Dunia ni kama VIDEOGAME isio na uhalisia wowote

Uwesutanzania

JF-Expert Member
Feb 9, 2019
859
1,012
Fikiria kidogo na namna dunia ilivyo na namna unavyoiishi.

Ni kama (VIDEOGAME) isiyo na maana wala uhalisia wowote katika maisha halisi.

Hauwezi nielewa kama wewe ni mtu usiyependa ishughulisha akili yako katika vitu uvionavyo.

Kama wewe ni mtu unayeangalia (BRITAIN'S GOT TALET) na unaamini kuna matukio ya uchawi mule ndani basi andiko langu hauwezi lielewa kamwe.

Ninachokitaka kwako penda sana kuimani akili yako, na usipende kuamini vya visivyo onekana.

Em wacha twende kwenye mada kwanza.
Unajua kwanini nimesema DUNIA ni kama VIDEOGAME?

Em tuliza akili yao alafu twende pamoja.


Je, ulishawahi tumia nguvu kubwa hata ukagombana na mtu kwenye kuitafuta PESA?

Kama jibu ni ndio je hiyo pesa ulikuja ifayaje baada ya kuipata?
Si ulijengea nyumba, si ulimpa mwanamke, ukanunua na magari? Je unahisi hiyo pesa inaendelea kukupa furaha?

Au umerudi tena kwenye uhalisia wako na msongo wako wa mawazo?.


Je, ulishawahi tumia nguvu kubwa hata ukagombana na watu wengine kwenye kumpata MWANAMKE/mwanamume umpendaye, je baada ya kumpata umeona huyo mwanamke anaendelea kukupa furaha au unaendelea kuitafuta furaha?


Ndugu zangu dunia na vilivyomo ardhini havina maana yeyote ni kama VIDEOGAME isiyo na uhalisia katika maisha halisia.

Je maisha halisia ni yapi?

Maisha halisia ni kufa pekee.
Ukitumia akili utaelewa kwanini nimesema maisha halisia ni kufa pekee.

Wengi wetu wakati VIDEOGAME limechanganya hatupendi kuzima mtambo. Hata kula tunasahau.

Ndio dunia sasa.

Dunia limechanganya kwa kasi na kuona kila kilichomo ni kilicho bora na hatupendi kuzima MTAMBO.

Ndugu yangu dunia inakudanganya sana.,
 
FB_IMG_1703734587446.jpg
 
Huo ni ukweli ,kila siku tupo kweny mission mpya kulingana na umri & majukumu ...Hatutoweka kupumzika hata upate nn bado utaona hamcha maana ila mwisho wa siku tunakufa.

Leo sio yule ex alikutambia kisa kaolewa basi miaka 2 mbele ile ndoa haina furah na washachokana kila mtu anatafuta exit plan ....Tuishi tu kwa kutafuta hata upate upendacho bado utatafuta tu hayo ndio maisha.
 
USICHO KIJUA HADI LEO NIKWAMBA
Hakuna uhalisia wakila kitu kilichopo duniani,yani mfano wake nimtu alie play movie ya expandable kisha akaenda zake n'je kucheza bao. huku n'je anampiga mabao yakutosha nakule ndani kwenye movie mabom ya nyuklia yanalipuka nakuangamiza kila kitu duniani.
Hapo majiniazi pekee mmenielewa.
Kwahiyo hii ni thread ta Ma-geneous watupu?
 
Kweli unachosema, watu tunajipa stresss bure mara uwe na watoto sijui ujenge, mi huwa nawauliza watu ufanye yote hayo then?

Huo ni ukweli ,kila siku tupo kweny mission mpya kulingana na umri & majukumu ...Hatutoweka kupumzika hata upate nn bado utaona hamcha maana ila mwisho wa siku tunakufa.

Leo sio yule ex alikutambia kisa kaolewa basi miaka 2 mbele ile ndoa haina furah na washachokana kila mtu anatafuta exit plan ....Tuishi tu kwa kutafuta hata upate upendacho bado utatafuta tu hayo ndio maisha.
Alafu mbaya zaidi ndani ya hizo mission kuna zawadi ambazo hatuna matumizi nazo zinazopelekea watu tunanyanyasana na kuuwana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom