Duru za siasa - Matukio

UCHAGUZI WA MAREKANI

Kampeni za uchaguzi wa Marekani zinaendelea kwa kasi. Mwishoni mwa wiki hii chama cha Republican kitakuwa na mkutano wao Tampabay, Florida kumuidhinisha Mitt Romney na Paul Ryan kama wagombea wa chama chao.
Baada ya hapo Democrats nao watafanya mkutano wao Carolina kwa minajili hiyo hiyo.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2008 Demo walianza kufanya mkutano mkuu wa taifa kwanza wakifuatiwa na Republican.
Hii haitokei kwa kuwahi au kuchelewa bali utaratibu maalumu ambao tutaufafanua.

Uchaguzi wa Marekani ni tofauti na huu wa hapa nyumabani au wa commonwealth countries nyingi. Wao Rais hachaguliwi moja kwa moja kwa kura za wananchi (popular vote). Wana utaratibu wao unaoitwa electral college. Nisisitize kuwa utaratibu wa marekani si wao peke yao kuna nchi na hata vyama vya siasa kama Labour cha Uingereza vina utumia.

Kinachomchagua rais wa marekani ni kura ya mtu lakini si moja kwa moja bali kupitia utaratibu tutakaouleza.
Rais anachaguliwa kwa utaribu gani,tarehe zinapangwa vipi na majimbo gani yenye ushawishi katika kura ni baadhi ya mambo tutakayoyaangalia kwa ukaribu sana katika kipindi hiki.

Itaendelea.......
 
KIFO CHA ZENAWI

Pamoja na hayo Zenawi amejitahidi kutumia misaada vizuri ilkiwa ni pamoja na mradi mkubwa sana wa umwagiliaji na umeme kwa kutumia sehemu ya mto Nile. Amefanikiwa kuifanya Ethiopia iwe stable kwa kiasi fulani ingawa pia ni mwepesi kutumia FFU kuzima demokrasia.

Wasi wasi uliotanda ni jinsi gani nchi itatawalika baada ya Zenawi. Wapo wanaodai hali inaweza kuwa kama ya Iraq ambapo mkono wa chuma ndio uliokuwa sahihi kuiweka nchi sawa.
Nini kinafuta baada ya Zenawi bado ni kitendawili

Tusemezane

Ethiopia ya Meles ilitawaliwa kwa mkono wa chuma. Katiba yao ni Federal system na maajimbo yalitakiwa yawe na uhuru kiasi fulani lakini hali halisi haiko hivyo bali serikali kuu inasimamia karibu kila kitu.
Kati ya majimbo 9 yanayofanya muungano wa Ethiopia, matano yana vikundi vya waasi wanapigana kujitenga. Hali ni mbaya zaidi kwenye mikoa ya Somali (ogaden), Oromia na Afar ambako sehemu kubwa ya mikoa hiyo inatawaliwa na waasi. Na imekuwa kama ada ya kila mwaka kwa serikali kuu kutuma vikosi vya jeshi kufanya operesheni katika maeneo haya ingawa huishia kuwaua wakulima maskini waishio vijijini kwa kuunga mkono uasi. Baadhi ya maeneo haya hufungiwa msaada wa chakula wakati wa uklame kama adhabu.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, upinzani waliungana dhidi ya chama tawala na hakika walishinda ingawa matokeo yalichakachuliwa na wabunge wachache wa opposition waliopita wakaishia jela kwa kosa la 'uhaini'.

Meles ameondoka na huku nyuma ameacha ombwe la uongozi; Deputy wake Hailemariam Desalegn ambaye contitutionally ndie angechukua madaraka hadi uchaguzi wa 2015 bado kuapishwa, eti nchi iko kwenye maombolezo. Duru za siasa ndani ya chama tawala zinaeleza kuwa Hailemariam ambaye anatokea kabila dogo kusini mwa nchi aliwekwa pale kwa vile asingekuwa tishio kwa Meles kisiasa, na hawa jamaa wanapanga akaimu kwa muda wakati wanatafuta miongoni mwao nani akalie nafasi hiyo ya juu.

Nilizungumza na rafiki zangu wawili wa-Ethiopia; m-Oromo na m-Somali, walionyesha kusherehekea kifo cha Meles na kuashiria huenda mapambano ya kujitenga Waoromo na Wasomali yakapata msukumo mpya.
Iwapo Hailemariam hataapishwa ndani ya wiki chache zijazo, tutarajie mwanzo wa matatizo makubwa katika eneo hili la pembe ya Afrika.
 
Ethiopia ya Meles ilitawaliwa kwa mkono wa chuma. Katiba yao ni Federal system na maajimbo yalitakiwa yawe na uhuru kiasi fulani lakini hali halisi haiko hivyo bali serikali kuu inasimamia karibu kila kitu.
Kati ya majimbo 9 yanayofanya muungano wa Ethiopia, matano yana vikundi vya waasi wanapigana kujitenga. Hali ni mbaya zaidi kwenye mikoa ya Somali (ogaden), Oromia na Afar ambako sehemu kubwa ya mikoa hiyo inatawaliwa na waasi. Na imekuwa kama ada ya kila mwaka kwa serikali kuu kutuma vikosi vya jeshi kufanya operesheni katika maeneo haya ingawa huishia kuwaua wakulima maskini waishio vijijini kwa kuunga mkono uasi. Baadhi ya maeneo haya hufungiwa msaada wa chakula wakati wa uklame kama adhabu.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, upinzani waliungana dhidi ya chama tawala na hakika walishinda ingawa matokeo yalichakachuliwa na wabunge wachache wa opposition waliopita wakaishia jela kwa kosa la 'uhaini'.

Meles ameondoka na huku nyuma ameacha ombwe la uongozi; Deputy wake Hailemariam Desalegn ambaye contitutionally ndie angechukua madaraka hadi uchaguzi wa 2015 bado kuapishwa, eti nchi iko kwenye maombolezo. Duru za siasa ndani ya chama tawala zinaeleza kuwa Hailemariam ambaye anatokea kabila dogo kusini mwa nchi aliwekwa pale kwa vile asingekuwa tishio kwa Meles kisiasa, na hawa jamaa wanapanga akaimu kwa muda wakati wanatafuta miongoni mwao nani akalie nafasi hiyo ya juu.

Nilizungumza na rafiki zangu wawili wa-Ethiopia; m-Oromo na m-Somali, walionyesha kusherehekea kifo cha Meles na kuashiria huenda mapambano ya kujitenga Waoromo na Wasomali yakapata msukumo mpya.
Iwapo Hailemariam hataapishwa ndani ya wiki chache zijazo, tutarajie mwanzo wa matatizo makubwa katika eneo hili la pembe ya Afrika.
Kakalende, naliona tatizo la Ogaden likirudi tena.
Ulichosema kuhusu anayekaimu ni tatizo la katiba za kiafrika zinazoweza kubadilika kila dakika.
Jeshi halina imani sana na huyu bwana na kwa vile ametoka uliKosema hana nguvu ya kisiasa. Well said and written Kakaelende.
Ni kweli kuwa mkono wa chuma ulitawala na tuliona wakati wa uchaguzi wasomi walivyosagwa na madereya.

Hali bado ni tete sana nchini Ethiopia na tutaendelea kuwaletea yanayojiri hapa Duru za siasa matukio.
 
AIBU YA FAMILIA YA KIFALME UINGEREZA

Tutaendelea kujadili mada ya uchaguzi wa marekani kama ilivyoanza katika bandiko 61 tukiangalia taratibu za uchaguzi wao kwa mtindo wa electral college.

Kwa wakati huu mkutano mkuu wa chama cha Republican unaendelea Tampa Bay FL, huku kukiwa na taharuki kubwa ya kimbunga cha Isaac kuharibu taratibu na kwa kuanzia tu mkutano utaanza rasmi kesho kwa hotuba ya ufunguzi.
Tutaendelea kujadili kadri matukio yanavyotokea.

Aidha, tutajadili hali tete nchini Ethiopia, Syria na Mashariki ya kati kwa ujumla wake.
Katika Duru za Siasa matukio, leo tuliangalie tukio lililopewa uzito na vyombo vingi vya habari duniani.

Tukio hilo ni lile la mwanafamilia ya kifalme kuonekane katika picha akiwa utupu. Pengine ni bahati kwa wengine kumuona mfalme 'mtarajiwa ikibidi' akiwa utupu.

Nasema ni mfalme mtarajiwa ikibidi kwasababu kufuatana na mtitiriko wa uongozi wa kifalme yeye kwa wakati huu ni namba 3, baada ya Prince William na Baba yao Prince Charles. Kwa maneno mengine endapo wanaofuata hawatatumikia ufalme kwa kiwango cha Elizabeth basi anaweza kuwa mfalme japo kwa wiki moja.

Hata hivyo, kufuatana na tabia ya Harry kwa sasa Waingereza wengi wameondoa matumaini juu yake.
Kumekuwepo na shinikizo la kubadili muundo wa utawala 'throne' katika hekalu la Backingham.
Muundo unaopendekezwa ni ule ambao hautamruka mwanamke.

Watafiti wa historia wanaonyesha kuwa jina la mfalme aliyejulikana kama Harry linashabihiana sana na Prince Harry wa kizazi chetu. Wote ni wepesi katika vurugu za hapa na pale hasa kuwanyemelea akina dada.

Prince Harry alipewa hadhi ya kuwa mgeni katika kufunga Olympic akimwakilisha Malikia na familia ya Kifalme. Hili lilifanyika ili kumleta karibu na shughuli za utawala na ufahamu wa dunia ikiwa ni pamoja na kujitambua.

Baada ya hapo alielekea Las Vegas Marekani ili kupunguza uchovu (kama mwanamfalme anaweza kuwa nao).
Las Vegas ni jiji la maraha na starehe, jiji lisilo lala. Wengine wanal
iita sin city wakimaanisha mji wa dhambi. Huko kitafanyika kila kitu kinachowezekana hapa duniani.

Harry akiwa na rafiki zake na kimwana, alipigwa picha na mmoja wa washiriki wake bila kujijua na ghafla picha hizo zikaingia katika mtandao wa habari dunia kama upepo, wenyewe wakisema ' gone viral'.
Hakika hili ni tukio lilofedhehesha kasri ya kifalme na umalikia kule London.

Kumekuwa na mgongano wa mawazo kuhusu jambo hili. Waingereza ambao ni mafundi wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari wamejitahidi kulikingia kifua tukio hili wakisema yule ni kijana na alikuwa katika nafasi yake kama kijana mwingine. Hakukuwa na idhini yake kupigwa picha na hilo ni ukiukaji wa 'privacy'.

Magazeti yameacha kuandika tukio hili ili kuisitiri kasri. Gazeti pekee lilojitokeza ni la The sun ambalo mhariri wake amesema, kama mwana wa familia ya malkia akikaa uchi siyo habari, je habari ni nini?

Upande wa pili unasema, Harry hafai kupata kinga yotote. Ingelikuwa amesukumwa mlangoni basi hiyo ingekuwa habari duniani. Wanasema yeye akiwepo mahali basi bendera ya Uingereza inayojulikana kama union jack itapanda, na wimbo wa taifa God bless our king/Queen utaimbwa. Kwa muktadha huo Harry anadhima ya kulinda heshima kama anayopokea.
Wao wanasema with great power comes responsibility kwa maana kuwa nyadhifa huambatana na wajibu.

Kuna kundi la tatu linalosema, je inakuwaje mwanawa familia asiwe na walinzi wa kumuongoza? Ukweli ni kuwa alikuwa na walinzi lakini walinzi wanamipaka, hawawezi kumkodolea macho pale anapokuwa anapata ulua kwa kuikonga nafsi yake na barafu wa moyo, wala hawawezi kumwekea kiwango cha glass za mvinyo ingawa wanaweza kushauri uwepo wake katika tukio.

Yote haya bado ni maswali yasiyo na majibu huku waingereza wenye kodi zao wakilalama kuwa zinatumika kulea baradhuli 'Hooligan'. Hakika Harry ameendelea kutengeneza vichwa vya habari kwa njia ya aibu.

Tusemezane
 
UCHAGUZI WA MAREKANI

Mkutano wa Republican umemalizika ukiwa umefunikwa na tufani(hurricane) ISAAC ambayo kwa takwimu ilitokea katika siku ile ile na muda ule Katrina ilipotokea kule Lousiana na New Orleans. Tofauti na Katrina hii ilikuwa ya kiwango cha dhoruba (storm).

