E- Parking Mwanza ni hujuma kwa Magufuli au uelewa mdogo wa wasaidizi wake?

Parking fees wakati barabara zenyewe zimejaa vumbi na mashimo, au hayo makusanyo ni kwa ajili ya kugharamia maisha ya kifahari ya mwanamfalme asiyetumia gari za kuhongwa
 
Lipeni tu Mkuu ili Serikali ikusanye Kodi yake ,wakati Wakazi wa Dar es Salaam tulipo pandishiwa Ushuru kufikia Sh 500/= kwa Saa moja ,mlitubeza na hamkutusikia sasa wacha na nyie msomeshwe Namba..Hakikisheni mnachukua na Risiti za EFD..

CCM HOYEEEEEE..., na 2020 msisahau kuichagua tena
 
Nashauri system hii mpya mbovu na kandamizi ya utozwaji ushuru wa maegesho wa magari jijini Mwanza iondolewe na utozwaji wa ushuru wa magesho wa magari ufanyike kama ilivyokuwa hapo awali.
Kwani hapo awali ilikuwa vipi!
 
Lipeni tu Mkuu ili Serikali ikusanye Kodi yake ,wakati Wakazi wa Dar es Salaam tulipo pandishiwa Ushuru kufikia Sh 500/= kwa Saa moja ,mlitubeza na hamkutusikia sasa wacha na nyie msomeshwe Namba..Hakikisheni mnachukua na Risiti za EFD..

CCM HOYEEEEEE..., na 2020 msisahau kuichagua tena
Dar Es Salaam sh. 500/= ni kwa saa na Mwanza sh. 1,500/= ni kwa siku alafu jamaa kelele nyiiiiingi!
 
TARURA mwanza ni wapuuzi sana,mwanzoni walikuwa wanakhpuga fine tzs 40,000 kama hujalipia ndani ya saa 24. kuna wadada wenye nyodo wanatembea kwenye mitaa na kupiga picha magari na kurusha TARURA. Ukiwaomba maelezo wanakuijibu vibaya, mmoja jana alingia anga zangu maeneo ya Mwanza Hotel mkabala na ofisi za ATC alinijibu " nenda TURURA ukajieleze huko huko utaelimishwa" mimi nikachukuwa simu yangu nikawapiga picha. Ana bahati nimesafiri. Mfyooo!
Ukiwa mwanza na gari ukipaki tu hata dakika 2, 5, 7, au 15 yaani unanunua vocha, unasubiria mtu ambaye say umeenda kumpokea na ukafika yuko tayari kitendo cha kubakia mzigo na ndugu yako, au umefika dukani kuuliza kitu na ukaambiwa hakipo, ujue tayari unadaiwa 1500TZS eti parking fee ya siku nzima hata kama umetumia dakika 5 tu hapo mjini.

Zamani ilikuwa unapaki kwa saa TZS 300 tu, kipimo cha chini kilikuwa saa yaani dakika 60, japo kisayansi kipimo cha muda SI unit ni SEKUNDE. watu walilalamika japo walilipat tu hiyo mia 3, leo pomoja na kukua kwa teknolojia TARURA ama kwa makusudi kumuhujumu JPM ama kwa uwezo mdogo wa akili wamekuja na kichinjio cha iwe dakika 1, 2, 5, 15 au 20 utalipishwa 1500TZ kama umepaki siku nzima ambayo haraka haraka tusema ni masaa ya kazi 12.

hali hii ni tata na ya ajabu sana, huduma zinashuka kiwango na bei inapanda kwa kasi, inashuka kiwango kwa maana ipi? maana ni kwamba kulipa sio tena njia fupi ni shule kamili ya namna ya kulipa uanze kwa kutafuta invoice namba GOeP kasha ulipe, mara kadhaa ukiuliza deni lako pia unaambiwa huna kama siku mbili hivi ya tatu ndio unakuta deni limeingia, huenda umekwishasahau kabisa kama ulipaki mjini kwa dakika 2 au 5. huduma mbovu kabisaaa, yaani kulipia ni mbinde japo tunalipia wizi wa mchana tena wakati huu wa serikali ya wanyonge. why charge 1500TZS siku nzima mtu katumia dakika 15?

eti wanapunguza msongamani wa magari mjini, wanaongeza mapato. ongeza mapato kwa kupata pesa halali, yaani mtu alipe kadiri anavyotumia sio dunia ya flat rate hii.

