Dunia inaogopesha ila wewe Usiogope, Maisha sio mashindano

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,050
50,996
DUNIA INAOGOPESHA ILA WEWE USIOGOPE 02! MAISHA SIO MASHINDANO

Anaandika Robert Heriel,

Umekata tamaa, hauna tumaini, mambo yote yameenda Kombo, kila ulichokuwa unakitumainia kimekusaliti, kila uliyekuwa unamuamini amekugeukia, dunia imekupiga kikumbo, hakuna yeyote aliye Kwa ajili yako! Loooh! Hayo ndio Maisha!

Maisha yanaogopesha Kwa sababu wengi huisubiri kesho, wakati kesho haipo Kwa ajili Yao. Kwa maana ya Leo huishia leo, na yakesho ni kwaajili ya hao watakaokuwako kesho.
Tena Kama ilivyo kesho ndivyo zilivyo Akili za watu. Usiitegemee kesho usije ukaona utisho wa Dunia.

Dunia inaogopesha Kwa sababu wengi huwategemea Watu, utamtegemeaje mtu usiyejua anachofikiri, hujui ayawazayo moyoni mwake. Ndio maana nikasema kuitegemea kesho ni Sawa na kumtegemea mtu.

Usiogope, usikate tamaa, ishi maisha yako.

Dunia inaogopesha pale utakapoishi maisha ya watu wengine.
Kutaka mazuri waliyonayo wengine, ilhali wewe na wao mpo tofauti.

Unasoma ili uwe kama Fulani,
Unasomesha watoto ili wawe Kama Familia fulani,
Nakuhakikishia Dunia itaku- suprise,
Matokeo yake yatakutisha na utapoteza shabaha ya kuishi, utaogopa na kukata tamaa.

Soma ili uwe wewe uliyebora, sio uwe kama wengine ili baadaye ujipende na wala sio ujipendekeze
Somesha watoto ili wawe wao sio wawe Kama familia Fulani, ili uwapende watoto wako na sio kuwalaumu Kwa sababu yeyote Yule afanyaye Jambo lolote Kwa mtoto wake Kwa kuwalinganisha na wengine hatawapenda watoto wake Bali atawalaumu.

Taikon hata mambo nimeyapima, tena nimeyatolea hesabu iliyo kamili, ni hiyari yako kunisikia au kuyapuuza.

Kama utatafuta pesa, zitafute Kwa ajili yako mwenyewe, wala sio Kwa ajili ya watu wengine. Tena sio ili uwe kama fulani, Bali uwe wewe katika ubora wako. Kwa maana lengo la maisha Kwa kila mtu ni kuishi maisha yake.
Lakini dunia imekuwa uwanja wa vita Kwa sababu watu hutafuta Kwa ajili ya watu wengine.

Tafuta pesa Kwa sababu unazipenda na nihitaji lako binafsi. Usitafute sifa Kwa watu wengine.
Hiyo ndiyo namna ya kuishi Kwa Furaha na Amani. Kuishi kwa Yale unayoyapenda, bila kujali wengine wanayaonaje.

Heshima ya mtu haijengwi Kwa kuwapendeza wengine, heshima ya mtu inajengwa Kwa mtu kuishi maisha yake bila kuathiri maisha ya wengine.

Vijana wa siku hizi wapo katika mtihani mzito Kwa sababu wanahangaika kutafuta mambo Kwa ajili ya wengine,
Hawatafuti pesa Kwa sababu Yao wenyewe, Bali hutafuta pesa ili wapate heshima wasijue heshima ya mtu hutoka ndani yake na wala sio nje.

Kijana, nisikie Mimi Taikon, pesa hazitakufanya uheshimike bali zitakufanya ujione Kama unaheshimika, unisome unielewe.

Kadiri unavyozitafuta pesa ndivyo unavyozidi kuwa mhitaji, kadiri unavyozipata ndivyo na mahitaji yako yanakuzidi.

Sisemi usitafute Pesa, Ila nasema tafuta pesa Kwa ajili yako mwenyewe, wewe na familia yako. Hapo ndipo utazifurahia.
Maisha sio mashindano.
Maana wivu ndio huleta mashindano, na wivu husababishwa na tamaa mbaya.

Usiolewe Kwa sababu ya watu wengine, Olewa Kwa sababu ni hitaji lako, unampenda na upo tayari kuanzisha familia.
Usiangalie wengine wanasemaje au wanafanyaje, ishi maisha yako lakini usisahau kanuni ya Asili ambayo ndio inalinda utu wako na kukutofautisha na Wanyama.

Usifuate mkumbo!

Fanya harusi vile uonavyo wewe na sio Kwa kuangalia wengine walifanyaje, usijitese.
Kusherekea sio lazima uite Watu wengi au kukodisha Ukumbi au kuita magari mengi na wapiga tarumbeta. USIWE MTUMWA WA MAISHA YAKO, Acha maisha yakutumikie wewe na sio wewe uyatumikie.

Dunia inaogopesha Kwa sababu Wazuri wanawaogopa Wabaya,
Wenye akili wanaongozwa na Wajinga,
Wenye Haki wanaamuliwa na Waovu,
Wenye macho wanaonyeshwa njiwa na Vipofu,
Watu wema wanajificha vichakani na Watu Wabaya wakipita Kwa kujiamini barabarani,

Wenye maarifa huona aibu kuyatoa maarifa Yao Kwa jamii, lakini wapumbavu hutoa upumbavu wao Kwa jamii bila haya.

Dunia inaogopesha Kwa sababu,
Wazazi wanawategemea watoto ambao wao ndio walipaswa wategemewe,

Wanaume wameacha kuwaongoza Wanawake.

Hata hivyo zingatia,
Hata kama ungesoma mpaka wapi lakini Dunia inahitaji Akili ya kuzaliwa ambayo huwezi kuisomea,

Hata kama Ungekuwa mzuri Kama Malaika wa Tibeli, ndoa halindwi na uzuri isipokuwa Hekima na busara. uzuri unachakaa lakini hekima na busara havichakai.

Hata kama ungekuwa Mbaya wa Sura Kwa kiwango gani, Dunia inahitaji uthubutu kupata yaliyo mazuri.

Mwisho, Hata ungepata kila kitu, lakini Moyo unachohitaji ni Furaha, na furaha inapatikana Kwa kuishi katika wewe na sio kuishi Kwa kumuangalia mtu mwingine.

Ndimi, Taikon kutoka Nyota ya Tibeli, Nyota yenye Mbawa mbili irukayo kutoka Ulimwengu huu mpaka ulimwengu mwingine.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
kuna muda unaweza jiona una changamootoo mingi hadi kukata tamaaa ... ila ikitokea tu umesikiliza ama kuona changangamoto za mwinginee.... unaishia kujisemeaa ' duh kumbe mie nina afadhali'

Ni kweli Kabisa.
Maisha yanahitaji Subira, kisha uthubutu, lakini kukubali matokeo hata kama mambo yakienda Kombo.
 
Nina kadi 6 za kuchangia harusi Zote za mwezi wa 7, minimum ni laki saba hiyo.

Last weekend imeisha harusi moja nimejikausha kama sipo, ni kweli usipoishi kama wewe utakuwa kama mtumwa duniani kutaka uonekane mwema kwa kila mtu.
 
😂😂😂

Changia tuu Bro
 
DUNIA INAOGOPESHA ILA WEWE USIOGOPE 02! MAISHA SIO MASHINDANO

Anaandika Robert Heriel,

Umekata tamaa, hauna tumaini, mambo yote yameenda Kombo, kila ulichokuwa unakitumainia kimekusaliti, kila uliyekuwa unamuamini amekugeukia, dunia imekupiga kikumbo, hakuna yeyote aliye Kwa ajili yako! Loooh! Hayo ndio Maisha!

Maisha yanaogopesha Kwa sababu wengi huisubiri kesho, wakati kesho haipo Kwa ajili Yao. Kwa maana ya Leo huishia leo, na yakesho ni kwaajili ya hao watakaokuwako kesho.
Tena Kama ilivyo kesho ndivyo zilivyo Akili za watu. Usiitegemee kesho usije ukaona utisho wa Dunia.

Dunia inaogopesha Kwa sababu wengi huwategemea Watu, utamtegemeaje mtu usiyejua anachofikiri, hujui ayawazayo moyoni mwake. Ndio maana nikasema kuitegemea kesho ni Sawa na kumtegemea mtu.

Usiogope, usikate tamaa, ishi maisha yako.

Dunia inaogopesha pale utakapoishi maisha ya watu wengine.
Kutaka mazuri waliyonayo wengine, ilhali wewe na wao mpo tofauti.

Unasoma ili uwe kama Fulani,
Unasomesha watoto ili wawe Kama Familia fulani,
Nakuhakikishia Dunia itaku- suprise,
Matokeo yake yatakutisha na utapoteza shabaha ya kuishi, utaogopa na kukata tamaa.

Soma ili uwe wewe uliyebora, sio uwe kama wengine ili baadaye ujipende na wala sio ujipendekeze
Somesha watoto ili wawe wao sio wawe Kama familia Fulani, ili uwapende watoto wako na sio kuwalaumu Kwa sababu yeyote Yule afanyaye Jambo lolote Kwa mtoto wake Kwa kuwalinganisha na wengine hatawapenda watoto wake Bali atawalaumu.