Hali ya hewa imeathiri sana mkutano mkuu kwasababu baadhi ya watu katika majimbo 4 wapo katika wasi wasi mkubwa wa maisha. Kwa maneno machache coverage yake imekuwa chini ya kiwango kilichokusudiwa.
Hatujafahamu effectiveness ya waoengaji lakini ni wazi kuwa Democrat watajibu vikali mapigo waliyopata wiki itakayofuata.

Wakati hayo yakiendelea kuna jambo limejitokeza ima kwa bahati mbaya au kukusudia.
Katika kipindi hiki cha uchaguzi kila mbinu inatumika. Jopo la watu makini 'think tank' ya Republican wanajua wazi kuwa eneo lao la usalama wa taifa limedhibitiwa baada ya kutokuwa na mashumbulio japo hadi sasa na kumuua Osama.

Obama pia amelisambaratisha vibaya kundi la alqaeeda na kumaliza uongozi wa juu ingawa kila siku wanatokea wengine.

Kwa kutambua hilo, think tank imeamua kufanya mkakati wa kuzuia Obama asitumie kifo cha Osama kupata credit za kisiasa. Ametokea mmoja wa Seal kile kikosi kilichomuua Osama anataraji kutoa kitabu kinachoeleza jinsi Osama alivyo uawa. Maelezo yake yanatofautiana na yale ya Rais Obama wakati akihutubia taifa kuhusu kifo cha Osama.
Habari za mwanajeshi huyu ambaye sasa sura ipo wazi zinatolewa na Televisheni ya Fox. Jitihada zote ni kutaka kuvunja nguvu hoja kuhusu ukweli kuwa Obama amefanya kilichowashinda akina Bush.

Lakini pia Republican wamefanya hivyo kama mkakati 'pre-emptive strategy' kwasababu zipo fununu kuwa watengeneza filamu wanatarajia kuitoa filamu ya kifo cha OBL hiyo siku za karibu sana na uchaguzi ambazo zingemuongezea Obama umaarufu.

Kwa mantiki hiyo watengeneza filamu itabidi warudi kuihariri ili isije ikaleta mkanganyiko kati ya maelezo ya Rais na mtu aliyekuwa katika operesheni. Haya yote ni siasa za Marekani.

Waliberali wana hoja kuwa endapo mambo yangeharibika Obama angebeba lawama kwanini asisifiwe pale yanapokwenda vizuri?
Wahafidhina wanasema hilo lilikuwa suala la kitaifa na wala Obama hapaswi kupewa sifa kwasababu ni ulinzi wa taifa na siasa haipaswi lkuwemo.

Kitu kimoja kilichojitokeza katika mkutano wa Republican ni kuwa ile agenda ya usalama wa taifa ambayo watu kama Meya wa zamani wa New York Rudi Gullian wameitumia kisiasa imekosa mashiko kabisa katika mkutano huu.

Hoja ya uchumi ndiyo hasa inatawala lakini pia ina ugumu hasa pale Republican wanapoambiwa kuwa miaka 8 wakiwa madarakani wameifikisha Marekani hapo tofauti na hali ya sasa. Ingawa hali ni mbaya sana lakini si kwa kiwango cha kupoteza kazi 600,000 kwa mwezi.

Hata hivyo historia inaonyesha kuwa katika kiwango cha asilimia 8.2 ukosefu wa ajira ni nadra sana Rais kurudi madarakani. Takwimu za miezi miwili kuhusu biashara, mitaji, mauzo, ujenzi zinaonyesha kuongezeka. Hata hivyo hazijaweza kuondoa kiwango cha kukosa ajira kutoka 8-2 na kurudi chini.

Tutaendelea kuleta matukio kadri yanavyojiri.
 
UCHAGUZI WA CCM 2012

Kwanza nimshukuru msomaji mmoja aliyeaniandikia na kuuliza kwanini wakubwa ndani ya CCM wanapigana vikumbo katika nafasi kama za ujumbe wa NEC na CC badala ya kujijenga kama wana nia ya kuwania uongozi wa Taifa.

Swali hili nimelipenda sana kwasababu linagusa siasa za nchi yetu na lina mantiki kubwa sana.
Ieleweke kuwa vyombo vikubwa vinavyofanya maamuzi katika vyama vya siasa kama CCM ni ujumbe wa halmashauri kuu na kamati kuu ya chama. Mkutano mkuu ni kuidhinisha maamuzi ya vikao vya CC na NEC. Kwahiyo nguvu kubwa ndani ya chama ipo katika CC na NEC wala siyo Ubunge, Uwaziri, ukuu wa mkoa n.k.

Kwa mfumo wa CCM ukiweza kuikamata NEC na CC basi mambo yatakunyookea sana.
Kama mnakumbuka miaka ya nyuma baada ya Kikwete kuenguliwa kwa kura 'kutokutosha' aliunda mtandao wake kwa kushirikiana na EL.

Mtandao huo uliojulikana kama wa vijana, ukwelihaukuwa na madhumuni ya ujana kama tujuavyo. Ilikuwa ni mbinu ya kuwaondoa wazee wenye hekima zao katika uongozi wa CCM taifa. Tulishuhudia wafanyabiashara wenye mabilioni wakigombea ujumbe wa NEC na kundi la mtandao likitumia mamilioni kulaghai umma kwa kibwagizo cha huu ni wakati wa vijana.

Hili lilipofanikiwa wakawa tayari wameshajenga ngome zao ndani ya UWT, UVCCM na Wazazi.
Jumuiya hizi zina uwakilishi mkubwa sana ndani ya NEC na CC kwahiyo nguvu yao ni kubwa sana kimaamuzi.
Hata pale wazee wlipomshtua BWM, usalama wa taifa ukamwambia mizizi tayari imeshaota, kumtosa JK kungekuwa na madhara makubwa sana.

JK akatangazwa kuwa mgombea na kisha Rais. Ushahidi wa mtandao ni pale JK alipounda baraza kubwa sana la mawaziri na manaibu lenye watu 60. Kwa nchi masikini kama yetu hii ilikuwa ni kulipa fadhila na wala si kutawala na kuendesha
serikali. Yaliyoendelea na yanatokea tunayajua.

Kwasasa hivi wakati uchaguzi ukikaribia mwezi Oktoba, wale wenye kiu ya uongozi kama EL, Sitta n.k tumeona wakipita huku na huko kujinadi na kunadi watu wao. Majuzi Sitta alikuwa Bukoba na kufanyiwa sherehe kubwa sana ya kijadi.
EL naye amekazana kutokea katika vyombo vya habari hata kuinanga serikali aliyoitumikia kwa sera zile zile.

Lakini pia ukichunguza utaona wagombea hawa wakipita maeneo fulani yenye nguvu za wagombea ili kuwasaidia wakijua kuwa uwepo wa wajumbe hao NEC na CC ndiyo ufunguo wa mambo yao. Fuatilia ziara zao utaona kuna mwenendo fulani.

Nikumbushe kuwa wakati Sitta akiwa Spika alikuwa mwiba mkali kwa kundi la mtandao kwa kuruhusu mijadala inayohusu mambo ya kitaifa. Wanamtandao wakamsubiri wakati wa kuomba tena nafasi hiyo. Kwa vile wao walikuwa wanamiliki CC na NEC wakatumia njia rahisi tu kusema huu ni wakati wa akina mama na hapo Sitta akapoteza nafasi ya Uspika.

Nafasi ya Uspika ilipangwa makusudi kabisa kwa kuwaweka akina Anna Makinda, Anna Abdallah na Kate Kamba. Hawa wote ni watu wa kundi moja na uwepo wa Anna na Kate Kamba ilikuwa kuonyesha tu kuwa nafasi hiyo ilikuwa inaliliwa na akina mama na ilikuwa ni zamu yao. Ukweli ni kuwa walijua kuwa Spika ajaye ni Makinda.

Makinda ni sehemu ya kundi la mtandao lililofaidika sana na fedha haramu za mafisadi. Kwahiyo aliwekwa pale kulinda masilahi ya wakubwa waliopo ndani ya CC na NEC. Tunaona jinsi anavyozuia mijadala ya kitaifa, jinsi alivyogeuka kuwa ' mwenyekiti' wa chama ndani ya bunge. Amesahau kuwa amekalia kiti chenye nembo ya taifa.

Kwa ufupi ni kuwa uchaguzi wa mwaka huu ndio utaamua wajumbe watakaounda vyombo vya maamuzi ya kuwapata Wabunge na Rais watakaogombea mwaka 2015. Ni cuhaguzi utakaojaa kila aina ya mbwembwe na rushwa. kama kuna kipindi wapokea rushwa wanataraji mavuno basi hiki ndicho haswa!

Watu gani hatimayao ipo mashakani, tutaendelea......
 
Inaendelea....

Tumesema kuwa NEC na CC ndizo nguzo za chama na kama utazikamata basi utakuwa salama. Vita ndani ya UVCCM, UWT na Wazazi ni vita ya makundi na si ya watu. Kwa mfano, UWT kuna Sofia Simba ambaye ni msemaji mku wa kambi ya mtanadao -mafisadi na Anne Kilango aliye katika kundi la CCM wazee.
Unapokuwa na wajumbe wa NEC muhimu kama hawa utakuwa umefanikiwa sana. Maamuzi yao yataathiri chaguzi zote za ngazi za chini na kuleta wajumbe wengi zaidi ndani ya NEC.

Katika mchakato huu kuna watu ambao ni waathirika wa NEC na CC watake wasitake. Tunakumbuka kuwa Kigwangalla alikuwa mshindi wa tatu, baada ya Bashe kuenguliwa kwa kigezo cha Uraia. Bashe ni mfanyakazi katika moja ya mashirika ya watuhumiwa nchini. Kugombea kwake kulilenga kuongeza nguvu ndani ya bunge na chama kama sehemu ya mtandao.
Kuondolewa kwake kulikuwa 'technically' na wala haikukusudiwa. Hili lilikuwa kuepusha kashfa kama ingedhihirika vingenevyo.

Lucas Selelii ndiye alikuwa wa pili kwahiyo alipaswa kuchukua nafasi hiyo. Yeye alienguliwa kwasababu alikuwa mwiba mkali ndani ya bunge. Kuenguliwa kwake kulifanyika ndani ya CC iliyokuwa inamilikiwa na wathumiwa wa ufisadi. Ilikuwa ni foul play kubwa sana. Kwanza alichezewa shere na Yusuf Makamba baada ya kugawa jimbo aliporuka kikwazo hicho hakuvuka ndani ya CC.

Kigwangalla akachukuliwa kwasababu ya uhusuiano wake na 'jikoni'. Ni utaratibu huo huo wa kupitia NEC na CC Ulimweka Kigwangalla madarakani kama mbunge ndio utatumika kummaliza. Utatumika kwasababu ya misimamo yake juu ya serikali.
Kwa hili Kigwangalla ni 'victim' na ngazi yake kisiasa inategemea majaliwa zaidi. Kwa bahati mbaya yeye hajielewi na tumesikia kashfa kama za vitumbua na kutishiana. Ukweli ni kuwa anacheza karata ngumu sana.

Deo Filikunjombe naye ni victim kwa misimamo yake ambayo mingi inalenga katika kusimamia kilicho kweli. Sina uhakika wa yeye kugombea popote, ukweli ni kuwa ni lazima aandae makazi ya siku zijazo maana kwa kutokuwa na kundi litalaomtetea ndani ya NEC au CC hatima yake ni maajliwa sana.

Makongoro Nyerere ambaye ni maarufu kwa 'kule site' wanasema mafisadi..... naye ni victim. Tofauti na wenzake yeye ana ngao ya jina kubwa na huenda kumwacha nje ya sytem kunaweza kuzua makubwa. Wamiliki wa CC na NEC kwasasa hapendi arudi katika uongozi, wakati huo huo wapo wanaotaka jina hilo libaki kama heshima kwa Nyerere. Ni kazi nzito kumuengua kwa mizengwe lakini tayari jitihada zinaendelea ili aenguliwe mapema huko Musoma kabla hajafika NEC au CC kukwepa lawama.

Nape Jnr, yupo matatani sana. Kijana huyu aliyekuwa na mtazamo wa kitaifa zaidi aliwahi kukorofishana na kinara wa mtandao mzee EL. Kwa vile umiliki wa NEC na CC ni wa mtandao naye alionja adha kwa kuenguliwa kutoka UVCCM technically. Si kuwa hakuna aliyekuwa anajua umri wake! la hasha, walimkatizia mbele kwa kutumia wingi wao katika vyombo vya maamuzi wakamtupa nje.

