Inaendelea..
Idadi ya wapiga kura mwaka huu imepungua kulinganisha na 2008. Kura walizopata wagombea (popular vote) zinakaribiana sana ukilinganisha na uchaguzi uliopita. Hii maana yake ni kuwa pamoja na Obama kushinda lakini kura zilizomchagua zimepungua.Kwa taratibu za uchaguzi marekani wingi wa kura si hoja, hoja ni idadi ya wajumbe wanaohitajika kumchagua rais abao Obama amepta zaidi ya 300, wajumbe 30 zaidi ya kiwango kinachohitajika(270)
Obama aliungwa mkono na wanawake, vijana kati ya 20-29, wapenzi wa jinsia zinazofafana, weusi na Walatino.
Ukiangalia mgawanyo idadi ya wanaume waliompigia kura hasa weupe imepungua kwa kiasi sana.
Romney aliungwa mkono na weupe wengi, evangelics, wazee na wahafidhina.
Katika makundi yaliyomuunga mkono, Obama alipata uungwaji mkono mzuri sana ukilinganisha na mpizani wake.
Siri kubwa ya mafanikio ya Obama ni kuzingatia mchanganyiko(diversity), kusimamia anachokiamini bila kutetereka hata kama anajua kitamgharimu kwa upande mwingine.
Obama ameunga mkono mashoga hadharani ingawa alijua kuwa kufanya hivyo atakosa kura za evangelics na hata watu wa dini zingine kama waislam. katika uchaguzi uliokaribiana sana kila kura ni muhimu na alilifahamu hilo.
Kitu kimoja ni kuwa hajawahi kubadili msimamo kwasababu alijua kuna kura nyingine.
Obama alisimama kidete kuhusu mikopo ya wananfunzi na umuhimu wa elimu, kwahilo tu akavuna vijana wengi.
Amepitisha sheria inayohusu masilahi ya akina mama, jambo lililomuongezea uungwaji mkono na wanawake.
Kwa upande wa Walatino, Obama amekuwa mstari wa mbele kutaka watoto waliozaliwa USA na wazazi waliohamia kwa njia za haramu wapewe uraia.
Tofauti na Obama, Romney alikuwa katika nafasi isiyoeleweka. Uumini wake wa kanisa la Mormon ulihusishwa na kanisa la kishetani na wengi hawakuwa confortable hasa wale evangelics. Romney ametumia muda mwingi sana kuisafisha imani yake na si kueleza sera zake. Tumeona katika mkutano mkuu wa Republican ambapo Romney alitumia muda mwingi sana kuliongelea.
Mitt hakuwa na sera zozote zinazohusu vijana au wakina mama. Tena kwa akina mama Republican walitoa kauli zilizo wafanya Democrat washupalie ajenda ya akina mama. Kauli za kejeli na dharau.
Na ndivyo ilivyokuwa kwa mambo mengine.
Kwa upande wa Romney kampei yake ilikumbwa na mambo mengi. Kwanza walianza kumshaulia Obama kwa kejeli na matusi. Walizusha uongo na kugeuza hata hadithi. Walifikia mahali pa kusema mdororo wa uchumi ni matokeo ya sera za Obama wala si Bush. Baada ya kutumia miezi takribani 7 bila mafanikio ndipo walipogeukia agenda ya uchumi na hapo uhai ukawa umerudi. Hilo ni kosa la kwanza la Romney ambalo tutaliangalia katika mizani ya siasa zetu baadaye.
Mitt alibanwa sana na Obama camp kwasababu yakubadili sera. Wakati akiwa Gavana wa Massachussets Mitt alianzisha mpango unaofanana na Obama care, in fact wataalamu wake ndio Obama aliwatumia.
Alipoanza kampeni akawa kati na kati na mwisho wa kampeni akageuka na kusema ata repeal Obama care.
Mitt Romney alikuwa na mzigo wa kauli zake kuhusu auto bail aliyeosema haina maana na makampuni ya magari yaachwe yafisilisike tu. Viwanda vingi vipo Michigan na Ohio. Kwahiyo Ohio aliyo ihitaji sana ilikuwa kikwazo kwake.Akatumia muda mwingi sana Ohio bila kujua kuwa Colarado ilikuwa inamponyoka.
