'' Trust, Integrity, Credibility ''
Jeshi la Polisi lanyooshewa kidole tena
Polisi warudia makosa yale yale ya kujichunguza
Hapa chini kuna link ya hotuba ya Mzee Jaji Warioba katika kongamano la TLS
View: https://www.youtube.com/watch?v=OCLDXl-xRkE
Kabla ya kujadili hotuba ya Jaji, tupitie maneno matatu yenye maana zinazofafana lakini ni tofauti kwa mantiki. Trust ( kwa tafsiri isiyo rasmi ni aminika, au kuaminika ) Mtu mwenye ''trust' ni anayeweza kuchukua dhamana ya jambo fulani.
Integrity ( Uaminifu/uadilifu), kwa maana ya kuaminika katika uadilifu.
Halafu kuna credible '' sadiki, sadifu) kwa maana ya jambo lenye sadifu
Mtu anapokuwa na trust, anakuwa na integrity na anachosema kinakuwa credible.
Katika link, Mzee Warioba amehoji Jeshi la Polisi kwa mambo kadhaa. Moja, kwanini walikamata Watu waliokwenda Mahakamani kwa amani na wengine kama Heche kukamatwa hata kabla ya kufika.
Jaji anauliza kwanini hawakufunguliwa mashtaka zaidi ya kuzungushwa na magari kisha kuachwa.
Mzee Warioba akasema wapo waliotupwa Mabwepande, halafu jeshi limekanusha !
Jaji Warioba akasema Polisi wanatumika kisiasa. Lakini kubwa zaidi ni pale alipohoji '' halafu wanataka waaminiwe'' kwa maana ya kwamba habari zao zinakinzana , hazina ithbati kulingana na vitendo.
Kwa maneno mengine , Mzee alihoji, trust ya Jeshi, integrity katika utendaji na credibility.
Hili ni jambo zito kutoka kinywani mwa mstaafu Waziri Mkuu, Mwanasheria mkuu , waziri wa sheria.
Jeshi la Polisi limesema linafanyia kazi tuhuma za Raia kushirikishwa na Askari katika ''ujasusi' dhidi ya Mwanaharakati ailiyetekwa. Jeshi la Polisi limeunda kikosi kazi.
Kwamba tuhuma zinaelekezwa kwa Polisi halafu kikosi kazi ni cha Polisi ili kimchunguze Polisi!
Taarifa yoyote itatiliwa shaka kwasababu hakuna trust, integrity au credibility ya Jeshi la Polisi
Na hii inatokea kwasababu RPC keshasema Polisi hawamshikilii Mwanaharakati.
Kwa maneno mengine RPC amewasafisha Askari wake. Halafu kuna kikosi kazi cha kumchunguza RPC na Askari wake kinachoundwa na Polisi. Hapa integrity, trust na credibility inatoka wapi?
Kwa mtazamo huo, ili Jeshi liaminike na kuaminiwa na kusadikiwa taarifa za kukinzana, zisizothibitika zinaliondolea uaminifu mbele ya Umma.
Tuhuma za Askari Polisi zichunguzwe na chombo huru!
Hakuna haki ya Polisi kujichunguza, na hilo tu linazidi kupoteza imani ya Wananchi.
Hata kama Mwanaharakati huyo ametekwa na ''kaka au Baba au nduguye'' hakuna atakayeamini taarifa ya Kikosi kazi cha Polisi hasa katika wiki hii ambayo taarifa za Polisi zimekinzana, zisizoaminika na kuoenekana zinapootosha Umma. Mzee Warioba kaeleza kwa kina haya ! asikilizwe
Kama Taifa tunaelekea wapi?