Nape aliporejea kama katibu mwenezi alianza kwa ari, nguvu na kasi mpya kwa kuwalenga mafisadi. Jitihada zake zimepigwa break kwasababu maamuzi ni ya CC na NEC na yeye hakuwa na usaidizi wa kutosha katika kufanikisha hili.
Ametuhumiwa kukivuruga chama na kwa kiwewe tu ameacha hoja za kitaifa zilizomjenga na kuishambulia Chadema kwa hoja za hovyo sana. Hili ni baada ya kushindwa kuwashughulikia mafisadi ndani ya chama chake wanaomiliki CC na NEC.
Majuzi NEC ilimtuhumu na kutaka sekretariati ifanyiwe mabadiliko ya kumondoa. Nguvu ya NEC na CC inaonekana

Ni nguvu hiyo inayotaka Wilson Mukama naye aondolewe kwa kushindwa kukiendesha chama. Mukama ndiye aliyetoa mapendekezo ya kuvunjwa kwa sekretariati zote zilizokuwa na wajumbe waliotokana na mafisadi au ushawishi wa mafisadi. Naye ni next victim

Wengine ni akina Mwambalaswa, Mwakyembe kwa uchache tu.
Lipo kundi ambalo litakuwa 'victim of circumstance' na ambalo haliwezi kuathirika moja kwa moja na uamuzi wa NEC au CC, au kuathirika kwao kunaweza kuwa na matatizo katika chama.

Mfano ni Magufuli ambaye kwa kutajwa tajwa kuhusu kuwania urais tayari alishaundiwa zengwe kuwa analeta kero kwa wananchi. Kuna watu kama akina Membe ambao kutajwa tajwa kwao kunaundiwa zengwe kwa vile si rahisi kuwa-deal moja kwa moja kwa kutumia NEC au CC.

Tumemsikia EL akisema wizara ya mambo ya nje ina matatizo huku akiwa amefanya ziara za balozi mbali mbali. EL anajua bajeti ya wizara ni ndogo, pamoja na udogo huo pia wizara haipati mgao stahiki. Maana yake ilikuwa moja kuanza kumchafua Membe kwasababu ni ngumu sana kupitia CC au NEC bila kuwa na ushahidi au zengwe la kutosha.
Lakini wasi wasi mkubwa wa EL ni kuwa CC na NEC inaweza kuja na watu tofauti kwa hiyo ni vema 'udongo ukauwahi ungali maji'.

Nadhani hadi hapa tunaona ni kwanini ni muhimu sana kuwa na nguvu katika chama kuliko serikali. Ubunge ni zao la chama, serikali ni zao la chama na chama ndicho kimeshika hatamu kwa mujibu wa CCM.
Mpambano uliopo wa uchaguzi wa chama si wa kupata viongozi wa kukivusha chama katika nyakati hizi ngumu, ni mkakati wakujipanga kwanza ndani ya vyombo vya CC na NEC ili kuwahangaikia 'waharibifu' kabla ya kuhangaika na wapinzani.

Mgombea wa CCM ajaye hatapatikana kwa merits bali nguvu ndani ya chama hasa CC na NEC.
 
Inaendelea....

Tumesema kuwa NEC na CC ndizo nguzo za chama na kama utazikamata basi utakuwa salama. Vita ndani ya UVCCM, UWT na Wazazi ni vita ya makundi na si ya watu. Kwa mfano, UWT kuna Sofia Simba ambaye ni msemaji mku wa kambi ya mtanadao -mafisadi na Anne Kilango aliye katika kundi la CCM wazee.
Unapokuwa na wajumbe wa NEC muhimu kama hawa utakuwa umefanikiwa sana. Maamuzi yao yataathiri chaguzi zote za ngazi za chini na kuleta wajumbe wengi zaidi ndani ya NEC.

Katika mchakato huu kuna watu ambao ni waathirika wa NEC na CC watake wasitake. Tunakumbuka kuwa Kigwangalla alikuwa mshindi wa tatu, baada ya Bashe kuenguliwa kwa kigezo cha Uraia. Bashe ni mfanyakazi katika moja ya mashirika ya watuhumiwa nchini. Kugombea kwake kulilenga kuongeza nguvu ndani ya bunge na chama kama sehemu ya mtandao.
Kuondolewa kwake kulikuwa 'technically' na wala haikukusudiwa. Hili lilikuwa kuepusha kashfa kama ingedhihirika vingenevyo.

Lucas Selelii ndiye alikuwa wa pili kwahiyo alipaswa kuchukua nafasi hiyo. Yeye alienguliwa kwasababu alikuwa mwiba mkali ndani ya bunge. Kuenguliwa kwake kulifanyika ndani ya CC iliyokuwa inamilikiwa na wathumiwa wa ufisadi. Ilikuwa ni foul play kubwa sana. Kwanza alichezewa shere na Yusuf Makamba baada ya kugawa jimbo aliporuka kikwazo hicho hakuvuka ndani ya CC.

Kigwangalla akachukuliwa kwasababu ya uhusuiano wake na 'jikoni'. Ni utaratibu huo huo wa kupitia NEC na CC Ulimweka Kigwangalla madarakani kama mbunge ndio utatumika kummaliza. Utatumika kwasababu ya misimamo yake juu ya serikali.
Kwa hili Kigwangalla ni 'victim' na ngazi yake kisiasa inategemea majaliwa zaidi. Kwa bahati mbaya yeye hajielewi na tumesikia kashfa kama za vitumbua na kutishiana. Ukweli ni kuwa anacheza karata ngumu sana.

Deo Filikunjombe naye ni victim kwa misimamo yake ambayo mingi inalenga katika kusimamia kilicho kweli. Sina uhakika wa yeye kugombea popote, ukweli ni kuwa ni lazima aandae makazi ya siku zijazo maana kwa kutokuwa na kundi litalaomtetea ndani ya NEC au CC hatima yake ni maajliwa sana.

Makongoro Nyerere ambaye ni maarufu kwa 'kule site' wanasema mafisadi..... naye ni victim. Tofauti na wenzake yeye ana ngao ya jina kubwa na huenda kumwacha nje ya sytem kunaweza kuzua makubwa. Wamiliki wa CC na NEC kwasasa hapendi arudi katika uongozi, wakati huo huo wapo wanaotaka jina hilo libaki kama heshima kwa Nyerere. Ni kazi nzito kumuengua kwa mizengwe lakini tayari jitihada zinaendelea ili aenguliwe mapema huko Musoma kabla hajafika NEC au CC kukwepa lawama.

Nape Jnr, yupo matatani sana. Kijana huyu aliyekuwa na mtazamo wa kitaifa zaidi aliwahi kukorofishana na kinara wa mtandao mzee EL. Kwa vile umiliki wa NEC na CC ni wa mtandao naye alionja adha kwa kuenguliwa kutoka UVCCM technically. Si kuwa hakuna aliyekuwa anajua umri wake! la hasha, walimkatizia mbele kwa kutumia wingi wao katika vyombo vya maamuzi wakamtupa nje.

Nape aliporejea kama katibu mwenezi alianza kwa ari, nguvu na kasi mpya kwa kuwalenga mafisadi. Jitihada zake zimepigwa break kwasababu maamuzi ni ya CC na NEC na yeye hakuwa na usaidizi wa kutosha katika kufanikisha hili.
Ametuhumiwa kukivuruga chama na kwa kiwewe tu ameacha hoja za kitaifa zilizomjenga na kuishambulia Chadema kwa hoja za hovyo sana. Hili ni baada ya kushindwa kuwashughulikia mafisadi ndani ya chama chake wanaomiliki CC na NEC.
Majuzi NEC ilimtuhumu na kutaka sekretariati ifanyiwe mabadiliko ya kumondoa. Nguvu ya NEC na CC inaonekana

Ni nguvu hiyo inayotaka Wilson Mukama naye aondolewe kwa kushindwa kukiendesha chama. Mukama ndiye aliyetoa mapendekezo ya kuvunjwa kwa sekretariati zote zilizokuwa na wajumbe waliotokana na mafisadi au ushawishi wa mafisadi. Naye ni next victim

Wengine ni akina Mwambalaswa, Mwakyembe kwa uchache tu.
Lipo kundi ambalo litakuwa 'victim of circumstance' na ambalo haliwezi kuathirika moja kwa moja na uamuzi wa NEC au CC, au kuathirika kwao kunaweza kuwa na matatizo katika chama.

Mfano ni Magufuli ambaye kwa kutajwa tajwa kuhusu kuwania urais tayari alishaundiwa zengwe kuwa analeta kero kwa wananchi. Kuna watu kama akina Membe ambao kutajwa tajwa kwao kunaundiwa zengwe kwa vile si rahisi kuwa-deal moja kwa moja kwa kutumia NEC au CC.

Tumemsikia EL akisema wizara ya mambo ya nje ina matatizo huku akiwa amefanya ziara za balozi mbali mbali. EL anajua bajeti ya wizara ni ndogo, pamoja na udogo huo pia wizara haipati mgao stahiki. Maana yake ilikuwa moja kuanza kumchafua Membe kwasababu ni ngumu sana kupitia CC au NEC bila kuwa na ushahidi au zengwe la kutosha.
Lakini wasi wasi mkubwa wa EL ni kuwa CC na NEC inaweza kuja na watu tofauti kwa hiyo ni vema 'udongo ukauwahi ungali maji'.

Nadhani hadi hapa tunaona ni kwanini ni muhimu sana kuwa na nguvu katika chama kuliko serikali. Ubunge ni zao la chama, serikali ni zao la chama na chama ndicho kimeshika hatamu kwa mujibu wa CCM.
Mpambano uliopo wa uchaguzi wa chama si wa kupata viongozi wa kukivusha chama katika nyakati hizi ngumu, ni mkakati wakujipanga kwanza ndani ya vyombo vya CC na NEC ili kuwahangaikia 'waharibifu' kabla ya kuhangaika na wapinzani.

Mgombea wa CCM ajaye hatapatikana kwa merits bali nguvu ndani ya chama hasa CC na NEC.

Nimepata picha ya kwa nini watu wanaingia gharama kubwa ya kugombea NEC taifa hata kuvutiana trigger ili mradi apenye ingawa inaeleweka ni nafasi ya kujitolea na wala si ajira.

Kinachonishtua ni kwamba hawa NEC Taifa ndo watoa maamuzi ya mwisho, na kama umefanikiwa kuwashika hao utakuwa umeandaliwa njia nyeupe kupenya kwenye kinyang'anyiro ambacho chama ndicho chenye kutoa maamuzi ya kukufungulia green lights. Kwa mantiki hiyo hawa jamaa wa NEC Taifa ndio Catapila la kusaficha njia, na catapila ili lifanye kazi vizuri ya kusafisha njia huhitaji fuel pamoja na parts kitu ambacho huweza kumgarimu anayetaka kulitumia hilo Catapila. Ukitaka njia yako iwe nzuri zaidi let jembe la kusawazisha udongo, vinginevyo kasi yako haitamfikia ambaye yupo kwenye njia iliyo na milima na mabonde.

CCM ina sera nzuri mno pengine kupita vyama vyote, na ukweli ni kwamba vyama vingine vya upinzani vimejenga sera zao kutoka mhimiliwa CCM na kwamba sera hizo haziko mbali sana na Sera za CCM, walichofanya ni kuchepusha kidogo tu njia ili ionekana wako na tofauti kidogo za kiitikadi ingawa kinachoongelewa ni kitu kile kile.

Napata picha ya kundi fulani ndani ya chama linaloongoza nchi kifisadi lakini kwa sura zao ndio wanaoonekana waadilifu. Vigumu kushika mtoa rusha ngazi za NEC taifa, watakaoshikwa ni dagaa vijijini ambao hawana kinga (ngao). Hiyo ndiyo inayonishangaza kuona kama kilichotokea Moshi sasa hivi Naibu Waziri Mwanri kuenguliwa kugombea NEC kwa vile wanaccm Moshi wamesema yeye Mbunge, Yeye Waziri, na bado anang'ang'ania NEC, kwa nini hawaachiii wenigine wasio na ajira nafasi hizo, kwa nini nafasi zote hizo ajaziwe mmoja tu?

Kuna kitu ambacho hakiko wazi kuhusu mfumo wa utawala wa CCM hasa uongozi wa juu na kuna siri nzito, na kama inapotokea mmoja kutoka ngazi ya juu akitaka kujiengua inatumika nguvu ya ziada sana kumtuliza na kuridhisha asitishe kwani kuna mmoja anaweza kutoa siri hizo.

