E- Parking Mwanza ni hujuma kwa Magufuli au uelewa mdogo wa wasaidizi wake?

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,443
2,000
Ukiwa mwanza na gari ukipaki tu hata dakika 2, 5, 7, au 15 yaani unanunua vocha, unasubiria mtu ambaye say umeenda kumpokea na ukafika yuko tayari kitendo cha kubakia mzigo na ndugu yako, au umefika dukani kuuliza kitu na ukaambiwa hakipo, ujue tayari unadaiwa 1500TZS eti parking fee ya siku nzima hata kama umetumia dakika 5 tu hapo mjini.

Zamani ilikuwa unapaki kwa saa TZS 300 tu, kipimo cha chini kilikuwa saa yaani dakika 60, japo kisayansi kipimo cha muda SI unit ni SEKUNDE. watu walilalamika japo walilipat tu hiyo mia 3, leo pomoja na kukua kwa teknolojia TARURA ama kwa makusudi kumuhujumu JPM ama kwa uwezo mdogo wa akili wamekuja na kichinjio cha iwe dakika 1, 2, 5, 15 au 20 utalipishwa 1500TZ kama umepaki siku nzima ambayo haraka haraka tusema ni masaa ya kazi 12.

hali hii ni tata na ya ajabu sana, huduma zinashuka kiwango na bei inapanda kwa kasi, inashuka kiwango kwa maana ipi? maana ni kwamba kulipa sio tena njia fupi ni shule kamili ya namna ya kulipa uanze kwa kutafuta invoice namba GOeP kasha ulipe, mara kadhaa ukiuliza deni lako pia unaambiwa huna kama siku mbili hivi ya tatu ndio unakuta deni limeingia, huenda umekwishasahau kabisa kama ulipaki mjini kwa dakika 2 au 5. huduma mbovu kabisaaa, yaani kulipia ni mbinde japo tunalipia wizi wa mchana tena wakati huu wa serikali ya wanyonge. why charge 1500TZS siku nzima mtu katumia dakika 15?

eti wanapunguza msongamani wa magari mjini, wanaongeza mapato. ongeza mapato kwa kupata pesa halali, yaani mtu alipe kadiri anavyotumia sio dunia ya flat rate hii.

Unapunguza msongamano kwa kumzuia mtu kutumia gari lake ambalo kaliingiza na kulipa kodi? kalipia kodi ya 40TZS kwa kila lilta ya mafuta, kalipia bima na kafanya service na kununua vipuri huku akilipa VAT 18%.? kwa nini msizuia magari kuingia nchini? kama lengo ni magari yamezidi idadi? kwa nini msiruhusu magari mapya pekee kuja nchini ili wachache wamudu gharama hivyo wale waliomudu gharama watumie mali zao kwa raha? kuliko kumuruhusu mtu aingize gari mpatae kodi aweke mafuta anunue vipuri halafu mzuie kuingia nalo mitaani tena kijanja janja.?

Kwa ufupi sana ni kama mnamhujumu jpm na kuleta chuki za kisiasa dhidhi yake. na ama ni mmeshindwa kufikiria kwa kasi ya jpm, tarura mwanza ni vema mkajitathmini na kupisha watu wenye uwezo kumsaidia rais wakafanya kazi hiyo.

1500TZ kwa kila ukiingia mjini ni sawa na kusema mwenye gari sasa hapa TZ analipishwa kila siku 1500x365=(tozo ya mwaka) ikiwa juu ya kodi zingine zote za vipuri mafuta na bima.

HAIWEZEKANI KABISA
 
vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
3,637
2,000
TARURA Mwanza hii Huduma yao ya e-Parking itaondoka na kichwa cha mtu kwani hata hapa tunataka tuende ofisi zao za hapo Cappripoint wanieleze kwanini tulipark kwenye jengo la mtu (Eca Cliff ) halafu wao wametuletea invoice....hii huduma ni ya kipumbavu kabisa kwa nchi maskini kama Tanzania.
 
pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
3,730
2,000
Hata hivyo nyie wa Mwanza mna unafuu Mkubwa kuliko huku dar.
Parking zetu huku ni tsh 500/= Kwa kila saa 1 inamaana kutoka asubuh Hadi jioni ni tsh 6000/=

Huu wizi wa parking unatutesa Sana kuliko mikoani ifike wakati serikali iangalie hili
 
fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,443
2,000
Mwanza kuna tatizo moja wasukuma hawajui kulalamika hata pale wanapofanyiwa mambo ya kijinga na ajabu ni nduhu tabu.

How come on earth gharama itoke say 300 for average users of city parking areas maana wengi wanaenda kununua vitu na kusepa iwe 1500, mara 5 zaidi why?

