fikirikwanza
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 7,452
- 3,065
Ukiwa mwanza na gari ukipaki tu hata dakika 2, 5, 7, au 15 yaani unanunua vocha, unasubiria mtu ambaye say umeenda kumpokea na ukafika yuko tayari kitendo cha kubakia mzigo na ndugu yako, au umefika dukani kuuliza kitu na ukaambiwa hakipo, ujue tayari unadaiwa 1500TZS eti parking fee ya siku nzima hata kama umetumia dakika 5 tu hapo mjini.
Zamani ilikuwa unapaki kwa saa TZS 300 tu, kipimo cha chini kilikuwa saa yaani dakika 60, japo kisayansi kipimo cha muda SI unit ni SEKUNDE. watu walilalamika japo walilipat tu hiyo mia 3, leo pomoja na kukua kwa teknolojia TARURA ama kwa makusudi kumuhujumu JPM ama kwa uwezo mdogo wa akili wamekuja na kichinjio cha iwe dakika 1, 2, 5, 15 au 20 utalipishwa 1500TZ kama umepaki siku nzima ambayo haraka haraka tusema ni masaa ya kazi 12.
hali hii ni tata na ya ajabu sana, huduma zinashuka kiwango na bei inapanda kwa kasi, inashuka kiwango kwa maana ipi? maana ni kwamba kulipa sio tena njia fupi ni shule kamili ya namna ya kulipa uanze kwa kutafuta invoice namba GOeP kasha ulipe, mara kadhaa ukiuliza deni lako pia unaambiwa huna kama siku mbili hivi ya tatu ndio unakuta deni limeingia, huenda umekwishasahau kabisa kama ulipaki mjini kwa dakika 2 au 5. huduma mbovu kabisaaa, yaani kulipia ni mbinde japo tunalipia wizi wa mchana tena wakati huu wa serikali ya wanyonge. why charge 1500TZS siku nzima mtu katumia dakika 15?
eti wanapunguza msongamani wa magari mjini, wanaongeza mapato. ongeza mapato kwa kupata pesa halali, yaani mtu alipe kadiri anavyotumia sio dunia ya flat rate hii.
Unapunguza msongamano kwa kumzuia mtu kutumia gari lake ambalo kaliingiza na kulipa kodi? kalipia kodi ya 40TZS kwa kila lilta ya mafuta, kalipia bima na kafanya service na kununua vipuri huku akilipa VAT 18%.? kwa nini msizuia magari kuingia nchini? kama lengo ni magari yamezidi idadi? kwa nini msiruhusu magari mapya pekee kuja nchini ili wachache wamudu gharama hivyo wale waliomudu gharama watumie mali zao kwa raha? kuliko kumuruhusu mtu aingize gari mpatae kodi aweke mafuta anunue vipuri halafu mzuie kuingia nalo mitaani tena kijanja janja.?
Kwa ufupi sana ni kama mnamhujumu jpm na kuleta chuki za kisiasa dhidhi yake. na ama ni mmeshindwa kufikiria kwa kasi ya jpm, tarura mwanza ni vema mkajitathmini na kupisha watu wenye uwezo kumsaidia rais wakafanya kazi hiyo.
1500TZ kwa kila ukiingia mjini ni sawa na kusema mwenye gari sasa hapa TZ analipishwa kila siku 1500x365=(tozo ya mwaka) ikiwa juu ya kodi zingine zote za vipuri mafuta na bima.
HAIWEZEKANI KABISA