Siri za maficho ya pesa za Uswiss tangu awamu ya kwanza ni mfumo endelezi ambao mhusika mkuu ni chama cha CCM la sivyo wasingehusika suala hilo lingelikwisha fanyiwa kazi sana tu. Mheshimiwa Rais katika hotuba yake mwishoni mwa mwezi amekwepa kabisa kugusia suala hilo jambo ambalo linashangaza wakati wengi wetu tulitazamia anglitolea kauli kama kiongozi wa Kitaifa aliyeguswa nalo.

Kwa vyo vyote kuna mambo ya kufanyia kazi ambayo CCM imechepuka na hayo kwa kuto yatilia maanani yanazidi kuwachanganya zaidi na kuruhusu mtifuano ulio mgumu kuutuliza wakati source yake wanaijua lakini hawako tayari kugusa huko ila matawi ambayo yameshikiliwa na hiyo source, hakuna kitakachowezekana kama gome linalootesha matawi halikatwi.
 
DURU-MATUKIO (MWANGOS)
Kwanza kabisa tutoe pole kwa Mke, watoto, ndugu na jamaa wa mwandishi Daud Mwangos kwa tukio baya na la kikatili lililotokea Iringa. Mungu ampuzishe kwa amani mwenzetu Mwangos

Kutokana na tukio hilo yapo yanayojitokeza kijamii na kisiasa. Ni tukio ambalo hatuwezi kuliweka kisiasa kwa asili yake na muundo wake, lakini limetokea katika mazingira ya kisiasa na tutalijadili pamoja na machungu tuliyo nayo.

Tutakuwa na mtirirko wa suala hili kwa safu mbili tukiangalia mambo kama
1. Athari zake kisiasa kwa nchi na jamii
2. Mwenendo wake tangu mwanzo hadi mwisho
3. Ushiriki wa vyama vya kisiasa
4. Nafasi ya chadema katika kuungoza umma katika misuko suko kama hii
5. Hatima ya CCM kufuatia matukio ya mauaji


Na kisha majumuisho.
Tutaendelea kuwapa habari kadri inavyowezekana.

Tunarudia tena kutoa mkono wa pole na kumtakia Mwangos mapunziko ya amani huko aliko.

R.I.P D.Mwangos
 
Marehemu Mwangos aliuawa kwa mlipuko baada ya kushambuliwa na askari zaidi ya watano waliokuwa na silaha.
Marehemu ameonekana akianguka akiwa na kamera yake huku mitutu ikimwelekea kichwani.
Picha za kusikitisha zinaonyesha Mwangos alivyoumizwa na kufikia mauti kwa hali ya kinyama na kikatiki.

Maswali rahisi tu ni kuwa ilikuwaje Polisi wakaamua kutumia mabomu kumlipua mtu wanayemfahamu vizuri na ambaye kupatikana kwake kusingehitaji hata fikra.

Ilikuwaje askari zaidi ya watano wakiwa na silaha na tayari wamemdhibiti marehemu wafikie hatua ya kumlipua.
Busara gani zilitumika hadi kufikia mahali pa kusema silaha za moto ndio jibu.
Je, ingetokea nini kama wangemuacha na kumwita au kumtia mbaroni kwa wakati mwingine muafaka.
Mwangos aliwaudhi Polisi kwa jambo gani kiasi cha kulipuliwa n.k.

Maswali yote hayo hayana majibu ya haraka kwa watu wenye dhamana. Si mkuu wa mkoa au kamanda yoyote yule aliyejitokeza japo kuelezea tukio.

'Shujaa' ni msemaji wa jeshi la Polisi ambaye inabidi asamehewe kwani uwezo wake wa kufikiri hauhitaji kujadiliwa kwa kauli kuwa marehemu alitupiwa kitu kutoka kwa raia pembeni alipokuwa natafuta usalama kwa polisi.

Na jama gazeti moja limenukuu Polisi wakiendeleza uongo wa kudai kuna kitu kilitupwa.
Ni ujinga kwasababu wangeona kile kilicho katika mitandao na yale yaliyofichwa kusitiri utu, asingetokea mtu mwenye akili timamamu kutetea upuuzi wa aina hiyo.
Hili linazidi kushadidia hoja za mitaani kuwa jeshi la Polisi ni genge tu la watu waliovaa uniform.

Matukio kama haya yamekuwa yanajirudia na njia ya kijinga imekuwa kuunda tume za kipuuzi kuwapumbaza Watanzania. Wasichokijua ni kuwa dunia inaona.Katika uwanja wa kimataifa tumepoteza thamani yetu ya kukemea maovu.
Leo Kaburu angekuwa bado yupo sijui JK angesimama na kunyooshea kidole kipi.
Ni wapi Tanzania itasimama na kusema ina utawala wa sheria, utawala bora na wa haki.

Dunia inaona haya na tukio la Iringa limeandikwa na vyombo vingi duniani.
Pengine halimuhusu Kikwete kwasababu anamaliza muda wake na rais ajae atarudisha heshima ya nchi kama alivyosema tatizo la TANESCO litashughulikiwa na Rais ajaye.
Anayedhani Rais wetu si mdhaifu basi ajitazame kama amevaa nguo

Wakati jeshi la Polisi likishindwa kusema ukweli dunia nzima imeona unyama huo.
Maelezo yanayotolewa yanazidi kulidhalilisha jeshi ambalo ni chombo muhimu sana katika usalama wa taifa.

Kama tulivyotarajia viongozi wa nchi hii wanatafuta njia za mkato za kulinda ajira zao wala si heshima, utu na ubinadamu wa raia wa taifa hili. Tumeona mkanganyiko wa tume za uchunguzi, mkuu wa polisi akiwa na yake na waziri wa mambo ya ndani yake.

Ni vurugu tu kwasababu viongozi waliopaswa kusimama na kulinda wananchi na mali zao wamejificha.
Rais hajulikani anasema nini wakati huu dunia ikiona uvunjaji wa haki za binadamu wa hali ya juu.
Waziri mkuu mwenye serikali inayotuhumiwa naye hajulikani anasema nini.

Marekani ina watu milioni 300, India milioni 900 na uingereza milioni 60, linapotokea tukio kama hili mkuu wa nchi atasimama kuwaeleza wananchi wake nini kimetokea.
Tanzania yenye watu milioni 40 rais anaona mauaji yanayoendelea ni kitu cha kawaida.

Rais amesahau kiapo na wajibu wake, amesahau thamani za taifa, anaangalia taifa likitumbukia katika machafuko na kupoteza heshima duniani.

Mkuu wa jeshi la Polisi linalotuhumiwa angekaa pembeni ili uchunguzi umsafishe au umtie hatiani.
Waziri wa mambo ya ndani ambaye ameshuhudia mauaji ya kutosha naye alipaswa akae pembeni.

Waziri alipaswa akae pembeni kulinda serikali ya chama chake na boss wake ambao sasa hawana pa kutokea.
Mauaji haya ni mlolongo wa mauaji kama yale ya Igunga, Arusha, Tarime n.k. na haionekani kama serikali imeshtuka na kuchukua hatua za kuyazuia, pengine si makosa kuihusisha kwa namna moja au nyingine.

Mauaji ya Iringa ni ya kisiasa hata kama washiriki si walengwa au wanasiasa.
Ni matokeo ya mvutano wa Polisi na chama cha Chadema kuhusu mikutano.

Jambo la kushangaza ni kuwa kule Iringa kulikuwa na ufunguzi wa ofisi baada ya sensa kuisha, sijui hilo lingeathiri vipi zoezi la sensa. Lakini basi Polisi wenye vifaa wangetumia vifaa vyao kwa uangalifu yasingefika hapa yalipo.

Kwa vile ni mauaji ya kisiasa, hatuwezi kuyatenganisha na serikali au chama tawala.
Hakuna shaka kuwa jeshi linatumia kisiasa kama alivyoonyesha waziri Nchimbi.
Jeshi halipaswi kuchukua ushauri kutoka kwa wanasiasa bali kufanya kazi kwa kutumia sheria, kanuni na tartibu.

Kwa muktadha huo, kukataa kujiuzulu kwa mkuu wa Polisi na Waziri wa mambo ya ndani kunaichafua CCM vilivyo.
Kunamchafua Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM, na inadhihirisha wazi kuwa CCM inaweweseka sana na wimbi la mageuzi.

Zile tetesi za mipango ya kuua viongozi wa upinzani sasa zinaonekana na wananchi kuwa hazina shaka.
Jaribio kama la Mabwepande halina utetezi tena. Chama kinachopteza mvuto kwa kasi hakionekani kujitambua

Badala ya kuwalazimisha viongozi husika kujiuzulu ili kunusuru taswira ya CCM, kumetokea watu wakiongea mambo yasiyokisaidia chama. Mkakati wa kuishambulia CDM kutokana na unyama wa Iringa unaijenga CDM kuliko CCM inavyodhani.

CCM tayari inadoa, sasa anapotokea mtu na kusema marehemu alitumwa na CDM kujilipua, au CDM walikuwa na watu waliomlipua n.k wakati ukweli wa kifo upo wazi unaijenga CDM kwa kile kinachoitwa huruma 'political Sympathy'

Kauli za akina Nape kuhusisha tukio hili na siasa au msajili kuishambulia CDM kunachochea hasira zaidi badala ya kuepusha shari. Walichotakiwa CCM kufanya ni kuonyesha kuwa CCM haikubaliani na unyama ule na njia nyepesi ilikuwa ni watu kuwajibika kwa hiari au lazima.

Kulifanya suala hili la kisiasa kwa kuilenga CDM ni kujimaliza.
Uharibifu umetokea na unaendelea kukimaliza chama.

Baada ya kulitazama suala kimataifa na kichama(CCM),tugeukie upande unaoonekana kuhusika ambao ni Chadema. Tuangalie uongozi wa CDM ulivyoshughulikia matatizo ya nyuma, ilivyosimama katika suala hili, ilipozembea na inakoelekea.

Tutaendelea......

.
 
Inaendelea...
Mashambulizi ya Polisi dhidi ya mikutano ya CDM yameendelea kwa muda mrefu. Kila mara yanapotokea maafa tunasikia pande mbili zimekubaliana abc. Pande hizo ni CDM na Polisi. Hali inajirudia kila mara na kwa mtindo ule ule.
Ikumbukwe kazi ya Polisi si kutoa vibali vya mikutano bali kusimamia usalama.

Inapotokea tafrani au mauaji CDM wamekuwa wakisubiri Polisi watoe taarifa na baada ya hapo mambo yanakwisha.
Tukio la Morogoro ni mfano mzuri, kumbe leo tunajua kuwa Nchimbi hana mamlaka ya kuunda tume na amekiri kuwa anaunda kamati. Kamati ni mkusanyiko wa watu kama zile za harusi kwahiyo haina matokeo yoyote ya maana wala yenye kuthibitika.

Kwa mantiki hiyo tume zote zilizoundwa huko nyuma huenda hazikuwa na mamlaka wala mantiki.
Tunachopaswa kujiuliza ni kuwa, hivi jeshi la Polisi linalotuhumiwa linawezaje kuunda tume ya kujichunguza?
Mfano, Nchimbi na Mwema wanawezaje kuunda tume ili hali wao pia wanatakiwa wachunguzwe? Ni nani anayeweza kumchunguza IGP au waziri wa mambo ya ndani wakiwa madarakani?

Haya yameibuliwa na CDM ambao kumbe wakati wanazikubali tume walijua hazina uhalali wala mantiki.
Jana mkurugezi wa operesheni M4C ametoa taarifa kuelezea nini walichokuwa wanafanya Iringa, haukuwa mkutano bali ufunguzi wa ofisi zao. Wakati hayo yakiendelea CCM walikuwa wanaendelea na mikutano.
Haihitaji elimu kujua kuwa Polisi ni sehemu ya chama na wanatumika hivyo.

Tumemsikia msajili wa vyama akiingia bila mpangilio kuhusu kukifuta CDM hata kama hana ushahidi.
Tumeona matamko ya CCM na jinsi wanavyohusisha tukio la Iringa na CDM.
Ukiliingalia tukio hili na mengine ya nyuma utaona kuhusishwa kwa CDM na matatizo, wala si Polisi na wananchi.

Chadema wanapoita mikutano wanaohudhuria si wana CDM kila mtu ana haki.
Mfano, kifo kilichotokea Morogoro tumeanishwa kuwa kijana Ali alipigwa na kitu kizito.
Hii ni kuonyesha kuwa CDM ni washari kama ilivyozoeleka.
Kwamba CDM imekuwa Bangusilo, kila anayetaka kujisafisha anachukua taulo la CDM.

Katika duru za siasa-mgongano wa mawazo, bandiko la kwanza linazungumzia 'damage contro'. Tumeweka wazi kuwa CDM wanatatizo kubwa sana la kulinda taswira zao.