YAANI kwa uchumi huuu mtu anakuja na dili dirisha la kukamua raia na wananchi zaidi na zaid why? JE MWANZA kuna city built parking areas? au hizo za roadsides ambazo tumeshazilipia ndio tunatozwa nazo mara mbili mbili kwa mara 5 zaidi?

road sides zipo kwenye michoroya barabara maana gari inafahamika hupakiwa, ndio maana wajenzi wa barabara wanaziweka na tulikwisha zilipia Enzi za road lisence ama sasa 40TZS kwa lita ya mafuta.

CHARGING PEOPLE TWICE OR MULTIPLE TIMES ni wizi tu, na ndio maana hatuendelei kwa kuibia raia

TARURA Mwanza hii Huduma yao ya e-Parking itaondoka na kichwa cha mtu kwani hata hapa tunataka tuende ofisi zao za hapo Cappripoint wanieleze kwanini tulipark kwenye jengo la mtu (Eca Cliff ) halafu wao wametuletea invoice....hii huduma ni ya kipumbavu kabisa kwa nchi maskini kama Tanzania.
 
fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,443
2,000
TARURA-Serikali ya WANYONGE INAYOKANDAMIZA NA KUPANGA MIPANGO YA KUIBIA WANYONGE?

Hio ni afadhali saana mbaya kabisa kwa wale wapiga cheni
Yaani ukipaki hata haujashuka ndani ya gari tairi ishapigwa cheni unaambiwa ulipe fain elf50
Kama huna unasema nao kikubwa unawakatia 20 au 30 wanakufungulia♂
 
pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
3,730
2,000
Hio ni afadhali saana mbaya kabisa kwa wale wapiga cheni
Yaani ukipaki hata haujashuka ndani ya gari tairi ishapigwa cheni unaambiwa ulipe fain elf50
Kama huna unasema nao kikubwa unawakatia 20 au 30 wanakufungulia♂
Mitaa ya Kariakoo kuna watu wanaitwa risasi kidole yaani wao kazi Yao kuzungukia mitaa wakiona gari imepaki ovyo kazi Yao ni kupiga simu Kwa jamaa wa TARURA na tena wanakuja na pikipiki zao wanakuja kufunga Matairi

Na watakupiga mikwara mpaka utoe tsh 30000 ndipo wanajiachia na Yule risasi kidole anapewa buku 5 maisha yanaendelea
 
fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,443
2,000
mimi naongelea watumiaji wengi ambao ni kupaki na kupakia ndani ya 30minutes, sasa wewe kama unahamishia gari mjini siku nzima may be unaduka na ni kila siku wewe uko hapo lazima ulipie japo pia 6000 kwa siku ni wzi mtu mkuu.

Mtu anaenda kununua dawa mseto 1500, parking fee 1500TZS hahahahaha, JPM anawaona hawa?

Hata hivyo nyie wa Mwanza mna unafuu Mkubwa kuliko huku dar.
Parking zetu huku ni tsh 500/= Kwa kila saa 1 inamaana kutoka asubuh Hadi jioni ni tsh 6000/=

Huu wizi wa parking unatutesa Sana kuliko mikoani ifike wakati serikali iangalie hili
 
fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,443
2,000
Tulisema tunatako tuondokane na wezi matapeli na madalali mjini kumbe TARURA ndio wanatuhujumu? jutakuta mtu mzima kazi yake ni kusubiria kuita tarura wakufunge cheni apate 5000/- je huku ndio kila mtu afanye kazi? tutaendelea kwa misheni town kila kona hata kupitia ofisi za serikali kama TARURA?

Mitaa ya Kariakoo kuna watu wanaitwa risasi kidole yaani wao kazi Yao kuzungukia mitaa wakiona gari imepaki ovyo kazi Yao ni kupiga simu Kwa jamaa wa TARURA na tena wanakuja na pikipiki zao wanakuja kufunga Matairi

Na watakupiga mikwara mpaka utoe tsh 30000 ndipo wanajiachia na Yule risasi kidole anapewa buku 5 maisha yanaendelea
ema
 
Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
8,254
2,000
Hii nchi tumekuwa wajinga mno. Kwa nini tumekuwa watu wa ndiyo kwa kila jambo? Mambo ya kipuuzi kama haya ni kuyagomea kwa nguvu.

Serikali inatakiwa kutenda jinsi wananchi wanavyotaka na siyo jwa serikali kupanga mambo ya hovyo ya kuwatesa wananchi.

