Dv 4.19 pcb niende wapi?

kijana acha kutafuta shortcut kwenye maisha..
Ushauri uliopewa na wadau ni mzuri kabisa..Na kama ni kweli unataka SHORTCUT ni bora ukasoma Nursing...(ajira nje nje)..

Ila kama unataka kusoma vitu vya maana na hiyo DIV IV, ni vyema uka-resit..(hii itakusaidia miaka ijayo)..wewe bado ni mdogo, unamuda wa kutosha kujipanga tena na kurudia mitihani..Hakuna mwajiri ambaye anachukua mtu hovyo hovyo..(vinginevyo akupate ajira za wahindi, na mishahara yao ya mawazo)

ALL the best..
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Ok ukimaliza diploma unasoma Aadnaced diploma sio.????? Mimi nimekupa ushauri mzuri we umeona dharau kutoka na PCB yako ungeeda unesi ungeaza kula mshahara mapema alafu ungewezza kujiendelza tena kwa mikopo ya serikali. Kuna sekta ukiwepo unaweza kupata sponsorship hata za nje na hata za serikali. Sekta zenyewe ni elimu na afya. Do u get it.....???????

Ukizuga kwenye ualimu au ukiwa nia ya kusoma unaweza kupata scholarship kirahisi za nchi kama sandnavia. ukakuta from DIV IV to a teacher to degree from scholarship. Lakini ndo hivyo hutaki ualimu hutaki Unesi wakati una DIV IV. may be wewe ni mtoto wa kigogo.

Anyway way wewe mwenyewe ni muamuzi wa maisha yako. Get as may advice as you can lakini mwisho wa siku mwenyewe ndo kuwa muamuzi.

Mkuu inaonyesha hata kama angefaulu na kusomea udaktari angekuja kudharau watu wengine simply because wao ni wakulima, manesi au hata walimu. Kwa kweli s/he needs to get back to the reality. Kwa qualifications zake, options are very limited. Lakini kama akizingatia ushauri kama wako inaweza kumsadia. The issue is not to make the next move but to make the right move. Kwa maneno mengine it is not about WHAT, HOW, WHY but WHY, HOW, WHAT.
 
tatizo lako wewe unataka tukushauri mambo mazuri wakati umefeli...hapa tunakupa live bila chenga..wewe mambo ya kusoma huwezi kwa nini unakuwa mbishi lakini...PCB ulitaka kuwa Dr wa mambo ya wakina mama au? chukua unesi basi...lakini kwa maksi zako hizo wewe mambo ya kilimo ndo yanakufaa sana hasa kilimo cha mboga mboga lima matikiti maji mapera na hata ubuyu una hela sana....viazi pia msimu wa mfungo wa mwezi ramadhani,na pia fuga kuku wa kienyeji maana chipsi zinalika sana na vijana wa shule hasa mabinti ...
dah! Ndugu umetumia maneno magumu kwel, yaan mstar baada mstar umeshindilia msumar wa moto! Tatzo jamaa anakejel, unaomba ushaur, mzur mbaya yote unapokea, unatoa thnx, mwsho una hitimisha mwenyewe.
 
Kijana tafadhali acha nyodo. Umeanzisha hii thread kuomba ushauri. Sasa badala ya kutakafari ushauri uliotolewa na watu unawaita great foolish. Hii inaonyesha huna heshima kabisa. Probably ndio maana ulipata hiyo division 4 due to lack of respect. Mtu mwenyewe umejiunga jana halafu unaleta nyodo na division four yako. Unafikiri wanaochangia humu nao walifeli kama wewe? Kuwa na heshima kijana. Enzi zetu ulikuwa ukipata division three form six ni kwenda kulima tuu. Leo una division four bado unazungumzia kwenda kusoma vitu wanavyosoma wenye division one. Kumbuka wengine humu ni waajiri so wanakupa vitu live.

Kwanza kwa nini umepata division four? Kuna sababu zozote za msingi au ulikuwa unacheza tuu shuleni? Kwa nini ulisoma PCB? Ulikuwa na malengo yoyote ya kusoma hiyo combination? Kwa nini sasa unataka kubadilisha na kusoma marketing, procurement na accountancy? Nini kimekusukuma ubadilishe?