Kwanza katika tukio zito kama lile uongozi wa taifa wa chama ulipaswa kusimama na kulinda taswira na masilahi ya chama. Ukimsikiliza Kigaila ukaangalia picha zinazoonyesha wanachama wakiwa katika jengo lao ni wazi kabisa CDM walikuwa na uwezo wa kujenga kesi mbele ya wananchi. Ukichanganya na zile za mauaji ilikuwa ni wazi kabisa CDM hawakuwa na tatizo isipokuwa tatizo ni la Polisi.

Nimeshangaa sana kusikia kauli zinatoka kwa viongozi wa ngazi za chini wa CDM katika jambo kama hili.
Kwa vile Dr Slaa alikuwepo kule isingekuwa muafaka kwake kuongelea kuepuka biasness.
Lakini basi yuko wapi Mwenyekiti wa Chama au Naibu katibu mkuu au Makamu Mwenyekiti kulinda taswira ya chama inayohusishwa na mauaji na vurugu?

Suala la Iringa sasa linageuzwa kuwa si la Polisi ni tatizo la Chadema. Mwangos hakuwa anafanya kazi za kisiasa!
Kwa bahati mbaya sana kwa vile CDM hawajui kuzuiza damage sasa wanabeba mzigo usio wahusu.

Ni muhimu kusema kuwa hata mikutano kati ya Dr Slaa na Polisi haikuwa ya lazima na kama ilibidi basi CDM walipaswa kuwa na kitu kinaitwa 'communique' yaani mawasiliano na base yao ya kisiasa. Chakushangaza utasikia Dr Slaa amesema abc mitandaoni au kwenye mikutano. Kuna tatizo gani kuitisha mkutano na vyombo vya habari kueleza nini kimefikiwa?

Lakini pia CDM lazima wawe na strategy. Wao wanajua kuwa Polisi ni tawi la chama kwahiyo wanapaswa kucheza nao vema. Ni lazima waangalie mazingira na nyakati ili kupanga taratibu zao kwa ufanisi kabisa.

Kwa upande wa kisiasa, kwa mtazamo nilio nao CDM hawakuonyesha uongozi katika nyakati za majaribio.
Kuna tatizo ndani ya chama lakini halisemwi. Matokeo yake ni haya ya Chama kutokuwa na viongozi hata pale kinapohujumiwa.

Mwenyekiti Mbowe, Said Arif na Zitto kwa hili muwajibike. Sauti zenu si sawa na za Heche au Kigaila, sauti zenu zina nguvu, mamlaka na kinga. Kutojitokeza kwenu na kuacha CDM ikichafuliwa ni ukosefu wa uongozi! (leadership).
Ni kutengeneza ombwe la uongozi lile lile mnalolisema kuhusu CCM na serikali yake.

Na mwisho, je, waandishi wa habari nao wanaudhaifu gani katika matukio kama haya!

Itaendelea....
 
Inaendelea..
Waandishi wa habari wamekuwa waathirika wakubwa wa matukio ya polisi.
Hili la Marehem Mwangos limepita mpaka, na huo ndio ulikuwa wakati mwafaka kuonyesha kuwa fani yao ni mhimili wa nne
wa dola.

Kuna mambo yamejitokeza kuhusu suala hili.
1. Kususia habari za Polisi kwa ujumla wake.
2. kushiriki katika tume au kamati

Kwanza niseme tu kuwa umoja huo wa kususia habari hauwezekani. Hauwezekani kwasababu katika soko huria wapo wanaotegemea habari kama sehemu yao ya maisha. Tumeona wengine wakijitokeza kueleza wazi kuwa wao hawatashiriki.

Pili, kwa kutambua kuwa suala hili limefanywa pengine kwa maelezo kama yale ya kufungia gazeti la mwanahalisi,waandishi hawakupaswa kushiriki katika tume au kamati yoyote inayoundwa na wale wanaowatuhumu.

Njia muafaka ilikuwa ni kushinikiza kwanza wanaowajibika ambao ni IGP na Waziri wa mambo ya ndani wakae pembeni.
Kitendo cha kushiriki hakikuwa sahihi kwasababu huo tu ulikuwa ushirikiano na wizara ile ile waliyogomea kuandika habari zake.

Tatu, waandishi wa habari wenye weledi wa siasa za nchi, wanafahamu kuwa nia ya serikali na CCM siku zote ni kunyamazisha na kuzima mijadala inayolihusu taifa. Wamefanya hivyo bungeni, serikalini n.k.

Tukio la Iringa lina mshindo wa chuki kwa CCM na serikali yake. Kwa kutumia mbinu zile zile za kunyamazisha mijadala tumesikia kuwa askari walioonekana eneo la tukio wanashikiliwa na Polisi na Jumatatu watafikishwa mahakamani.

Hadi hapo mada ya Mwangos na waandishi itakuwa imefika tamati. Itachukua miaka 5 kuchunguza na wakati huo kila kitu kitakuwa kimeshaulika kabisa. ''Askari hawana makosa lilikuwa kosa la marehemu hukumu itasomwa na kuhitimisha''

Waandishi hawana sababu ya kususia shughuli za wizara ya mambo ya ndani kwasababu hilo ndilo CCM na serikali yake walikuwa wanalihitaji. Walilitaka ili kuzuia uharibifu unaotokana na mijadala.

Waandishi walitakiwa kuandika habari zaidi na kuanika ukweli wa tukio ili kila awaye afahamu udhalimu huu.
Walichokifanya ni akunyimaye kunde kakupunguzia mashuzi. Hawakupaswa kususia wala kutoa ushirikiano katika kamati.

HITIMISHO
Tukio hili kwa ujumla imechafua sana taswira ya nchi mbele ya uso wa dunia.
Kwa waziri na IGP kugoma kujiuzulu, wamemchafua bosi wao,CCM na serikali yake.

CCM haikupaswa kulifanya jambo hili kama tatizo linalotokana na CDM.
Njia bora ilikuwa kujisafisha kwa kuwawajibisha IGP na Nchimbi.
Kuishambulia CDM ni kuendeleza chuki dhidi yao kwani wananchi wa Tanzania ya leo hawazugwi na mazungumzo baada ya habari au maoni ya gazeti la uhuru.

Chadema, wameshindwa kuzuia uharibifu usiotokana nao, na badala yake wamekaa kimya chama chao kikihusishwa na mauaji ya Iringa. Hakuna damage control wala uongozi uliojipanga.
Ni wazi chama ambacho tumesema hakijajengwa kama taasisi sasa kinaonyesha ufa.

Haiwezekani tukio kubwa kama hili linaongelewa na mratibu wa mikutano ya CDM.
Hili lilikuwa la Uongozi wa juu wa chama na hakuna anayeona athari hadi suala kugeuzwa kuwa si mauaji ya Polisi ni mikutano ya CDM na mauaji. Nadiriki kusema kwa hili hakukuwa na leadership

Waandishi wameshindwa kutumia maarifa kukabiliana na uonevu huu. Kinyume chake wametoa ushirikiano usio wa lazima kwa wale wale wanaowatuhumu. Theophil Makunga anapaswa ajitoe katika kamati ya Nchimbi isiyo na nguvu za kisheria.

Wakati wakijitoa, hawapaswi kususia habari za 'mbaya' wao kwani kufanya hivyo ni kumpa nafasi aliyotaraji.
Nani ataandika habari za Mwangos au washiriki walioona tukio?

Kama hakuna, ukweli utapatikanaje kama si kuendelea kuandika !!
Walichofanya waandishi ni kuisadia serikali isiende mahakamani kuzuia jambo hili kwa staili yao.
Waandishi wametoa ushirikiano bila kutaraji kwa kususia kusiko na maana.

Tusemezane.
 
MASHARIKI YA KATI (LIBYA NA MISRI)
Katika duru za siasa wiki hii tuangalie lile shambulio lililoua wana wa ubalozi wa Marekani kule Benghazi Libya.
Tukio hilo limekwenda samba samba na shambulio katika ubalozi wa Marekani kule Misri.

Moja ya sababu za mashaumbulizi hayo ni ile filam inayotarajiwa kutolewa ikiukashfu Uislam.
Kule Libya shambulio hilo linaonekana kama kukumbushia tukio la Sept 11.
Hadi sasa bado haijaeleweka wazi nini chagizo (motives) ya mashambulio hayo kwa uhalisia.

Wapo wanaodai kuwa filam ni sababu tu ya kuonyesha hasira za jambo lililojificha nyuma.
Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanasema mikutano mikuu ya vyama vya siasa vya Democrat na Republican hasa kuonyesha wazi kuitetea Israel vimeamsha hisia kwa makundi yenye siasa kali.

Na inasemekana pia kile kitendo cha vyombo vya habari kuonyesha kifo cha Osama vinaweza kuwa vinachangia.
Ni wiki hii mmoja wa askari waliomuua Osama alitoa kitabu 'No easy day' na ameonekana akihojiwa katika kipindi cha '60 minutes' jinsi walivyotekeleza mpango huo.

Katika safu ya duru za siasa, huko nyuma tumeeleza utata katika mashariki ya kati.
Tumeeleza jinsi gani Misri ilivyo na ushawishi katika siasa za mashariki ya kati hadi kuitwa 'mama wa dunia' kule uarabuni.
Tulisema kuwa Marekani ilipigana kwa kila namna kuhakikisha kuwa washirika wao kama Mubarak au awaye wanabaki katika madaraka. Hilo halikuwezekana kwa nguvu za umma na hakika matokeo yake yanaanza kujidhihiri.

Kushika madaraka kwa Muslim Brotherhood hakukuwa na athari Misri bali mashariki ya kati yote. Tulisema kuwa ingawa wanaonekana moderate ukweli ni kuwa wao ndio wana injinia mambo mengi ya mashariki ya kati.
Ni mapema mno kuzihusisha vurugu hizi na wao lakini pia si rahisi kuwaondoa katika kundi la washukiwa.
Wao wameto tamko kuwa aliyeandaa filam hiyo aweke rumande.

Wakati hayo yakiendelea, kumekuwa na vugu vugu la mapambano kati ya Iran na Israel. Ni wazi kuwa Israel inataka kuishambulia Iran. Kitu kimoja kinachowakwaza ni ukweli kuwa bila ya Marekani hali inaweza kuwa ngumu kwao kama ilivyokuwa kama kule kule kwa Hassan Nasrallah.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Ayatollah Khameneni ameunga mkono matamshi ya uchokozi 'provocative' juu ya Israel.
Kinaschowashangaza wengi ni jinsi Iran inavyojiamini.
Hata hiyo vikwazo vinabaki kuwa tatizo kwani vinaendelea kuiumiza Iran.

Kwa wakati huu Marekani haingependa kuingia katika vita. Wakati Republican wakionekana kuiunga mkono Israel kuingia vitani, Obama hataki hilo litokee. Kinachofanywa hapa ni mchezo wa kisiasa ili Republican baadaye wageuke na kusema hivi ni vita vya Obama.

Cha muhimu zaidi ni kutafuta kuungwa mkono na Jews ambao wana umiliki na ushawishi mkubwa wa habari katika siasa za Marekani.
Hili linaendelea kuleta mvutano kati ya Netanyahu na Obama.

Turaendela kuwajuza kile kinachojiri
 
DUNIANI WKI HII

Marekani:
Baada ya mikutano mikuu ya vyama vya kisiasa , chama cha Democrat kimeonekana kuwa na hamasa zaidi kuliko wapinzani wao. Kura za maoni zinamweka Obama mbele ya mpinzani wake Mitt Romney.
Hata hivyo katika kura za maoni zilizotangazwa leo tofauti baina yao ni point moja.
Kura hizi huendeshwa na taasisi mbali mbali mbali na hubadilika kila mara kutegemeana na matukio.

Wiki hii mgombea wa Republican Mitt Romney alinukuliwa kwa siri akisema asilimia 47 ya wamarekani ambao ni wapiga kura wa Obama wanategemea 'handout' yaani kuishi kwa utegemezi wa serikali kama vile social welfare na unemployment insurance. Kauli hii imeleta mtafaruku na waliberali wameshadidia kuwa hilo lilikuwa tusi kwa wazee na wale wengine wanaopata msaada kwa makosa yasiyotokana na wao.

Mwezi huu haukuwa mzuri kwa Obama pia kwasababu idadi ya ajira zilizotengenezwa ni chini ya kiwango kilichotarajiwa.
Mashambulizi ya balozi za Egypt na Libya nayo yamewapa nguvu wahafidhina(Republican) ambao siku zote wamejivunia rekodi ya usalama wa taifa. Baada ya kifo cha Osama, kumalizwa kwa vita Iraq na hatua za kujitoa Afghan kuonyesha japo mweleko Republican hawana la kusema tena na wamebaki kudandia hoja dhaifu.

