Duu! Londa kafilisika hivi?

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
Meya wa manispaa ya Kinondoni aliyemaliza muda wake, Salum Londa, `amemnanga' mgombea ubunge wa jimbo la Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee, kuwa anatumia taaluma ya sheria kuganga njaa.
Londa ambaye alikuwa diwani wa kata ya Kawe, alishindwa kutetea kiti hicho na kwenda kuwania ubunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini mkoani Lindi, ambapo alishindwa.
Akimpigia debe mgombea ubunge wa jimbo la Kinondoni (CCM), Idd Azan, Londa alisema Mdee ambaye kitaaluma ni Wakili, anaishi kwa kutegemea kesi za wateja wake na kwamba hana uwezo wa kuongoza.
Mkutano wa kampeni hizo ulifanyika katika maeneo ya Manzese, kata ya Ndugumbi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Pia Londa alimshambulia kwa maneno ya kejeli mgombea wa Chadema katika jimbo la Ubungo, John Mnyika.
Alisema wanasiasa hao vijana wamekuwa wakiwachonganisha watu, ili wapate hela katika kutetea kesi zao.
"Hivyo kazi yao kubwa ni kutaka watu wagombane ili wajipatie fedha," alisema Londa.
Alisema kuwa Mnyika amekuwa akidai kuwa CCM haiwawezi ila amechemka kwani jimbo hilo la Kinondoni haliwezi kwenda kwenye upinzani na kwamba wamejipanga kikamilifu. Hata hivyo, alipowasiliana na NIPASHE kwa njia ya simu, Mdee alisema kauli za Londa ni sehemu ya madhara yanayotokana na kushindwa katika uongozi.
Mdee alisema Londa anamhofia (Mdee) na Mnyika kwa kutambua kwamba wakiingia bungeni, miongoni mwa kazi watakazozifanya ni kuhakikisha Meya huyo wa zamani anawajibishwa kutokana na kashfa zinazomkabili.
Londa ni miongoni mwa viongozi waliotajwa mara kadhaa kuhusika katika kashfa ya migogoro ya ardhi hasa uuzaji holela wa viwanja na maeneo ya wazi.
Hata hivyo hakuna hatua za kisheria zilizochukuliwa na kumtia hatiani.
Lakini Mdee alisema kama Londa anajiona yupo safi, alipaswa kuyasema maneno hayo katika jimbo la Kawe alipodai kuwa wananchi hawataki kumuona.
"Mwambieni Londa asikimbilie Kinondoni, aje huku Kawe alipokuwa diwani wao, tuzungumze huku, ayaseme hayo," alisema.
Kwa upande mwingine, Londa alisema Azan amefanikiwa kuleta maendeleo jimboni humo, hivyo kuwataka wananchi wampigie kura.
Kwa upande wake, Azzan alisema mambo aliyaahidi mwaka 2005, ameyatekeleza na kwamba kwa sasa amejipanga kuliboresha zaidi katika jimbo hilo.
Alisema kama atashinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ataziboresha sekta mbalimbali za jamii ili ziwanufaishe wananchi.




CHANZO: NIPASHE
 
Siasa za maji taka.
Kama umeshindwa kuwapatia maendeleo watu, achia nafasi wenye uwezo wafanye hivyo na siyo kuwabeza ilhali unajua HUWEZI hata kwa miujiza.
 
Ni lazima Londa amuofie HALIMA MDEE mmesahau jinsi MDEE alivyokabana bungeni MAKAMBA na LONDA kuhusu viwanja na uozo wao mwingine, Eti MAKAMBA na LONDA wakampeleka katika kamati ya maadili ya BUNGE kuwa amewachafua na kutumia lugha isiyofaa BUNGENI kamati kupita SPIKA ilimtaka MDEE awasilishe ushahidi wa kauli zake na MAKAMBA na LONDA wawasilishe utetezi wao kuthibitisha kuwa wamechafuliwa. HALIMA MDEE akawasilisha nyaraka za uthibitisho wa hoja zake MAKAMBA na LONDA wakaanza longolongo bila kuchelewa MAKAMBA akaibuka na kudai ETI amemsamehe HALIMA maana bado ni Binti mdogo hivyo si vyema kumshitaki akikua ataacha kuropoka, Mkubwa LONDA yeye akawa bubu. Hivyo LONDA akimuona MDEE anamuhofia utadhani wanafunzi wa shule za msingi wa enzi zetu wakisikia kuna Nyonya damu (muumiani)
 
ccm woote ni wezi ama wanategemea kunufaika na udokozi wa mali ya umma. kwahiyo londa nisawa na kina RA WANAVYOOGOP chadema.
 
watu wengine bwana....kwa nini asiende kuwaambia wananchi wa kawe ambako MDEE anagombea kama maneno yake (LONDA) anadhani yana-impact yoyote?
 
Kumbe Londa anaogopa wanasheria? Amefanya nini mpaka aogope?

Ana madudu mengi ya uporaji wa viwanja huku Dar. Mbezi Beach kachukua viwanja vingi sana, alipokuwa Meya wa Kinondoni. Anatajwa kuhusika kwenye ripoti ya uchunguzi kuhusu uuzwaji wa viwanja vya wazi kwenye Wilaya ya Kinondoni!

Lazima awaogope wanasheria, wanamsubiria Novemba, kesi zitakapoanza kuunguruma Kisutuuuuuu!
 
Back
Top Bottom