Wadau wamekupa options nzuri. Badala ya kuwakashifu is better uchague option ambayo unaona inakufaa. Kama hazikufai ziache hapa hapa, watakuja wengine na tutawaelekeza. Options ilizopewa kulingana na qualifications zako ni pamoja na:

1) Kilimo - siku hizi hata wasomi wameamua kurevert kwenye kilimo. Ni bora ungeuliza kilimo cha aina gani badala ya kudharau kilimo. Unajua kilimo cha miti wewe?
2) Unesi - because inarelate na combination uliyosoma form six. Kuna nchi kibao zina uhaba wa manesi na wanalipa vizuri kweli.
3) Kurudia/resit - hii itakusaidia kutengeza cheti chako na kuomba kozi za juu zaidi
4) Computer certificate

Mimi ningekushauri uresit. Why? Kwa sababu waajiri makini siku hizi wanataka watu wenye excellent track record. Imagine unaomba kazi ukiwa na degree lakini form six ulipata division 4 ya points 19? Unless utakuwa na sababu za msingi za kupata division four, mwajiri makini ataanza kuku-question.

Lakini la msingi heshimu michango ya watu hata kama ni mibaya. This is JF

Asante mkuu nimekuelewa unapoint nzuri, mimi nimedhamilia kusoma diploma af niingie degree naona iko sawa au vp. Kingine mimi mwanzoni nilipenda udr lakini matokeo yamenitema na nilikuwa na uhakika wa kufaulu coz hata ukiangalia background yangu nilikuwa fit eg. Form 4 nilipata dv 2 ndo nikachaguliwa advance na nimegundua naweza hata kutumia cheti cha 4 kusoma diploma na i believe nitasonga ili kufikia malengo yangu.
 
Jamani nawashauri mjaribu kupitia matokeo ya resiters pcb mwaka huu mwone, yaani kwa hii kombi ukiresit kutoka ni inshu ndo maana mie naonelea diploma itanifaa af Mungu akijalia nisome degree na kwa swala la unesi, kilimo na ualimu kiukweli hizi field naziheshimu lakini moyo wangu haupo kabisa, na nafikiri mnajua mtu anasoma kitu ambacho hata moyo wake unapenda sasa ukilazimishwa kusoma kitu ambacho hupendi,huwezi na hauafikiani nacho ndo yaleyale unakuja kuboronga kazini. Mawazo yenu yote nayapokea ila na mimi najaribu kuchuja na kuangalia hili litanifaa ili nipate mwafaka. Na nimejaribu kuulizia Ifm nimeambiwa naweza kusoma diploma, ngoja nisome hiyo diploma af degree nitacheki mbeleni.
 
Ungeomba radhi tungekuelewa zaidi....baada ya kuona wadau wamegeuka mbogo ndo unaleta usamaria wako .Big NO
 
Nimefuatilia naona huyu jamaaa ni msanii tu. anawachora tu hapa. watu watatoa consluntacy wakati hana mpango wowote. na elimu

Ebu tuambie PCB syllabaus ya biology au Kemia od fizikia topic tatu za mwazo form 5 ni zipi?
 
Ebana cheki tumaini ya hapo dsm utafanikiwa,pia huku arusha pre entry ipo makumira,stephano university moshi zote zina pre entry. Mambo ya kushauriana mtu akalime c vema coz hajauliza mambo ya kilimo hapa.
 
Safi mkuu unaweza kujua ada yao.
 
sio kilamtu njia yake inakua nyoofu wapo ma profesor kibao ambao wamesha wah kuwa na wakati mgumu kimasoma kama huo ulio nao kwahyo usikate tamaa kikubwa angalia nikipi unachotaka kukisoma napia uangalie na uwezo wako pia wakimasomo had ukasoma pcb inamana una pass mark nzur form 4.anza na certficate labda ndio option uliyo nayo kama hutaki ku rudia mtihani kwa pass mark hyo uliyo pata huwez kuanza na Dploma..Tuliza akili jpange upia utafika unapotaka kufika kielimu jitahdi usikurupike
 
tatizo lako wewe unataka tukushauri mambo mazuri wakati umefeli...hapa tunakupa live bila chenga..wewe mambo ya kusoma huwezi kwa nini unakuwa mbishi lakini...PCB ulitaka kuwa Dr wa mambo ya wakina mama au? chukua unesi basi...lakini kwa maksi zako hizo wewe mambo ya kilimo ndo yanakufaa sana hasa kilimo cha mboga mboga lima matikiti maji mapera na hata ubuyu una hela sana....viazi pia msimu wa mfungo wa mwezi ramadhani,na pia fuga kuku wa kienyeji maana chipsi zinalika sana na vijana wa shule hasa mabinti ...

Kigogo you have made my day kwa majibu murua, jitu limefeli halafu linatafuta shortcut, nina mashaka kama haza hizo diploma ataweza.
 
Back
Top Bottom