Unapunguza msongamano kwa kumzuia mtu kutumia gari lake ambalo kaliingiza na kulipa kodi? kalipia kodi ya 40TZS kwa kila lilta ya mafuta, kalipia bima na kafanya service na kununua vipuri huku akilipa VAT 18%.? kwa nini msizuia magari kuingia nchini? kama lengo ni magari yamezidi idadi? kwa nini msiruhusu magari mapya pekee kuja nchini ili wachache wamudu gharama hivyo wale waliomudu gharama watumie mali zao kwa raha? kuliko kumuruhusu mtu aingize gari mpatae kodi aweke mafuta anunue vipuri halafu mzuie kuingia nalo mitaani tena kijanja janja.?

Kwa ufupi sana ni kama mnamhujumu jpm na kuleta chuki za kisiasa dhidhi yake. na ama ni mmeshindwa kufikiria kwa kasi ya jpm, tarura mwanza ni vema mkajitathmini na kupisha watu wenye uwezo kumsaidia rais wakafanya kazi hiyo.

1500TZ kwa kila ukiingia mjini ni sawa na kusema mwenye gari sasa hapa TZ analipishwa kila siku 1500x365=(tozo ya mwaka) ikiwa juu ya kodi zingine zote za vipuri mafuta na bima.

HAIWEZEKANI KABISA
 
Hahaa, wasukuma wengi wanamin ni juhudi za ngosha kukusanya mapato, hata laki 2 kwa siku watauza shamba na kulipia.
Mwanza kuna tatizo moja wasukuma hawajui kulalamika hata pale wanapofanyiwa mambo ya kijinga na ajabu ni nduhu tabu.

How come on earth gharama itoke say 300 for average users of city parking areas maana wengi wanaenda kununua vitu na kusepa iwe 1500, mara 5 zaidi why?

YAANI kwa uchumi huuu mtu anakuja na dili dirisha la kukamua raia na wananchi zaidi na zaid why? JE MWANZA kuna city built parking areas? au hizo za roadsides ambazo tumeshazilipia ndio tunatozwa nazo mara mbili mbili kwa mara 5 zaidi?

road sides zipo kwenye michoroya barabara maana gari inafahamika hupakiwa, ndio maana wajenzi wa barabara wanaziweka na tulikwisha zilipia Enzi za road lisence ama sasa 40TZS kwa lita ya mafuta.

CHARGING PEOPLE TWICE OR MULTIPLE TIMES ni wizi tu, na ndio maana hatuendelei kwa kuibia raia
 
Hahaaa, TARURA Mwanza akina ngosha wanaunga juhudi za ngosha. 2 minutes= tzs 1.5k
9 hoursx60mins@tzs 1.5k
Kiburi si uungwana, TARURA MWANZA have to rethink tena faster, hiii ya kumuchonganisha JPM na wapiga kura kijinga jinga hivi sio kabisa. Parking fee itoke 300 ambayo ndiyo ya watumiaji wengi 75% iende 1500 how and why?
 
1500/= kwa siku...

300/= kwa saa... masaa 12 ni 3600/= kwa siku...

Kheri kulipia hiyo elfu 1,500/= kwa siku, alafu hiyo ticket usiitupe kila unapoenda kupaki unaonesha kwamba ulishalipia ya siku nzima na siku haijaisha bado...


Cc: mahondaw
 
Tunataka serikali iwe sikivu maana kujipatia kipato kwa njia za uzurumaji zurumaji sio hulka njema, why park for 5minutes and pay for a full day parking? Ukisia kuanza kushindwa kazi kwa waziri husika ndio hivi
 
Hio ni afadhali saana mbaya kabisa kwa wale wapiga cheni
Yaani ukipaki hata haujashuka ndani ya gari tairi ishapigwa cheni unaambiwa ulipe fain elf50
Kama huna unasema nao kikubwa unawakatia 20 au 30 wanakufungulia‍♂


Ndiyo maana umiwaona wana matumbo makubwa makubwa hayafanani na ujira wao
 
Sijamalizia kisoma uzi huu,nimeishia kwenye maneno "serikali ya wanyonge"...
 
Dar ndio tunanyooshwa, Tsh.500/= kwa saa,usafiri wa umma nao mateso, kutembea na gari lako napo adhabu sasa.
 
huu mfumo wa kulipia na wakucheck gari kama linadaiwa hata sijui..mwenye kuelewa anaweza kunisaidia..
 
Kweli hali ni mbaya Mwanza. Hii si haki kabisa, ni hujuma na hili lazima liangaliwe na viongozi.
Haiwezekani kusimama kidogo tu sh 1500. Kama mfumo ni mbovu bora watuambie tujue na warekebishe haraka. Huu ni unyonyaji kabisa.
Mpaka sasa pia hatujui huu muunganiko wa system na kujua muda halisi wa gari ku park.
 
Back
Top Bottom