja bila ya shaka zinaweza kufanana na hizi hapa chni baada ya kuzingatia Investment pamoja na mambo yote niliyoyataja hapo juu (Bandwidth zote ni full Duplex):

- 128 Kbps - $ 230 Per Month - Bei ya sasa $ 640 Per Month (Best Price)
- 256 Kbps - $ 460 PM - Bei ya sasa $ 1280 pm
- 512 kbps - $ 920 pm - bei ya sasa $ 2560 pm
- 1024 kbps (1 Mbps) - $ 1840 - bei ya sasa $ 5120

- Bei hizo ni mbali na Equipment na Installation ambazo gharama zake zinaweza kuwa kati ya $ 1000 hadi $ 3000.

Hii ina maana bei halisi ya Bandwidth kwa ulinganifu wa Full Duplex itapungua kwa karibu asilimia 60%. Lakini je ISP zitakubali kushusha bei au kuwaongezea wateja wao Bandwidth ili mapato yao yasianguke?
 
Mkuu ahsante kwa uchambuzi wako mzuri.Ukweli ni kwamba sidhani kama ISP wetu wako tayari kushusha gharama au kutuongezea Bandwidth,kama kupunguza bei wanaweza kupunguza kwa 10% ambayo kwa mtizamo wangu naona ni ndogo na bado bei zitakuwa ziko juu.
 
Bei lazima zitashuka msiwe na hofu! Hakuna monopoly kwenye makampuni ya simu/internet kuna ushindani mkali sana.

Zaidi ya hapo kushuka kwa bei kutawaongezea wateja so watatengeneza faida nyingi zaidi, sioni situation ambayo itasababisha bei kutoshuka.
 
Bei lazima zitashuka msiwe na hofu! Hakuna monopoly kwenye makampuni ya simu/internet kuna ushindani mkali sana.

Zaidi ya hapo kushuka kwa bei kutawaongezea wateja so watatengeneza faida nyingi zaidi, sioni situation ambayo itasababisha bei kutoshuka.

sawa mkuu tuendelee kusubiri tuone kama itakawa hivyo.Kama watashusha itasaidia sana kuwaongezea wateja.Mimi hofu yangu ni kwamba Je ISP wetu wanauwezo wakununu hiyo 155 mbps? kama wapo ni wachache sana.
 
Mkuu ahsante kwa uchambuzi wako mzuri.Ukweli ni kwamba sidhani kama ISP wetu wako tayari kushusha gharama au kutuongezea Bandwidth,kama kupunguza bei wanaweza kupunguza kwa 10% ambayo kwa mtizamo wangu naona ni ndogo na bado bei zitakuwa ziko juu.

Asante Mkuu Carth;

Kuhusu kushuka bei nina uhakika bei zitashuka hata kwa asilimia 60% kama nilivyosema. Kwa maoni yangu, kama kuna mteja kwa mfano alikuwa ananunua bandwidth ya 256 Kbps na analipa $ 1280, si rahisi apewe bei mpya ya $ 460 kwani hiyo itawapunguzia mapato ISP. Badala yake henda wakaongeza Bandwidth ili mteja aendelee kulipa pesa ile ile kwa hiyo anaweza akaongezwa Bandwidth ikawa 768 Kbps.

Hata hivyo kwa watumiaji wengi wa Internet, experience itabadilika sana kwa sababu ya fast speed na hivyo watajikuta mahitaji ya Bandwidth yakiongezeka mfano kudownload documents kubwa kubwa ambazo sasa hivi wengi hawawezi kirahisi kwa sababu ya Speed ndogo na capacity ndogo. Wengi pia sasa watapatana nafasi ya kudownload images, movies n.k.
 
Zaidi ya hapo kushuka kwa bei kutawaongezea wateja so watatengeneza faida nyingi zaidi, sioni situation ambayo itasababisha bei kutoshuka.

Mkuu Kang;

Hapo kuna challenge kidogo ingawa with time mambo yatabadilika. Unajua kwa sasa Fiber iko DSM. Lets us assume hata ikienda mikoani mwaka huu, lakini mpaka ISP zijipange kusambaza huko itachukua say miezi 6 hadi 12. Sasa DSM wateja watakuwa wa kugombania.

Kama ulikuwa una ISP A yenye mapato ya USD 2 Million kwa Mwaka, itabidi wateja wake waongezeke kwa asilimia 60% ili apate mapato yale yale vinginevyo labda awalazimishe wateja wake wakubali kuongeza BW kuliko kupunguziwa bei kitu ambacho kitategemea mteja na mteja na bajeti zao.

Kwa hiyo bei lazima zishuke, lakini pia usishangae kama utaona ISP nyingi sana ndogo ndogo zitakufa kwa shida ya kupata soko kwani ISP kubwa itabidi wafanye kazi ya ziada kuongeza volume ya wateja na kubuni products nyingine ili ku-maintain mapato yao.
 
Back
Top Bottom