Dunia ni zaidi ya tuijuavyo, cheza salama

Dunia ni zaidi ya tuijuavyo, cheza salama

Mbna nyota zimejaa kibao Angani , kwanini wasiende wakaibe nyota kwa wazungu , nchi iendelee la maendeleo ya maana , kwahiyo una maanisha Bashite kaibiwa nyota pia hahahahahahhaa
Bashite kaiba nyota ya mtu sasa anashindwa jinsi ya kuitumia. Inamsumbua.
 
Uwiiiii sijawah kucheka kama leo, wallah kaiba nyota kubwa kuliko uwezo wake , na mwenye nyota naona anamuandama usiku hatari mzee wa madhabauni sijui madhibauni sijui mabadhauni ... Hahahahah
Bashite kaiba nyota ya mtu sasa anashindwa jinsi ya kuitumia. Inamsumbua.
 
Habarini ndugu zanguni, poleni sana na mahangaiko ya dunia hii siku zote kumbuka mpaji ni MUNGU pekee.

Leo katika pita pita zangu za vijiweni na story za hapa na pale kulingana na story tulizokua tunapiga nikaikuta nimeseama “…..nikioa na mke wangu akiwa mjamzito nitampeleka akajifungulie kwao, maana siku hizi nasikia wadada wengi hawana Uhuru na nyumbani kwa mama mke…..” Mzee mmoja akanisikiliza sana kwa makini akasema “……kijana usijaribu huo mchezo, Mkeo ajifungulie kwako, tena ikiwezekana mtoto asionekane na mtu hadi zipite siku 40 akiwa ameshakua kila mahali kwa mwili na kitovu kitakua kimekauka……..”

Ndugu zanguni, nimeshangaa sana sana sana, mzee akaendelea kusema, kuna watu na viatu dunia hii akaongezea dunia tambara bovu, akasema unapompeleka mke kule kwao/kwenu watu wengi wanaokuja kumuona mtoto si wote wenye nia nzuri na mtoto, wengine wanakuja kutazama nyota ya mtoto afu wanamchukua wewe unaachiwa roboti linalopelekwa tuu, NIMEBISHA SANA

Mzee akaendelea akasema kijana wangu ulimwengu wa roho ni mmoja, akatoa mfano unakuta mtu ana akili sana lakini maisha yake utamuonea huruma n.k,n.k akaendelea akasema watu wanaoenda kwa mganga kupata kitu Fulani usidhani ni kwamba mganga anavyo hivyo vitu HANA, kwakua ulimwengu wa roho ni mmoja acnachofanya anaita mapepo/majini. How?

Ni hivi amesema, daily routine ya mwanadamu inakua recorded kila kitu (chochote unachofanya kinarekidiwa) upande wa shetani kivyake na MUNGU kivyake, so shetani anajua kila kitu kuhusu wewe hadi vipawa ulivyopewa na Mungu anajua hivyo ni rahisi kwake kujua wewe ni nani wa baaadae na unafaa kwa kipi na nyota yako ni ipi.

Sasa mapepo/majini yale yanakua na taarifa za kila mtu, mganga yule yeye anamsikiliza mteja wake anataka kitu gani, sio kwamba mganga anavyo, hata yeye HANA HATA KIMOJA anachofanya yeye anaingia kwenye ulimwengu huo wa roho anaangaza huyu mteja anataka nini anaita mapepo/majini yale yanajua kitu Fulani kipo kwa mtu Fulani so kinachofanyika ni kupokonywa nyota yako na kupewa yule mtu na wewe utabaki ukihangaika na kusumbuka chini ya jua hili kumbe umeibiwa zamani sana, mzee alikiri NI MUNGU TU ANAEWEZA KUIRUDISHA HAKUNA MWINGINE

Sasa unakuta mtu ni Inperation speaker mzuri san asana sana, asee kumbe amepokonya nyota ya mtu huko na anajua kabisa kuwa hii si yangu, mzee akasema wanailinda kuliko ulinzi wa raisi ikulu, wengine wanaenda hata kuzifungia nje ya nchi, wengine wanazitumia tu pale wanapokua na shughuli hiyo huiska wakimaliza tu wanairudisha kwenye ulinzi.