Mdahalo wa tarehe 3 mwezi ujao utatoa mwanga zaidi wa mchuano miongoni mwao.
Kitu kimoja kinachomkabili Mitt Romney ni kule kutopendwa tu, anaonekana kama mtu jeuri hata miongoni mwa wahafidhina wenzake. Hili nalo linamuumiza kwasababu katika uchaguzi kuna idadi kubwa inachagua kwa mtazamo tu na si sera na katika ufungamano wa karibu hao wanaweza kuamua nani mshindi.

Mashariki ya kati: Baada ya mashambulizi ya balozi hatimaye hali imetulia japo ni kwa muda.
Kitu kinachoshangaza wengi ni ile hali ya rais Morsi kutokusema jambo lolote hata pale balozi za marekani ziliposhambuliwa nchini mwake.Brotherhood wanaweza wasionyeshe makucha sasa hivi lakini ni suala la muda.

Somalia:
Kumefanyika uchaguzi ulio mwondoa rais Ahmed. Chaguzi za Somalia ni za aina yake kwasababu Rais anatawala sehemu ya Mogadishu na zilizo baki kama Bosaso n.k zinawatawala wake achilia mbali Alshabaab.
Kwa mtazamo wa haraka uchaguzi huu ni symbolic kwasababu impact yake katika kuleta suluhu ya kudumu ni ndogo sana.

Tatizo linaloikabili serikali ya Somalia ni pamoja na kuwa na viongozi masilahi. Uchaguzi na pesa zote za serikali huishia kulipa wabunge wengi sana kutoka karibu kila kona na kila ukoo.
Kwahiyo impact ya misaada kwa wasomali ni kama hakuna na wanachi wanajiuliza serikali hii ni ya nini, kwanani na kwa faida ya nani.Hali bado ni mbaya na hakuna dalili za kuimarika katika siku za karibuni.

Tanzani:
Baada ya tukio la kuuwa kwa mwandishi hali imetulia kiasi. Tukio lile kwa mara nyingine limeonyesha jinsi serikali ilivyo na mkono katika masuala tata. Taarifa za Polisi zimebainika ni za uongo, tume ya waziri wa mambo ya ndani haina tija. Kilichoudhi zaidi ni kulindana kwasababu uzito wa tukio lile ulipaswa kuandamana na mlolongo wa watu kupoteza kazi na kushtakiwa.

Chuki dhidi ya hayo inajionyesha wazi hadi kufikia waziri mkuu kuzomewa kule Mwanza.
Matukio kama haya si kuwa yanadhoofisha Upinzani bali yanaupa upinzani nguvu bila kutumia nguvu.
Ni ngumu kutengenisha CCM, Serikali na Polisi na sasa tunaona jinsi hasira za wananchi zinavyotamalaki.

Midhali imeanza hiyo basi tutarajie viongozi zaidi kuzomewa. Hii ni sehemu ya wananchi kuonyesha kutoridhika na hali ya kisiasa. kiuchumi na kijamii nchini.

Tutarajie makubwa zaidi inatosha tu kusema CCM imejiweka katika wakati mgumu hasa kutokana na matumizi ya hovyo ya vyombo vya dola, ufujaji na ubadhirifu. Hakuna kitu ambacho CCM inaweza kusimama na kujinadi nacho. Baada ya uchaguzi wa chama mwezi October kutatokea ufa mkubwa sana na huenda ukawa ndio mwanzo wa mwisho.

Madaktari:
Tukio lingine ni la Madaktari walio mafunzoni kujitokeza na kuiomba radhi serikali kwa kushiriki mgomo.
Tukio hilo limefuatiwa na chama cha madaktari nchini MAT kutoa tamko la kukanusha kuhusu madai hayo.

Madaktari wa 'intern' wana uasajili wa muda na hawajapata usajili wa kudumu hadi wanapomaliza mafunzo yao ya chini ya usimamizi 'internship'. Na hakika ni wao walianzisha mgomo na kuungwa mkono na wakubwa wao kikazi 'seniors' kama registrar, specialists na maprofesa. Walichokuwa wanakigomea ni masilahi duni lakini pia huduma za chini kwa jamii.

Baada ya wao kufukuzwa, mgomo umeendelea kichini chini na hata juhudi za kutaka warudishwe zilikuwa zinaendelea.
Kwa bahati mbaya au nzuri kutegemea uko upande gani, miongoni mwao inaonekana wameghilibiwa na kurubuniwa ili kuleta usaliti. Ni usaliti kwasababu kunawatu wameumia, wamepoteza na wengine kunusurika vifo kwa kile walichokiamini ni sahihi.

Hakuna ubaya wa madaktari kudai masilahi mazuri kwasababu hata wabunge wanadai na kwa njia ya siri serikali ile ile iliyosema haina pesa imewaongezea wao. Hakuna ubaya kudai mazingira mazuri ya kazi ikiwa ni pamoja na vitendea kazi na hali za usalama wa wagonjwa wawapo chini ya uangalizi na matibabu.
Kwa hali yoyote kulikuwa na usaliti wa hali juu kutoka kwa vijana hawa.

Hawa ndio vijana tunaoaminishwa kuwa wanapaswa wapewe uongozi wa nchi.
Ni hao hao walifanya mgomo eti leo wanaomba radhi. Haijulikani ni radhi kwa kosa gani.
Kitu kibaya zaidi ni kuwa baada ya internship wataingia katika soko la ajira na kupambana na ukweli wa maisha.
Kwa vyovyote viwango vyao vya masilahi vitakuwa ni vya chini kuliko wenzao ambao ni wazoefu wa siku nyingi.

Wanachokifanya hapa ni kuruka majivu ili waende wakakanyage moto.
Jamii haitawaelewa leo na kesho watakaporudi kudai masilahi bora kwani sasa wameshajifunga kitanzi cha kutoshiriki mgomo tena.

Inawezekana si wote lakini kitendo cha kuunga mkono hao waliojitokeza ni ishara ya kukubaliana nao.
Hao wachache waliohongwa wataishi maisha mazuri kwa muda fulani lakini kundi kubwa litabaki katika dhiki.
Huko mitaani hakutakuwa tena na ushirikiano na kwa hili wao wameamua kuiua sekta ya afya kabisa.
Wamekata mti walioukalia.

Duru-matukio
 
MATUKIO NCHINI

Waziri Mkuu:
Mheshimiwa Waziri mkuu amekiri kuwa alizomewa kule mjini Mwanza na kwamba hiyo haikuwa ishara nzuri.
Waziri mkuu amelalamika kuhusu viongozi wasiofikia wananchi kama chanzo cha tatizo.
Ukweli ni kuwa wananchi wa Tanzania sasa wamefikia hatua ya kusema liwalo na liwe.
Muda mwingi viongozi wamekuwa wakiwadanganya ima kwa ahadi au matukio na kuwafanya wajinga.

Tumeshuhudia wizi wa kutisha unaofanywa na viongozi katika ngazi ya taifa.
Ni wizi wa kutisha sana kwasababu mabilioni yanayoporwa ni kodi za hao wanaolala kwa dola moja kwa siku.

Hkuna hatua zozote za kinidhamu au kisheria zinazochukuliwa dhidi yao. Mathalani, waziri mkuu amekalia na kutumia nguvu zake zote kulificha suala la Kagoda kwa hadithi zisizo na maana.
Mtu kama huyo atasimama mbele ya umma kuuambia nini ikiwa ameshapoteza uhalali wa kiroho.

Kumetokea mlolongo wa mauji ya kisiasa yasiyo na maelezo, hali ya usalama wa nchi si nzuri kama watu wanavyoaminishwa. Tuhuma za kuuana sasa ni jambo la kawaida, makundi yanayohasimiana yanawindana kwa sumu.
Wenye dhamana ya kulinda amani nao sasa wamekuwa tawi la chama hata kuitwa Policcm.
Hii tu si ishara njema na ni dalili za watu kukosa imani na uongozi na vyombo vya dola.

Tukio la kuzomewa PM si la kwanza, historia inaonyesha kuwa wananchi wa Mbeya waliwahai kumpopoa kiongozi mmoja wa nchi kama maembe.

Licha ya tukio la kutisha la Iringa, wananchi wakiwa na Polisi na FFU karibu yao hawajali kumzomea waziri mkuu. Hawatishiki kutolewa utumbo wala kulala jela. Wamefikia hatua 'defiant' kwa kiwango cha hali ya juu sana.
Kama alivyosema Pinda endapo yeye amezomewa basi hali ni mbaya sana. Na ukweli ndio huo.

Ukweli huo hautashia hapo bali ni mwiba mchungu sana kwa CCM. Imefika mahali watu wanaweza kumuani hata mwendawazimu kuongoza nchi ilimradi tu isiwe ni CCM. Watu hawachukii jina la CCM wanachukia uongozi wa CCM na hawa ni pamoja na wanachama wa CCM. Kwa maneno mengine CCM imepoteza political base kabisa.
Kwa hali ilivyo leo basi JK atastaafu na CCM na hiyo ndiyo itabaki kuwa legacy yake maisha mwake.
Wapinzani wakachinga karata zao vema njia ni nyeupe, hilo kama litatokea au la ni suala la muda!

Mnadhimu wa Jeshi:
Wiki hii mnadhimu mkuu wa jeshi 'chief of the staff' Lt General A. Shimbo amestaafu kwa mujibu wa sheria.
Ikumbukwe kuwa hata alipoteuliwa muda wake ilibidi uongezwe.
Katika hali ya kawaida Rais hustaafu na mkuu wa majeshi na mnadhimu wake mkuu.
Hii si sheria au kanuni bali taratibu ili Rais aingiaye madarakani achague safu yake ya ulinzi wa nchi.
Utaratibu huu umeanza katika miaka ya 80 baada ya Mwinyi kuwa Rais.

Mwaka jana Shimbo alikabiliwa na tuhuma nzito sana za ubadhirifu wa mabilioni aliyoyaficha nje ya nchi.
Ingawa tuhuma zile zilisemekana kuwa si za kweli lakini ukweli unabaki pale pale hazikukanushwa kikamilifu.
Tulisikia habari zile zile za vyombo vya habari kutaka kulichonganisha jeshi na wananchi.
Hakuna kiongozi wa jeshi wala wa nchi aliyesimama na kuzikanusha, na hakika utakuwa ni wendawazimu kama tutadhani hazikuwa za kweli.

Halikuwa jambo rahisi hasa viongozi wa nchi masikini kumwachisha kazi mnadhimu wa jeshi.
Katika nchi kama Nigeria hili liliwezekana lakini si nchi kama yetu. Hawa ni watu wanaoogopwa sana na viongozi wa nchi.

Kustaafu kwakwe ni njia laini ya kumwajibisha mwaka mmoja baada ya tukio la tuhuma za wizi wa mabilioni.
Serikali inadhani kufanya hivyo wnanchi watakuwa wamesahau na pia itampa Shimbo fursa ya kupata mafao yake yote kama mnadhimu mstaafu.

Kama aliweza ongezewa muda huko nyuma hili halikuwa ni tatizo, ukweli wa mambo ni kuwa Rais amemwajibisha kiutu uzima na kwa kulindana.

Ni mambo kama hayo yanayochochea hasira za wananchi. kwamba sheria zimeandikwa kwa kundi fulani la jamii na kundi jingine limepewa 'pass' hata kama linavunja sheria. Tutashuhudia upopoaji wa viongozi hadi pale tutakapokuwa na mabadiliko ya kweli.

Maandamano:
Tumeona maandamano ya kulaani filamu inayokashifu dini. Kwa wale walioiona hiyo trailer hakika ni kashfa na wala halina ubishi. Nchi za magharibi zimetetea kuwa huo ni uhuru wa habari 'freedom of speech'.
Wasichokisema ni kuwa hiyo freedom of speech hata kwao ina mipaka.
Sijui ni nani anawezatoa filam inayomkashifu Malkia achilia mbali dini.
Kama ipo freedom of specch kwanini Juian Asange wa Wiki leak anatafutwa akamatwe?

Kwa vigezo vyote hakuna freedom of speech isiyo na mipaka. Ukiwa nchi za magharibi na kuwasema wayahudi vibaya hiyo inaitwa 'anti-semitism', ukitumia logo ya Hitler kama alivyofanya Prince Harry hilo ni kosa, sasa kwanini kutusi imani iwe freedom of speech?

