EAC yazindua meli ya utafiti Ziwa Victoria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

EAC yazindua meli ya utafiti Ziwa Victoria

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jun 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ( EAC) Balozi Juma Mwapachu  JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC), imezindua meli ya RV Jumuiya, itakayofanya kazi ya utafiti katika Ziwa Victoria.

  Uzinduzi huo ulifanywa jana na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Balozi Juma Mwapachu, ambaye alisema meli hiyo itafanya kazi ya utafiti utakaosaidia uchoraji wa ramani ya njia za meli.

  Kwa mujibu wa Balozi Mwapachu, RV Jumuiya inamilikiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki na ni msaada uliotolewa na Serikali ya Uingereza.

  Alisema huko nyuma, meli hiyo ilikuwa inafanya kazi katika Ziwa Nyasa kabla ya kuletwa Mwanza, ili kusaidia shughuli za utafiti katika Ziwa Victoria.

  "Meli hii itazisaidia nchi wanachama katika utafiti wa mazalia ya samaki, uandaaji wa njia za majini katika Ziwa Victoria na utafiti wa madini katika baadhi ya visIwa vilivyoko ziwani ,” alisema Balozi Mwapachu.

  Aliwataka watu binafsi na taasisi za serikali katika nchi wanachama, kuitumia Rv Jumuiya katika shughuli zao za utafiti kwa kuikodi.

  Alisema meli hiyo ni ya kisasa na kwamba ina vifaa bora kwa shughuli za utafiti.

  Kwa upande wake, Mhandisi wa Usalama wa Meli katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Gershon Fumbuka, alisema meli hiyo imetengenezwa kwa mfumo wa aina yake na kwamba ina uwezo mkubwa wa kustahimili dhoruba majini.

  "Rv Jumuiya, imefungwa vifaa vya kisasa ikiwa ni pamoja na rada,vifaa vya kukagua uchafu wa maji katika ziwa, vifaa vya hali ya hewa vinavyotoa taarifa kwa wavuvi na vyombo vya usafiri ndani ya ziwa," alisema Fumbuka.
  Chanzo EAC yazindua meli ya utafiti Ziwa Victoria
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ni manufaa gani yalipatikana kwa uwepo wake ziwa nyasa? Tunaomba tuambiwe. Si kutupa misifa ya meli tuuuuuuuuuuuuuuuu kumbe hamna kitu.
  Unasikia we Mwapachu?
   
 3. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tungoje Utafiti wa (EAC) na itabidi Tumuulize Mzeee Mwapachu mwisho wa huo utafiti utakuwa lini? Tunangoja jibu kwa Mzee Mwapachu
   
Loading...