Kwa serikali hii, kama kuna anayefikiria kuwa ina huruma na wananchi wake, anajidanganya sana. Hii ni serikali ambayo inawatesa wananchi wake, matajiri kwa maskini, kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea tangu uhuru wetu.
 
fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,443
2,000
Wameshusha parking fee kwa matajiri wenye maduka na biashara mjini wanaopark magari yao siku nzima kutoka say 300x9hrs=2700 kwenda 1500 kwa siku, ili hali wakimnyonya mpita njia mnyonge anaye paki kwa dakika 15, 30 hivi ananunu kitu anasepa zake. Wengine wanapaki masikini kununua dawa tu

Serikali ya wanyonge upside down

Hii nchi tumekuwa wajinga mno. Kwa nini tumekuwa watu wa ndiyo kwa kila jambo? Mambo ya kipuuzi kama haya ni kuyagomea kwa nguvu.

Serikali inatakiwa kutenda jinsi wananchi wanavyotaka na siyo jwa serikali kupanga mambo ya hovyo ya kuwatesa wananchi.

Kwa serikali hii, kama kuna anayefikiria kuwa ina huruma na wananchi wake, anajidanganya sana. Hii ni serikali ambayo inawatesa wananchi wake, matajiri kwa maskini, kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea tangu uhuru wetu.
 
fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,443
2,000
Kiburi si uungwana, TARURA MWANZA have to rethink tena faster, hiii ya kumuchonganisha JPM na wapiga kura kijinga jinga hivi sio kabisa. Parking fee itoke 300 ambayo ndiyo ya watumiaji wengi 75% iende 1500 how and why?
 
SIPIYU30

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
1,224
2,000
Hahahahah yaani itokee watu wote waache magari home for a month tuone kama watakamua ng'ombe asilishwa majani
Mkuu mimi nimepaki la kwangu, nasikilizia tu watu wanavyolia lia. Huwa nawasha pale ninapoona kuna ulazima kweli kweli, na muda muafaka ambao kero zinakuwa zimepungua. Haiwezekani sehemu naenda naweka mafuta ya 10k alafu unajikuta umebebeshwa costs za kijinga zingine kama 20k. Hiyo ni kuchota maji kwa gunia
 
fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,443
2,000
maamuzi magumu ndio hayo

Mkuu mimi nimepaki la kwangu, nasikilizia tu watu wanavyolia lia. Huwa nawasha pale ninapoona kuna ulazima kweli kweli, na muda muafaka ambao kero zinakuwa zimepungua. Haiwezekani sehemu naenda naweka mafuta ya 10k alafu unajikuta umebebeshwa costs za kijinga zingine kama 20k. Hiyo ni kuchota maji kwa gunia
 
kichinjio

Member
Jul 11, 2013
60
95
Naandika nikiwa na hasira moyoni. Uanzishwaji wa System mpya ya utozaji ushuru wa maegesho wa magari jijini Mwanza ni janga kwa taifa na sijui kwa hakika ni nani anafaidika kwa ukandamizaji huu.

Kwanza nianze na gharama za ushuru wa parking ambao ni shilingi 1500/= Ushuru ambao ni mkubwa sana na sijui waliangalia vigezo gani kutoza ushuru wa kiasi hiki na hapa haijalishi umepaki kwa mda gani.Iwe ni dk 15 , 30 au hata saa utalipia siku nzima.

Pili ni utozwaji wa fain iwapo umejisahau kwa namna yoyote ile kulipa. Hapa ndipo unapojiuliza ni nani haswa yupo nyuma ya jambo hili . Faini inayopigwa ni shs 20,000/iwapo hukulipa kwa Siku. Kiasi hiki ni kikubwa sana na kinaumiza . system yenyewe haikupi menu ya kuangalia bills yako kwa Siku then kesho tu ghafla unakutana na shs 20,000/= na haijulikan hiyo ishirini imefikiwa vipi? Yaan kutolipa hiyo 1500/= kiasi ambacho si sawa unapigwa faini ya shs 20,000/= faini ambayo haingalii muda na hupewi muda wa kulipa kama ilivyo kwa taasisi nyingine kama polisi na wengine.

Ombi.
Namuomba muheshimiwa Rais aingilie kati jambo hiki ambalo hatujui haswa linamfaidisha nani.

Ushuru ni mkubwa kwa Siku na ulipwe kulingana na muda wa maegesho kama ilivyokuwa hapo awali. System ni mbovu na iboreshwe kumuwezesha anayepaki kuangalia bill yake kwa siku baada ya muda wa magesho ili aweze kulipa. Faini inayopigwa ni kubwa sana na ipunguzwe na kupewa muda wa ulipwaji wake.

Mwisho
Nashauri system hii mpya mbovu na kandamizi ya utozwaji ushuru wa maegesho wa magari jijini Mwanza iondolewe na utozwaji wa ushuru wa magesho wa magari ufanyike kama ilivyokuwa hapo awali.
 
Top Bottom