Kuhojia dini zozote sio tatizo ili mradi tu kufanya hivyo ni kwa njia za kiustaarabu. Wapo mapadri, maasko kama yule wa Zambia au marehemu Moon ambao si tu wamehoji dini zao bali pia wamezipinga.
Wapo masheikh wanaotofautiana kimisimamo ndiyo maana kuna madhehebu kama Shia, Sunni, Ibadhi, Kadiaan, Wahabia, sufi n.k. Ndivyo pia yalipotoka madhehebu kama Roman Catholic, Seventh day, Lutheran n.k.
Hoja ni kuwa je lugha na maudhui yaliyotumika yalikuwa katika muktadha wa freedom of speech au yalikuwa freedom of spit!

Mtu aliyetengeneza filam hiyo ambayo ilitengenezwa kwanza kama 'desert warrior' ni mtu binafsi tena asiye na asili na Marekani. Filam zote hutengenezwa na mashirika au makampuni binafsi bila kuihusisha serikali ya Marekani kama ilivyo hapa kwetu na Bongomovie.

Hata hivyo kwa kuelewa unyeti wa suala zima mtu huyo amekamatwa pengine kupunguza hasira za waandamanaji mamilioni mashariki ya kati na kwingineko.

Hapa nchini Waislam wamekusanyika pia katika kulaani tukio hilo. Mkusanyiko wa kuonyesha hisia siyo tatizo katika jamii inayokubaliana kwa kuishi kwa uvumilivu na ni haki ya kila mtu ilimradi hakuna uvunjaji wa sheria au amani.
Tatizo limejitokeza katika mkusanyiko huo ambalo sijui kama linapeleka ujumbe uliokusudiwa.
Sijui kama kweli ujumbe uliokusudiwa hautatafsiriwa tofauti na kuleta maana tofauti.

Hebu tuangalie kwa uchache mapungufu yaliyojitokeza katika mkutano wa kidongo chekundu..

Itaendelea....
 
Inaendela.......
Mkusanyiko wa kidongo chekundu ulikuwa ni baada ya swala ya Ijumaa. Imekuwa ni taratibu kuitumia siku hiyo katika maandamano pengine kwan kuzangitia kuwa wengi huifanya kama sehemu ya mapunziko.

Hakukuwa na taarifa kuhusu mkusanyiko huo hadi pale ulipotokea. Katika masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na kutoa tamko kama waislam. Hapa ndipo ninaona kuna tatizo. Kwanini watu wa misikiti miwili au mitatu wajivike kofia ya kuwa wasemaji wa Waislam? Je, lini na wapi waliwasiliana kuhusu tamko hilo, na je, waislam wa sehemu nyingine huko mikoani walishirikishwa vipi kutoa tamko?

Moja ya matamko ni lile linalosema serikali ya Tanzania ivunje uhusiano na Marekani na kufunga ubalozi. Kinachonishangaza hapa ni kuwa serikali ya Marekani imeshatoa kauli za kulaani kitendo hicho.
Na wala kitendo cha kuwa na filamu si cha serikali ya Marekani. Hivi Bongomovie wakitengeneza filam inayohusu jambo la kuudhi Watu wa mgharibi hiyo inatosha kuvunja uhusiano na Tanzania.
Kuna wakati Waislam wa Tanzania waliandamana kupinga vita ya Iraq, hatukuwahi kusikia serikali ya Tanzania ikihusihwa na tukio hilo. Ninachotaka kusema hapa ni kuwa hilo linalopaswa kuangaliwa kwa mapana na si kuatfuta mchawi.

Katika Mabango ya waandamanaji yaliyoandaliwa kwa mpangilio, yanasomeka maneno ..... Marekani na Israel.
Hapa Israel imeingiaje wakati filam hiyo haina uhusiano wa aina yoyote na Israel?

Katika mkutano, zikarejewa kauli za kumuondoa Ndalichako na Mufti Simba. Labda hili la mufti Simba ndilo linatisha kwasababu naye kama sheikh Ponda anawafuasi Waislam wengi tu.
Sasa ni Waislam wapi Ponda aliosema wametoa tamko na wala si lile la mufti Simba?

Kinachoshangaza zaidi ni suala la Ndalichako kuingia katika ajenda ya kulaani filam. Nadhani masuala haya hayafanani na kama ni kuyashughulikia yalipaswa kuwa na muda wake na kwa namna zake.

Kilichojitokeza ni kuwa Waislam wana manung'uniko zaidi ya filam na hivyo wanatumia filam kama sehemu tu ya kutaka kukusanyika. Kuwa na manung'uniko ni jambo la kibinadamu kama hajaridhika, lakini kwa mwendo huu wa mpangilio wa vurugu, ni nadra sana kwa mtu mwingine kuelewa wanasimamia nini hasa.
Nilidhani tukio la juzi lingetumika kwa makusudio tarajiwa na si kuwa na mseto wa mambo.

Lazima pia wakati wanatoa matamko wahakikishe yanabeba ujumbe ambao mlengwa atautafakari kwa kina.
Kusema serikali ifunge ubalozi ni kitu wanafahamu hakiwezekani, sijui kwanini waliweka kitu hicho.
Labda hiyo ilikuwa fursa ya kufikisha ujumbe mwingine mzito kuliko ule ambao ni dhahiri haukuwa na nguvu.

Wakati mtu anajiandaa kufanya maandamano ni lazima ajidhirishie pasi na shaka kuwa anaelewa kwanini anaandamana.
Sina uhakika ni asilimia ngapi walioona hiyo filam. Ni jambo la hatari sana kuingia katika mjadala pengine mtu asioujua kiini chake. Haitoshi tu kusikia fulani katusiwa inapaswa uelewe dhalili ya tusi ili ujiwezeshe katika maamuzi.
Sidhani kusikia ni njia muafaka na pengine hiyo ndiyo imekuwa sababu ya kutoka nje ya mada na kuongelea akina Ndalichako na Mufti.

Nimalizie kwa kusema, mikutano au maandamano na yafanywe kwa njia za amani bila hamaki au taharuki. Jamii inawajibu wa kuelewa kwanini kuna mkutano au maandamano na matarajio yake ni nini. Ni vema kukawa na viongozi wanaofahamu taratibu za kuandaa vitu kama hivi ikiwa ni pamoja na matamko. Kazi hiyo isiachwe mikononi mwa watu maarufu bali ifanywe na watu wenye weledi.

Kinyume chake jamii haitawaelewa wanaofanya maandamano au mikutano. Jamii itachanganyikiwa kama ilivyo sasa.
Imechanganyikiwa kwasababu ya kushindwa kuunganisha mambo kadha wa kadha.

Je maandamano yalikuwa ya kulaani filam na kutafuta njia za kuzuia jambo hilo lisilete sintofaham katika jamii?
Je kuna chuki tu dhidi ya Marekani hata kama jambo hilo lipo katika kiwango cha mtu binafsi?
Je, kuna chuki na Israel ambayo kwa namna yoyote ile haihusiani na filam hiyo!
Je, Kuna hasira dhidi ya Ndalichako na Mufti iliyokuwa inatafutiwa sababu na eneo la mkutano
Je, Watu wanaposema hili ni tamko la Waislam wana maana Dar es salaama na kariakoo ndio Waislam Watanzania?

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3 kuna bandiko mwanajamvi mmoja aliomba kufahamishwa CV ya Sheikh Ponda lakini kwa mshangao wa wengi thread ilifikia post #70 bila majibu ya maana ikabidi mods waifunge.Kuna thread nyingine iliulizia mwenyekiti wa taasisi anayoiongoza Sheikh Ponda maana yeye ni katibu pia nayo ilikosa majibu.

Sheikh Mkuu Simba alinukuliwa na vyombo vya habari akimtuhumu Sheikh Ponda hajui hata kusoma Quran,hana elimu dunia wala elimu ahera.Makombora ya Sheikh Mkuu Simba hayakujibiwa ipasavyo na Sheikh Ponda alipoulizwa na wanahabari sana sana aliendelea na msimamo wake wa kutaka kumng'oa Sheikh Mkuu na Dr Ndalichako.

Nimejaribu kutafakari maandamano ya waIslamu ya kulaani Marekani na kuitumbukiza Israel na wakati huo huo Dr Ndalichako nimeanza kuamini uenda kauli ya Sheikh Mkuu ina ukweli kiasi fulani.
 
Last edited by a moderator:
KUHESHIMU UHURU WA MAWAZO
Mkuu Ngongo, kwa hakika sijawahi kuiona CV ya Ponda, ninachofahamu ni kuwa yeye ni mzaliwa wa Kigoma.
Hata hivyo inasemekana ana asili ya Burundi na kuna wakati alituhumiwa kwa hilo.

Labda tu kwa ufahamu wangu, Burundi sehemu kubwa na dini nyinginezo kama Ukristo na zile za asili.
Kuna kitongoji kinaitwa Buyenze, hicho kipo Bujumbura na kina waislam wengi karibu aslimia 99.
Hapo huwa kuna wasomi wa dini wengi na wengine hujifunza na kisha kujiendeleza.

Mimi ninaamini sana katika uhuru wa kujieleza na kueleza kile kinachomsibu mtu iwe kwa furaha au kwa manung'uniko.
Kuandamana sioni kama ni tatizo kubwa kwasababu kila jamii ina haki hiyo.
Tatizo ninalo liona ni je maandamano yanafikisha ujumbe uliokusudiwa?

Ni rahisi sana mtu kushindwa hoja zake pale anapochanganya mambo.Ni ngumu pia kueleweka katika jamii.
Na nirahisi sana kwa asiyeipenda hoja husika kutumia mwanya wa udhaifu kuigeuza hoja halisi na pengine kuipunguza nguvu.

Katika miaka ya 90 akina James Mbatia wakiwa chuo kikuu hawakuwa wanaridhishwa na mwenendo wa serikali. Nakumbuka moja ya madai yao ilihusu dampo la Tabata na afya za wananchi. Hakika waliungwa mkono sana, lakini walipoingiza ile hoja ya OMO(Operesheni Mwinyi out) ni wakati huo serikali ikatumia udhaifu kuonyesha kuwa wametumwa.
Madai yao ya msingi yakafutika kabisa na hoja ikawa jaribio la kumg'oa Mwinyi.

Dhima ya maandamano ya akina Ponda ilikuwa kulaani filamu, filamu ambayo hakika imejaa kashfa na kila mpenda amani anapaswa kuilani. Ni filam isiyoleta utengamano zaidi ya kujenga chuki miongoni mwa wanadamu.
Walipoingiza hoja za mufuti, Ndalichako na Israel kila aliyedhani suala hili lilikuwa na msingi wa manung'uniko alisita na kujiuliza hivi hoja ilikuwa nini? Mbona kunatumika mlango wa nyuma kuonyesha chuki tofauti na ilivyokusudiwa?
Ni hapo akina Ponda wanapoteza hoja hata kama hoja ilikuwa na mantiki.

Kitu kimoja ambacho wengi hawakioni kwa urahisi ni kuwa Ponda ni katibu wa shura ya maimam. Nadhani ni maimam wa Dar es Salaam lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa ni katibu. Mwenyekiti wa shura hajulikani kama mwenyekiti balia Amir wa shura ambaye ni Musa Kundecha. Kwa ufupi ni kuwa Ponda ni katibu wa shura ya maimam.
Hata hivyo kuna wadhifa wa katibu wa kamati ya kusimamia haki za waislam. Katika hali kama hiyo nachelea kusema si rahisi kujua ukatibu wake umeegemea wapi hasa!

Ponda si mratibu wa shughuli, ni kutokana na ushawishi wake anaonekana kuwa mstari wa mbele na pengine kudhaniwa ni kiongozi. Ni kama anavyoalikwa Zanzibar kuongelea mambo ya muungano.
Haitwi kwasababu ya uongozi tu, kubwa ni ushawishi wake miongoni mwa waumini.

Hakika mratibu mkuu wa shughuli zote ni mmoja wa wana JF. Huyu ndiye anayeratibu shughuli zote ikiwa ni pamoja na kutoa misamiati.

Endapo kufanya hivyo ni sahihi au siyo, lengo langu si kuonyesha ubaya au uzuri hasa katika masuala ya imani.
Ninajaribu kuonyesha tu hali ilivyo na jinsi watu wanavyoliangalia jambo hili kwa mtazamo tenge.

Nasema mtazamo tenge kwasababu Ponda ni mjumbe, watoa ujumbe ni nadra sana kuwaona hadharani, lakini kadri siku zinavyosonga utaweza kuwaona katika mikutano,makongamano, majarida,magazeti na vitabu wakieleza kwa undani kuhusu mpango mzima ulikuaje.