Mzee akasema, unakuta mtu ameenda kutafuta nyota za watu hata 5 anazo anazitumia tu.sasa kinachotokea watu siku hizi wanaiba nyota za watoto wanaozaliwa kwa kuwa watu wengii sana chini ya jua hili wameshaibiwa ko wakienda kuanganza wanakuta wengii wamechukuliwa nyota zao, akamaliza kwa kuniasa MKEO AZALIE KWAKO MWANANGU.

HAKIKA DUNIA NI ZAIDI YA TUIJUAVYO

Cc: Mshana Jr
1. Sikubaliani na kuiba nyota.
2. Nakubaliana na kumuweka mtoto chini ya uangalizi wa mama yake angalau kwa siku 40, hii ina faida kwa afya ya mtoto kwa maana mtoto anapozaliwa anakua bado hana kinga ya kutosha hivyo ni rahisi sana kuambukizwa magonjwa kwa njia mbalimbali.
 
Hapana si mara zote watu hujibu kwa usahihi.... Kujibu na jambo la kwanza kujibu kwa usahihi ni jambo la pili
Katika uchambuzi was vitabu(sekondari), kila mmoja huwa anachambua kulingana na alivyoelewa. Hivyo kuna nilivyoelewa ambayo si lazima ifanane na kila mmoja. Hivyo uko sahihi na mimi niko sahihi pia, maana kila mmoja kaelewa kulingana na utashi wake.
 
Nimesikitika sana kuona masuala ya kina mama yanazungumzwa kijiweni tena cha wanaume

Wellcome Again
 
Katika uchambuzi was vitabu(sekondari), kila mmoja huwa anachambua kulingana na alivyoelewa. Hivyo kuna nilivyoelewa ambayo si lazima ifanane na kila mmoja. Hivyo uko sahihi na mimi niko sahihi pia, maana kila mmoja kaelewa kulingana na utashi wake.
Ni kweli kabisa lakini huwa kuna uwiano na uhalisia wa kitu ndio maana walimu hutoa alama tofauti kwenye uandishi wa insha... All in all asante
 
Ulimwengu wa kiroho una mengi sana hata hivyo hakuna wa kuishi milele kuweza kuyafahamu yote hayo.
 
Acha kutishiwa Mkuu. Hizo ni porojo. Nyota ni kufuata maagizo na Amri za Mungu.

Hizo nyingine ni porojo. Mungu kakuwekea Kifo na Uzima. Akasema chagua Uzima upate kuishi.

Ukiasi amri za Mungu utahangaika kutafuta mchawi aliyekuibia nyota kumbe mchawi ni wewe.

Acha kuhadaiwa. Dunia ni simple sana kama utaamua kuwa hivyo. Ni complex ukiamua kuifikiri hivyo.

Hako kazee ni Kaboya na kapumbavu. Sasa kana taka kukuambukiza wewe.

Shika Amri na maagizo ya Mungu alafu uone maisha yanavyonyooka. Nyota ni Amri na maagizo ya Mungu. Usipozishika inazima ghafla na hakuna wakuiwasha zaidi ya wewe mwenyewe ukuamua kumrejea Mungu.

Mkuu acha kugeuzwa mjinga ungali unaakili.

Hakuna uchawi kwa mtu anayeshika amri za Mungu.

Mke azalie sijui porini, Sijui umpeleke Ukweni au vituo vya Yatima Ikiwa utamgundisha kushika na kutenda kama Mungu atakavyo hivyo vijini mshenzi na Vishetani uchwara havitasogea.

Umemtag Mshana Jr ili aendelee kuwahadaa wajinga na wapumbavu.

Mafanikio ni Kumjua Mungu na Kufanya ayatakayo.
 
Mambo ya kishirikina hayo.....ukiyaendekeza yanakutia motoni milele
 
Back
Top Bottom