Taikon hata mambo nimeyapima, tena nimeyatolea hesabu iliyo kamili, ni hiyari yako kunisikia au kuyapuuza.

Kama utatafuta pesa, zitafute Kwa ajili yako mwenyewe, wala sio Kwa ajili ya watu wengine. Tena sio ili uwe kama fulani, Bali uwe wewe katika ubora wako. Kwa maana lengo la maisha Kwa kila mtu ni kuishi maisha yake.
Lakini dunia imekuwa uwanja wa vita Kwa sababu watu hutafuta Kwa ajili ya watu wengine.

Tafuta pesa Kwa sababu unazipenda na nihitaji lako binafsi. Usitafute sifa Kwa watu wengine.
Hiyo ndiyo namna ya kuishi Kwa Furaha na Amani. Kuishi kwa Yale unayoyapenda, bila kujali wengine wanayaonaje.

Heshima ya mtu haijengwi Kwa kuwapendeza wengine, heshima ya mtu inajengwa Kwa mtu kuishi maisha yake bila kuathiri maisha ya wengine.

Vijana wa siku hizi wapo katika mtihani mzito Kwa sababu wanahangaika kutafuta mambo Kwa ajili ya wengine,
Hawatafuti pesa Kwa sababu Yao wenyewe, Bali hutafuta pesa ili wapate heshima wasijue heshima ya mtu hutoka ndani yake na wala sio nje.

Kijana, nisikie Mimi Taikon, pesa hazitakufanya uheshimike bali zitakufanya ujione Kama unaheshimika, unisome unielewe.

Kadiri unavyozitafuta pesa ndivyo unavyozidi kuwa mhitaji, kadiri unavyozipata ndivyo na mahitaji yako yanakuzidi.

Sisemi usitafute Pesa, Ila nasema tafuta pesa Kwa ajili yako mwenyewe, wewe na familia yako. Hapo ndipo utazifurahia.
Maisha sio mashindano.
Maana wivu ndio huleta mashindano, na wivu husababishwa na tamaa mbaya.

Usiolewe Kwa sababu ya watu wengine, Olewa Kwa sababu ni hitaji lako, unampenda na upo tayari kuanzisha familia.
Usiangalie wengine wanasemaje au wanafanyaje, ishi maisha yako lakini usisahau kanuni ya Asili ambayo ndio inalinda utu wako na kukutofautisha na Wanyama.

Usifuate mkumbo!

Fanya harusi vile uonavyo wewe na sio Kwa kuangalia wengine walifanyaje, usijitese.
Kusherekea sio lazima uite Watu wengi au kukodisha Ukumbi au kuita magari mengi na wapiga tarumbeta. USIWE MTUMWA WA MAISHA YAKO, Acha maisha yakutumikie wewe na sio wewe uyatumikie.

Dunia inaogopesha Kwa sababu Wazuri wanawaogopa Wabaya,
Wenye akili wanaongozwa na Wajinga,
Wenye Haki wanaamuliwa na Waovu,
Wenye macho wanaonyeshwa njiwa na Vipofu,
Watu wema wanajificha vichakani na Watu Wabaya wakipita Kwa kujiamini barabarani,

Wenye maarifa huona aibu kuyatoa maarifa Yao Kwa jamii, lakini wapumbavu hutoa upumbavu wao Kwa jamii bila haya.

Dunia inaogopesha Kwa sababu,
Wazazi wanawategemea watoto ambao wao ndio walipaswa wategemewe,

Wanaume wameacha kuwaongoza Wanawake.

Hata hivyo zingatia,
Hata kama ungesoma mpaka wapi lakini Dunia inahitaji Akili ya kuzaliwa ambayo huwezi kuisomea,

Hata kama Ungekuwa mzuri Kama Malaika wa Tibeli, ndoa halindwi na uzuri isipokuwa Hekima na busara. uzuri unachakaa lakini hekima na busara havichakai.

Hata kama ungekuwa Mbaya wa Sura Kwa kiwango gani, Dunia inahitaji uthubutu kupata yaliyo mazuri.

Mwisho, Hata ungepata kila kitu, lakini Moyo unachohitaji ni Furaha, na furaha inapatikana Kwa kuishi katika wewe na sio kuishi Kwa kumuangalia mtu mwingine.

Ndimi, Taikon kutoka Nyota ya Tibeli, Nyota yenye Mbawa mbili irukayo kutoka Ulimwengu huu mpaka ulimwengu mwingine.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ahsante
 
Umeongea funzo kubwa sana ambalo vijana wa Dunia ya sasa tunapaswa kujifunza .
Ubarikiwe Kaka✊✊
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom