Mkuu ni hivi; katika uso wa jua (corona) kuna miripuko ya moto kama vile miripuko ya volcano katika milimo, (solar flares/ coronal mass ejection), sasa hiyo milipuko isipotokea katika usovwa jua ndipo hali hiyo inaitwa "solar minimum"-- au kama ni ugonjwa unaweza kusema jua limekumbwa na ugonjwa wa "solar minimum".
Wasiwasi wa mleta ibara ni kwamba hali hiyo itasababisha joto kushuka katika uso wa dunia na hivyo kuharibu taratibu za mazingira na maisha kwa ujumla.
Mimi binafsi siafikiani naye au siafikiani na hao NASA, kwanza huo ni utabiri tu, pili reaction za kinuklia ndani ya kiini cha jua zinazosababisha joto na mwanga bado zitaendelea, isitoshe hiyo miripuko siyo chanzo kikuu cha joto na mwanga katika dunia yetu, hiyo milipuko ni kama bomba la moshi wakati hizo reaction zinapotendeka.
Kifupi ni kwamba hao NASA wametabiri (predict) tu na wala hawajasema hali hiyo itakuwa hivyo.
Pia hiyo hali sio mara ya kwanza kutokea, imeishatokea miaka ya nyuma.