Dunia kwa sasa haina tena taifa kubwa

Dunia kwa sasa haina tena taifa kubwa

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
10,502
Reaction score
16,712
Kushindwa kwa Urusi kuiteka Ukraine kwa haraka na kukimbizwa Marekani kule Afghanistan na wanamgambo wa Taliban kumedhihirisha kwa mara nyengine kuwa kwa sasa dunia hakuna tena taifa kubwa.

Baada ya Urusi kupeleka msururu mrefu wa vikosi vya jeshi vinavyofikia kilomita 4 kuuzunguka mji mkuu wa Ukraine,Kiyv tulitaraji shughuli ingekuwa imekamilika si zaidi ya wiki.Kumbe sehemu kubwa ya ule msururu wa jeshi umeangamia mikononi mwa askari wa Ukraine.

Pamoja na hilo hata wale askari wa Urussi waliosalimika wamerudi mikono mitupu bila vifaru vyao na silaha nyengine muhimu katika jeshi hilo.

Inasemekana mtambo muhimu wa kuongoza jeshi nao umechukuliwa na Ukraine na wameahidi kuupeleka Marekani ili kufichua siri zake.

Hii si mara ya mwanzo kwa Urusi kurudishwa nyuma katika vita namna hii.Mara ya mwanzo ni 1979 kule Afghanistan ambako vifaru vyao vingi na askari walipotea na hata wingu la ndege za kijeshi angani havikusaidia.

Safari nyengine ni kule Chechnya mwaka 2006 ambako hatimae walilazimika kutumia mbinu ya kuwagawa wachechnya badala ya kupigana nao.

Marekani kwa upande mwengine imeshindwa kabisa kupigana wala kuwaondoa madarakani viongozi kadhaa mahasimu dhidi yao mfano Venezuela,Syria,Irani,Korea kaskazini n.k.

Wamelazimika kufanya unyama mkubwa katika nchi za Iraq na Libya ambazo nazo zote wananchi wake hawajaridhika kukaliwa na taifa hilo na ndio maana kila siku wakipata fursa wanalipiza kisasi kinachopelekea Marekani kurudi nyuma.
 
Kushindwa kwa Urusi kuiteka Ukraine kwa haraka na kukimbizwa Marekani kule Afghanistan na wanamgambo wa Taliban kumedhihirisha kwa mara nyengine kuwa kwa sasa dunia hakuna tena taifa kubwa...
Siyo ukweli, bado kuna mataifa makubwa na mataifa madogo. Ukifuatilia hata huko unakosema ni kushindwa kwa US au Urusi utagundua ni kutokana na haya mataifa makubwa kuzungukana kwenye hivyo vita.
 
Mkuu vita sio lele mama haijalishi unaye pambana naye ni dhaifu kiasi gani.
 
watu tunashindwa kuelewa.hata leo tukisema tanzania ikavamie burundi tunaweza kutoka kwa aibu.
vita ngumu ni hile unakwenda kuvamia kwa mwenyeji ujui historia yake.Ndio maana unakuta unapoteza wanajeshi wengi sana.

Kama unakumbuka USA ilikwenda kuvamia ujerumani vita ya pili,USA ilipokwenda kuvamia vetnamu,USA ilipokwenda kuvamia somali.
hizo sehemu zitakupa mfano tosha kuwa kuvamia nchi za watu ni ngumu labda upate ushirikiano na wananchi
 
Ubeberu wa wamagharibi unaficha hata taarifa za uhalisia wa kinachoendelea Ukrain
Hapa naamini ndipo alipozidiwa nguvu Mrusi.Silaha anazo za kutosha.Wenzake wamekuwa na vyombo vingi vya habari kiasi kwamba hata wanajeshi wake wanavipata wakati wa mapumziko.Woga umewaingia na kupoteza hamasa ya vita.
 
Bado yapo na yataendelea kuwepo kwasababu ya factors zinazotoutisha mataifa kiuchumi, nguvu ya kijeshi, teknolojia na maendeleo ya kijamii zipo.
 
Nguvu ya kijeshi inapimwa na nini iwapo hao wenye silaha nzito wanashindwa na wanamgambo, Angalia hata Saudia anaavyoteswa na wanamgambo wa Houthi japo inajulikana amerundika masilaha tele ya hatari.
 
Hapa naamini ndipo alipozidiwa nguvu Mrusi.Silaha anazo za kutosha.Wenzake wamekuwa na vyombo vingi vya habari kiasi kwamba hata wanajeshi wake wanavipata wakati wa mapumziko.Woga umewaingia na kupoteza hamasa ya vita.
Hakuna mwanajeshi wa RUSSIA mwoga na alopoteza hamasa ya VITA(OP)
wao wapo field wanajua kwakiasi gani wamepata mafanikio huko field kwahio hizo kelele na maneno yakwenye media wala hayawatii khofu maana wanajua kipi wanachokifanya
Unadhani hao majeshi hawamsikii au kuona komedian analia lia nakuongea ongea kwenye bunge mbali mbali huko EU nakwengineko huku akiomba msaada
Hio tuu inatosha kukuonesha kwakiasi gani jamaa wanahali ngumu huko field mpaka wanaomba misaada
Huko field watu wanaamsha amsha yakutosha na wanapeleka moto wakutosha sanaaa yaani hawajali kuhusiana na propaganda wala nini sababu wanajua kama huko field mambo yanaenda kama yalivyopangwa
PUT IN anaendeleza OP yake kama alivyopanga nandio maana kila leo unaona jamaa wanaweka vikwazo kama ishara kwamba jamaa anatoa dozee dozee yakutisha nawanataka kumpunguza speed ila wanachemka!!!!!
 
Zelensky bad ni Rais wa Ukraine
 
Russia wamekimbia Kiev dunia nzima inajua
 
Mpaka hii vita iishe hakuna neno utakuwa umebakiza.Putin maliza hii vita kwa Nukes,unatesa sana ndugu zetu hapa JF unavyodemka tu kule Ukraine
 
Raisi aliyeweka rekodi ya kulialia wakati wa vita.Haijapata kutokea.
Na katika kulia lia kwake ndiyo amepelekea mpaka wewe kuanzisha hii mada au umesahau content ya mada yenyewe,vinginevyo sasa hivi ungekuwa unaitukuza Russia kwa kuwa 'super power'
 
Raisi aliyeweka rekodi ya kulialia wakati wa vita.Haijapata kutokea.
We ulitaka afanyaje historia itamkumbuka ni rais aliyemzuia Russia kwenye jaribio alilotaka kuipundua nchi kwenye vita kila mtu anatumia mbinu anayoijua yeye Cha muhimu ni ushindi
 
Back
Top Bottom