Watu wanatafuta CV pengine kwa kutaka kujua kina cha usomi wa huyu bwana. Ninachokifahamu ni kuwa Ponda ana ushawishi tu, behind the scene there some elite who orchestrate the drama.
They never show up on the stage rather operating behind the curtain
 
UCHAGUZI CCM-DODOMA

CCM inajiandaa kwa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba, ni uchaguzi utakaopanga safu ya uongozi itakyopambana na vyama vya upinzani mwaka 2015.

Tuliwahi kusema huko nyuma watarajiwa wa kubeba bendera ya CCM wanajipanga katika sehemu kama NEC na CC ili kurahisisha teuzi zao. Wapo wanaojipanga kama Marais, wengine wakipiga debe ili wafikiriwe muda muafaka utakapofika.

Katika hali ya kushangaza kundi la wazee wenye umri wa miaka 60+ ambao waliwahi kuwa viongozi kama akina Kate Katamba,Ali mchumo, Patrick Chokala, Seif Mpembenwe n.k. Wote wameidhinishwa kuwania nafasi mbali mbali.

Katika mshangao huo huo kundi la watu wanaojulikana kwa ufisadi nalo limeingiza timu ikiwa ni pamoja na wana mtandao.
Kundi lingine ni la viongozi wastaafu kitaifa na waliojiuzulu wakiwemo akina Sumaye na Lowasa.

Lipo kundi la vijana wachanga kisiasa ingawa ni dogo sana ukilinganisha na kauli za kila siku tunazozisikia kuwa sasa ni zamu ya vijana. Haionekani kama hilo ni kweli.

Na mwisho ni kundi la waathirika wa siasa chafu akina Kigwangalla na Bashe ambao 'wamechinjiwa baharini'.

Kutoswa kwao ni kutokana na misimamo yao ya kupingana na serikali ya chama chao kama kumuunga mkono mh Zitto katika karatasi iliyolenga kumuengua waziri mkuu. Hawa wametoswa ili kupeleka ujumbe kuwa chama kimeshika hatamu na ili uwe salama lazima uwe na utiifu, muoga, ujifunze uongo,fitna n.k.

Wakati hayo yakiendelea kuna tukio lisilo la kawaida hasa kwa mwenyekiti Kikwete.
Ratiba ya vikao vya chama ilipangwa kwa kuzingatia ratiba nyingine. Kwa sasa hivi kikao cha baraza kuu la umoja wa mataifa kinaendelea na kwa vyovyote vile ilijulikana tarehe tangu mwaka jana.
Katika hali ya kawaida ratiba ya vikao vya chama ingezingatia hayo ili kumpa Rais muda wa kuhudhuria kikao hicho muhimu.

Tofauti na hivyo, rais ametuma waziri wa mambo ya nje Bernad Membe kumwakilisha. Kwa bahati nzuri au mbaya ziara ya Membe imekuwa na publicity ya hali ya juu kiasi cha kuleta 'political bang' muungurumo wa kisiasa.
Je, hili limefanyika kwa makusudi au limetokea tu!

Kwamtazamo wa kisiasa kuna makundi haya yamejitokeza yakiwakilishwa na wajumbe kama niliyotaja makundi hapo juu.
1. Kundi la wazee wanaotaka kurudi katika uongozi wa chama
2. Kundi la mtandao likijumuisha mafisadi
3. Kundi la vijana!!
4. Kundi lisilo rasmi lenye ushawishi kwa kupitia nyadhifa.

Nani wanayaongoza makundi haya?
1. Kundi la wazee wanaorudi kwa kasi linasemwa kumuunga mkono Spika wa Zamani Samwel Sitta.
2. Kundi la mtandao(original) hili linasemwa kumuunga mkono Waziri mkuu aliyejiuzuku E.Lowasa.
3. Kundi la vijana, hili limemeguka lakini sehemu kubwa ni ile inayomuunga mkono Lowasa kwa'kushawishika'.
4. Kundi lisilo rasmi ni lile linalotengenezwa na sehemu ya mtandao uliomeguka na inasemwa kumuunga mkono B.Membe

Mbinu zitumikazo
Kama mnakumbuka waziri Sitta amekuwa mikoani kuunga mkono shughuli za maendeleo.
Aliwahi kwenda kanda ya nyanda za juu kusini, kanda ya ziwa na hivi karibuni kanda ya kati. Kila alipokwenda amekuwa akizusha kauli zenye utata.

Hilo ni muhimu kwasababu anajenga kitu kinaitwa'political existence'. Tumemsikia akishambulia CDM na CCM kwa nyakati tofauti. Ziara zao ni kutafuta kuungwa mkono na kushawishi baadhi ya wazee kurejea ili kujenga mazingira mazuri.

Tumekuwa tukimuona waziri mkuu aliyejiuzulu akihaha huku na huko, katika maulid na harambee za makanisani.
Huko alipita ili kufunga watu macho, ziara zake zilikuwa na vikao vya siri vilivyokuwa vikiujenga mtandao upya baada ya kupata 'ajali za kisiasa'. Tumeona hata walioachwa uwaziri wakirejea tena kugombea nafasi.

Kundi la vijana hili ndilo linakivuruga chama. Wapo vijana wanaounga mkono mtandao kwa vile wamewezeshwa na wameahidiwa makubwa. Lipo kundi la vijana wanaunga mkono kambi isiyo rasmi likiongozwa na watoto wa vigogo.

Kundi lisilo rasmi kama nilivyosema ni lile linaloongozwa na B.Membe. Kundi hili halionekani kuungwa mkono hadharani lakini kuna dalili zote za maana kuwa lina baraka za Rais na kundi la vijana lisilo rasmi.

Kwa kutambua kuwa nguvu ya kundi hili si kubwa sana, na kwa kujenga mkakati wa muda mrefu, kitendo cha Membe kumwakilisha rais katika wakati nyeti kama huu ni sehemu ya publicity.

Kundi hili la Membe halitaki kujitokeza mapema, wanachotaka kufanya ni kujenga msingi kwanza 'ground work' halafu litaibuka na kufanya shambulio la kushtukiza 'ambush'.

Katika kundi la mtandao, waziri mkuu mstaafu Sumaye ameonekana kurudi katika siasa.
Sumaye anaelewa wazi kuwa hawezi kupata nafasi ya uongozi.
Ikumbukwe kuwa wakati mafisadi wanakabiliwa na wakati mgumu ndani ya chama, ni Sumaye aliyewahi kusimama na kuwatetea kwa njia isiyo rasmi.
Uwepo wa Sumaye una maana kuu mbili.
1. Kuhakikisha kuwa yeye na BWM wanafahamu nini kinaendelea ndani ya chama kwa 'usalama' wao.
2. Kumuunga mkono E.Lowasa ingawa haionekani wazi. Haya yanafanyika kukiwa na chuki dhidi ya JK na wakati huo huo kufanya kitu ambacho mkurugenzi wa TIC Ole Naiko aliwahi kukisema.
Naiko alikaririwa akisema kuna mkakati wa kuwaondoa wamasai katika serikali na chama.

Hadi hapo tumeweza kuona jinsi makundi yanavyojipanga. Matokeo yatatoa picha halisi ya nani anaweza kubeba bendera ingawa kazi hiyo haitakuwa rahisi kwani uwezekano wa mpasuko mkubwa wa chama ni dhahiri.

Tutaendelea kuangalia nini kinajiri.
 
UCHAGUZI MAREKANI: MDAHALO, CCM: UCHAGUZI

Jumatano kutakuwa na mdahalo wa wagombea urais Marekani.
Obama anakwenda katika mdahalo huo akiwa anaongoza katika majimbo(states) 9 ambayo hubadilika kila mara(swing state). Majimbo hayo ndiyo yenye kuamua rais ajaye kwasababu yapo yanayojulikana kama red states(Republican) na Blue states(Democrat) na wagombea wanajua ushindi wao kuhusu maeneo yao

Kishindo cha mkutano mkuu wa Dem kimeongeza sana tofauti kati ya Obama na mpizani wake Romney.
Na kwa bahati mbaya, kisiasa wiki mbili zilizopita hazikuwa nzuri kwa Romney na hivyo kupunguza kasi ya kampeni ili kurepea uharabifu aliousababisha mwenyewe kwa matamshi yake.

Katika sehemu ambazo Romney ni lazima ashinde, Ohio ni mojawapo kutokana na wingi wa wajumbe.
Jimbo jingine ni Florida ambalo pia kama Ohio lina wajumbe wengi.

Kwa hesabu za haraka Romney ni lazima ashinde majimbo hayo kuweka matumaini hai.
Kwa kutumia udhaifu huo, Romney amekuwa akitumia muda mwingi sana kukampeni huko na Obama akiendelea kumbana huko huko ili asiweze kutoka na kwenda kwingine.

Mdahalo wa uchaguzi wa marekani umeonekana kuwa na nguvu sana ya kubadili mweleko wa kisiasa.
Ni kwa mantiki hiyo mdahalo wa kesho unaotarajiwa kuangaliwa na watu milioni 50 ni muhimu kwa pande zote.
Tofauti ya Obama na Romney ni ndogo sana kiasi kwamba si jambo jema kudharau jambo muhimu kama hili.

Advantage aliyo nayo Obama katika mjadala ni ukweli kuwa sera zake ziwe za afya, uchumi na kodi zinajulikana kwahiyo anachotakiwa ni kuzitetea. Romney ana wakati mgumu kwasababu hajaweza kuja na specifics za nini atakifanya na au nini ni sera zake. Amekua anabadili misimamo mara kwa mara jambo litakalomweka mahali pagumu kwa kiasi fulani.

Advantage ya Romney ni ukweli kuwa anauwezo mzuri wa kujieleza na anaweza kumshambulia Obama kwa sera zake kwasababu zake hazijawahi kujaribiwa. Kwa hiyo anakwenda akiwa na tension ya kuwa nyuma katika Polls lakini at easy.

CHAGUZI ZA CCM
Chama cha mapinduzi kimemaliza vikao vya uteuzi kama tulivyowahi kujadili.
Uchaguzi mikoani unaendelea huku baadhi ya vigogo wakilamba mchanga.
Japo wengine wanadhani kuwa hizo ni jitihada za kuusambaratisha mtandao, ukweli ni kuwa mtandao unajengwa kwa pesa na hivyo wajao wanaweza kuingia katika timu kama kawaida.

Kubwa katika matokeo ni lile la PM Sumaye kula mweleka. Kisiasa hapa kuna mambo mengi yamejichanganya.
Sumaye alikuwa mtetezi wa Lowasa na haijulikani kama mbio zake ni za kuwainia Urais au kumuunga mkono Lowasa.
Haijulikani kwanini autake ujumbe wa NEC mtu aliyefikia hadhi yake.

Mary Nagu ni mshirika mzuri wa Lowasa hata kama inaonekana wanakinzana baadhi ya nyakati na kwahakika ushindi dhidi ya Sumaye umepokelewa vizuri na Lowasa.

Lowasa anachokitafuta sasa hivi ni kuwa na wapinzani wachache ili njia iwe nyeupe. Anajua Sitta na Membe wanampumulia mgongoni, anafahamu kuwa kashfa zainazomwandaman zinaweza kutumiwa vilivyo kwahiyo anapokuwa na 'maadui' wachache ni bora zaidi.
Hamwamini Sumaye kwakujua kuwa naye pia anakiu ya kwenda magogoni na anaungwa mkono na BWM.

Umuhimu wa Nagu kwa Lowasa upo katika UWT. Kundi hili hatujaliongelea, umuhimu wake ni mkubwa kuliko jumuiya zingine. Ni kundi lenye wawakilishi wengi ndani ya NEC na mkutano mkuu. Lina wajumbe wengi bungeni n.k. tofauti na UVCCM au Wazazi.
Kwahiyo Nagu atasaidia sana katika kuwaweka wajumbe sawa.

Nigusie kidogo kuwa kinyang'anyiro cha UWT kina makundi mawili.
Sophia Simba ambaye ni Lowasa bila kubabaika.

Kuna Ann Kilango ambaye anaingia katika kofia mbili.
Kwanza kumuunga mkono Sitta kwasababu ya mzee kuwa sehemu ya kundi Sitta.
Ikitokea Sitta hatamudu mapigo basi atamuunga mkono Membe.
Kwa uchache mtifuano wa UWT ndio unategemewa kutoa picha ya kule twendako.

Tutazidi kuangalia duru matukio kila tunavyoyapata
 
Back
Top Bottom