DURU: Utangamano, Amani na Ustawi. Taifa linaelekea wapi?

DURU: Utangamano, Amani na Ustawi. Taifa linaelekea wapi?

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
3,622
Reaction score
9,301
Ustawi
Taifa lolote linalotazama Ustawi na maendeleo yake huzingatia utangamano na Amani.

Utangamano '(compatibility ) ni uwepo wa pamoja(coexist) licha ya tofauti za Raia katika rangi, Imani, itikadi za siasa na Utamaduni. Amani ni utulivu unaoletwa na uwepo wa maridhiano na haki.
Amani si Ukimya unaoletwa na shinikizo (subdue)....

Katika miezi michache kuna hali, matukio na kauli zinazoacha swali, Tanzania kama Taifa, je, tuna utangamano na Amani ? Taifa linaelekea wapi katika hali ya mivutano na michuano isiyo ya afya yoyote iliyopo, inayoendelea sasa...?

Ni kawaida kwa 'shughuli za tasnia au fani fulani kuwa na lugha zake....

Mfano, utani wa Simba na Yanga una lugha zenye karaha. Kwa asiye elewa lugha ya mpira, anaweza kupata shida sana...

Utani katika siasa kama kuitana nyumbu au zero brain ni wa kawaida nchini.

Pamoja na hayo utani wa simba na Yanga una mipaka yake. Kwani mwisho wa siku Watani hukaa pamoja na kula, hujumuika kuuguzana, na hushirikiana kuzikana. Ni utani wa mpira usiohusisha ubinadamu..

Siasa za vyama vingi hazijawahi kusimama bila matatizo, na matatizo yalipojitokeza yalishughulikiwa na viongozi. Ni ukweli usio na shaka kwamba kuanzia 2020 siasa zetu zimebadilika katika uelekeo wa ubaya wa hatari...

Tulimsikia kiongozi mmoja ambaye sasa ni RC akitamka '' Wapinzani wapigwe risasi''

Hivi katibuni tukasikia kiongozi mwingine akisema '' Wapinzani wakipotezwa'' polisi wasiwatafute
Kiongozi mwingine akisema, "Wapo Watanzania (CHADEMA) wanadhamiria kununua vidudu vya maradhi ya Ebola na M-pox na kuvisambaza nchini Ili kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025 usifanyike...''

Tumesikia gari la kiongozi likichomwa moto , wafuasi wa vyama wakirushiana makonde n.k...

Tumesikia watu kutekwa, kupotezwa n.k. katika mazingira yanayoashiria siasa za shari na chuki...

Katika hali ya kujengeka chuki na kauli za kichochezi zikihamasisha uhasama, tulitegemea sheria zichukue mkondo wake kwa wahusika kwa kuwa kufanya au kushughulikia mambo yetu na migogoro kwa kuzingatia misingi ya SHERIA ndio msingi wa HAKI inayoleta Amani....

Hata hivyo, vyombo husika katika kusimamia na kutoa HAKI ima vimefumbia macho au vimekuwa na makengeza kwa sababu za kisiasa na kwa masilahi ya viongozi wa kisiasa na si Taifa kwa upana wake...

Hali ni mbaya , makundi ya jamii yanaingia katika mivutano yakiwemo ya Dini bila kutaraji...

Viongozi wamejikita kutumia nguvu na vyombo vya dola kutafuta 'Ukimya'' na si Amani.

Viongozi wanahubiri uwepo wa Amani wakijua fika hilo ni Tunda la HAKI isiyokuwepo....

Ni katika mivutano iliyopo vyombo vya dola vilivyonyooshewa vidole kwa muda mrefu kuhusu matukio mabaya ya utekaji, mauaji na dhulma vimejikuta ''vikithibitisha mashaka ya muda mrefu kwa ushahidi waliohisi kuwa vinahusika na matendo hayo mabaya kabisa...''

Kwa mwendo huu, Taifa linaelekea wapi...?

Inaendelea...

NOTE: Andiko hili kwa sehemu kubwa nimelitoa Jukwaa la JF Great Thinker kwa hisani mkongwe wa JF ndugu Nguruvi3)
 
Back
Top Bottom