Romney amenukuliwa akisema 47 asilimia wanaishi kwa foodstamp na hao watampigia Obama. Kauli ilimmaliza kisiasa.
Wakati anasema anajua jinsi ya kutengeneza ajira, kumbu kumbu zinaonyesha aliua kampuni ya BAIN na watu kupoteza ajira, Hadi hapo wapiga kura wakalazmika kuiangalia historia yake kwa ukaribu jambo lililomletea matatizo
Ingawa mdahalo wa kwanza Romney alionekana kuibuka kidedea, inajulikana sasa kuwa uungwaji mkono mkubwa ulitokana na hamasa ya Republican waliokuwa wamekata tamaa na wala siyo sera. Katika mdahalo huo Mitt alionekana kuvuruga historia ya serikali ya Obama kwa makusudi na upotoshaji huku akiwa hana majibu ya sera zake.
Midahalo miwiwli iliyofuata Obama akatumia Chicago style na kumvuruga sana Mitt. Mdahalo wa mwisho ndio ulivuta kasi ya Romney nyuma. Baada ya hapo Romney akawa hana hoja kwasababu hoja za uongo zote zilitenguliwa.
TUANGALIE FUNDISHO.
Hapa tunajifunza kuwa ni lazima wagombea na vyama vyao visimame kidete katika misimamo inayohusu masuala ya kitaifa hata kama hayapendezi kundi lolote. Obama ndivyo alivyofanya kama nilivyowahi eleza.
Utashangaa chama cha upinzani kama cha Chadema hatujui msimamo wake halisi kuhusu baadhi ya masuala ya kitaifa. Mfano ni suala la katiba mpya na muungano. Hadi leo hakuna ajuaye CDM inasimamia wapi, kwa misingi ipi na kwanini.
Ni vema misimamo ikawekwa wazi ili kujua nani anasimamia wapi na wala siyo kuwa ''opportunist''
Pili, kuna funzo kuwa kumwangusha adui yako kisiasa si kumshambulia.
Hivyo ndivyo inavyotokea kwa upinzani kuweka hoja za ubadhirifu kama sera za chama.
Ni haki na vema kufanya hivyo, lakini basi tuambiwe mbadala.
Wananchi wanataka kusikia mbadala na si 'mabomu' ya wala rushwa tu.
Hapa pia nina mfano wa CDM. Chama hicho kina sera ya majimbo, labda atoke mmoja miongoni mwetu aeleze kwanini majimbo, yana manufaa gani ukilinganisha na muundo ulioopo. Huwezi kulisikia hili hata siku moja.
Wananchi wanataka kusikia kilimo, elimu na afya vitashughulikiwaje tofauti na ilivyo sasa.
Tatu, tunajifunza kuwa kampeni si mikutano ni mikakati. Hivi leo kuna sehemu wapinzani wameaacha kabisa kuingia na hakuna sababu za misingi pengine ni woga tu au kutokujua. Kwanini Iringa iwe ngome kubwa ya wapinzani na si Morogoro!
Kwa msingi huo wapinzani wanacheza karata ya Romney ya kuwatenga wapiga kura. CCM inalifhamu hilo ndio maana mara zote imejipanga katika maeneo dhaifu ya Upinzani. Haieleweki kwanini wapinzani waache jimbo kama la Korogwe kwa mtu asiye na elimu kabisa.
Lakini pia wapinzani waangalie sana makundi kama ya akina mama. Inasikitisha kuona kuwa chama cha upinzani kama CDM hakuna sauti ya akina mama. BAWACHA imebaki kuwa sehemu ya viti maalumu badala ya kiunganisho cha akina mama wa Tanzania. Kwa msingi huo watu wanaifahamu UWT zaidi kuliko chama kingine kwasababu tu ya udhaifu.
Kundi hili limemuumiza sana Romney na huenda dhambi hiyo ikatafuna wapinzani Tanzania.
Naomba ieleweke kuwa mijadala yetu haichukui sura za kisiasa. Ninaposhindwa kuongelea CCM ni pale ukweli unapojidhihiri kuwa huwezi kumfunza mbwa mzee mbinu mpya!
Tutaendelea....